Jenerali Ulimwengu na makala zake

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Nimejaribu ku-attach makala kuhusu maelezo ya Jenerali Ulimwengu jana Chuo Kikuu Dar.

i285_Jenerali1.jpg
 
Jenerali anapoint, nilishangaa sana kumsikia JK anasema vijana wasitumiwe kwa manufaa ya wachache wanaotaka madaraka.

Mbona yeye kawatumia vijana kwa kuwapa ahadi hewa wakamchagua na sasa kila siku anatesa kwenye mapipa kwenda Europe.

Hawa jamaa waache usanii, wanasomba mali zetu kwa kisingizio cha amani na utulivu. Rushwa ya sasa haina hata chembe ya aibu, wanafakamia hawa,

Nchi itatumbukizwa kwenye Vita na hawa wafakamiaji rushwa, nionavyo mimi JK hawezi kukemea hawa maswahiba wake na ninawasiwasi na uadilifu wake. Simwamini.
 
..nimesoma kidogo juu ya alichoongea jenerali.

..pamoja na kwamba ni ukweli,lakini,hivi yeye yuko chadema nowadays?

..ni swali tu!
 
..nimesoma kidogo juu ya alichoongea jenerali.

..pamoja na kwamba ni ukweli,lakini,hivi yeye yuko chadema nowadays?

..ni swali tu!


He! Siku hizi kila anayeongea mambo mazito sharti awe Chadema?
Kila mtu bila kujali itikadi ana uhuru wa kutoa mawazo yake.
 
Hume I think the message is clear, kwamba huu si ubishi tena kuwa CHADEMA ndo wanaonekana kwa sasa kuwa ni chama ambacho kian poits na kinchogusa maswala mazito yanayowagusa watanzania.CCM kwa vile wameamua kukumbatia ufisadi na rushwa hawawezi tena kuwa points,by the way kina Jenerali na weingie kama yeye wamekuwa wakosoajo wa serikali zilizoko madarakani long before Zitto Kabwe and Dr. Slaa came into the political scene ila tu kuwa wote wamejikuta wanaongea lugha moja:Ukombozi kwa mnyonge wa nchi hii ambayo ndiyo lugha ya Mwl. Nyerere (RIP) mpaka anaingia kaburini...
 
Naam ulimwengu yuko sahihi kabisa unajua ata Rwanda na Burundi kuanza kupigana hawakuanza na mambo mazito mno ni mambo haya haya as a result mnaamsha hasira kwa watu na ndo mwanzo wa kupigana.
Upole wa watanzania si wa kuubeza ila siku wakichaluka viongozi kazi mnayo.Na moto ndo ushaanza huo,aluta continua
 
Sasa wasomi mnaanza kunigusa kidogo.
Niliwahi kuuliza maswali yafuatayo huko nyuma kuwa wasomi wetu wako wapi wakati nchi yetu inaliwa na mafisadi? mbona hatuwasikiii? au kelele zao ni pale tu wanapotaka nyongeza ya posho za malazi na chakula? mbona hatusikii sauti zao? Hivi kweli ni Shivji tu na Baregu ndiyo wanayo midomo au?....
Lakini sasa angalau naanza kusikia sauti zao toka pale sehemu ya mlimani na kwingineko! hivyo ndiyo mnavyotakiwa kuwa!..simameni kidete kutetea, kuelimisha,kulinda,na kupigania maslahi ya wanyonge na walio wengi!! tunatambua kuwa nyinyi mnajua ila kusema ndiyo bado mnaogopa.
Wembe.
 
..nimesoma kidogo juu ya alichoongea jenerali.

..pamoja na kwamba ni ukweli,lakini,hivi yeye yuko chadema nowadays?

..ni swali tu!

Hivi kila Mtu mnayemuona yupo Tofauti na Mambo ya serikali mnamuona kuwa ni Chadema?.Basi kwa Mwendo huo Mzee Mwinyi,Prof.Shivji na Judge Bomani wote ni Chadema.

Nafikiri suala zima la Uongozi Mbovu, linaonekana kwa watu wa vyama vyote!Kinachotoa msukumo kuzungumza hapo ni Utanzania na si Itikadi ya vyama vyao.Tuzungumze kama Watanzania na si Ucuf au Uchadema!!
 
Hivi kila Mtu mnayemuona yupo Tofauti na Mambo ya serikali mnamuona kuwa ni Chadema?.Basi kwa Mwendo huo Mzee Mwinyi,Prof.Shivji na Judge Bomani wote ni Chadema.

Nafikiri suala zima la Uongozi Mbovu, linaonekana kwa watu wa vyama vyote!Kinachotoa msukumo kuzungumza hapo ni Utanzania na si Itikadi ya vyama vyao.Tuzungumze kama Watanzania na si Ucuf au Uchadema!!

..mkuu,i was wondering out loud!that's all!kama umenisoma vizuri!

..kwani?butiku naye chadema?

..btw,hamtaniwi?au ndo mko serious mnapandikiza chuki?[no offense!]
 
Nampongeza jenerali Ulimwengu kwa kauli zake nzito juu ya usanii wa serikali yetu.
Kama alivyosema Ibambasi ni kweli kuwa Jenerali amekuwa mwanaharakati wa kuikosoa serikali tangu muda mrefu hata kabla ya akina Slaa na Kabwe kujulikana. Naweza kusema magazeti yao hasa RAI ndiyo yaliyonifanya nikawa mwanaharakati wa mabadiliko.

Lakini magazeti yale siku hizi yamekuwa ya kutetea utumbo wa serikali. Nasikia yamenunuliwa na Rostam Aziz, ni kweli? Waandishi wake isipokuwa Jenerali na Johnson Mbwambo, wamekuwa wapambe wa serikali na nina wasiwasi kwamba ndo maana Salva Rweyemamu kapewa cheo ikulu. Tusubiri huenda Gideon Shoo naye anatafutiwa cheo.

Lakini kama kina Jenerali waliishiwa mtaji kwa nini hawakutuomba wasomaji wao tukanunua hisa kuliko kuliuza gazeti kwa List of Shame?
 
kwa kweli Jenerali yuko right kabisa,yeye mbona alituahidi vijana ahadi hewa?
 
jenerali ni mwandishi, anasahili pongezi sawa tu na waandishi wengine na si zaidi

pongezi za ziada na wapewe kina mwinyi kwa kusema maovu ndani ya chama chao
 
Hume Bwana hapo na tofautiana na wewe kidogo tu. Hivi sasa umeibuka mtizamo kwamba mtu anye-challenge uozo na uvundo wa watawala wetu, anabatizwa na kuwa mpinzani. Nadhani hizo ni slogan za CCM, maana tumekuwa tukiambiwa wapinzani hawafai wanataka kuvuruga amani. Sasa kichekesho,amani bila tumbo kushiba ni amani gani?vijana wetu wanaoshinda barabarani bila kazi na wala hawajui watakula nini, au kulala wapi hao wanaamani?wanavijiji huko mambo magumu, huduma za msingi hakuna, wanalala giza, wanashinda njaa, wanatembea kilomita kadhaa na mgonjwa mabegani na huduma hakuna katika dispensari hiyo ni amani? pembejeo hakuna, mazao wanavuna kiduchu raha iko wapi? Kuna siku wataona hakuna cha kupoteza, twende tukale nao hizo nyama choma waliko huko oysterbay, masaki, mikocheni na kwingineko hapo nadhani hapatakalika
 
Ni kweli kuwa Jenerali ulimwengu amesema kweli kuhusu falsafa nzima ya uongozi halisi wa nchi hii. Mie napenda kumpongeza kwa hilo na kwa ushujaa alio uonyesha.
Nadhani wasomi wa nchi hii wana la kujifunza kutoka kwake, na nina jaribu ku-imagine kama Pro. Chachage angekuwa hai, hapo mlimani pangekuwa hapatoshi siku hiyo.

Bravooooooooo Ulimwengu .
 
Hume, what we're stressing at the moment is not who is belong to chadema or ccm. The subject matter is who had or continued to sphoning our very limited resources. The ruling government(leaders) and their associates should be responsible for our cry. I think we need to discourage and throw away the defence mechanism which they always employed when people demanding them to fulfill what they had pledged during the general election. This defence mechanism is nothing than preaching 'peace and tranquility'. Guys are you ready to cheers up while your stomach is empty?Are you ready to to see our mothers, fathers, children, brothers and our sisters die out there because of lack of medical services in our dispensaries? Are you ready to stay idle without utilizing your professions because of fisadis? why should we watch our wealth being scrambled, plundered, and abused by fisadis? Let us shout to them, our joint marginalized voices is power. Remember, for them, have coercive instruments like police, judiciary, prisons, national security, forces etc. We, don't have such instruments, the only weapons which we have is our jointly voices
 
Interesting indeed. Nimesoma article ya Ulimwengu ya jana nimeona niwasheheeshe. Anasema tunahitaji mambo manne kuendelea nayo ni uongozi bora, uongozi bora, uongozi bora na uongozi bora. Kisha anatoa sifa za kiongozi bora, halafu anatoa homework kuwa baada ya kusoma sifa hizi, kila msomaji ajiulize alikutana lini na kiongozi bora Tanzania?

Katika sifa zote imenigusa zaidi hii ya bidii ya kujielimisha kuhusu mambo ya jamii, taifa na dunia kwa ujumla. Swala la ujuzi na ujuvi. Hapa kwa kweli naona moja kwa moja alikuwa anamlima Makamba na viongozi wa CCM kwa ujumla. Hawa jamaa ni wazembe sana, hawajisomei wala kujielimisha ndio hufanya maamuzi halafu ndio wanatafakari baada ya kitendo. Ni problem kwelikweli.

Please nawe soma and let's discuss.
_______________________________________________________________

Here we go:
________________________________________

Uongozi tu, basi


MANTIKI ya msingi kabisa katika hayo niliyosema wiki iliyopita ni kwamba ili tuweze kuendelea tunahitaji vitu vinne: Mosi, uongozi bora, pili, uongozi bora, tatu, uongozi bora na nne, uongozi bora.

Basi.Vingine, kama nilivyosema, tunavyo, kuacha siasa safi, ambayo haina budi kutokana na uongozi bora. Hili ndilo suala litakalotusumbua kwa muda mrefu, na kabla ya kulidurusu ipasavyo na kulipatia ufumbuzi, hakuna matumaini ya kupiga hatua yo yote ya maendeleo. Tutaendelea kusuasua na kubabaisha; tutakimbilia kunukuu mafanikio ya kitakwimu na maliwazo ya sifa za kinafiki za "wafadhili", lakini hatua endelevu za kimaendeleo hazipigwi katika mazingira yaliyokosa uongozi bora.

Sasa inabidi kujadili dhana yenyewe ya uongozi bora, kwa sababu kwa jinsi tulivyoivuruga dhana ya uongozi katika nchi hii haitashangaza iwapo tutashindwa kuelewana kuhusu dhana yenyewe.

Iwapo nafasi nyingi zinazoitwa za uongozi zimekamatwa na walaghai, matapeli mabazazi na mafisadi, nadharia juu ya ‘uongozi' itasaidia nini wakati wananchi wamekuwa wakiona sifa mbovu na matendo machafu ya hao wanaojiita viongozi?

Hata hivyo hatuna budi kuendelea kukumbushana kuhusu sifa zinazotakiwa kuambatana na uongozi. Ni kitu gani kinachomfanya raia au mwanajamii awe kiongozi, tofauti na raia au wanajamii wengine?

Hapana shaka kwamba haya nitakayosema hapa ni yale yale yaliyosemwa miaka yote hii. Lakini ukweli ni kwamba matendo yetu hayaendani kabisa na sifa hizi ninazozizungumzia . Namwalika msomaji azipitie tena sifa hizi, halafu aamue mwenyewe ni lini mara ya mwisho aliwahi kukutana na kiongozi.

Kwanza kabisa hana budi kuwa na sifa kadhaa ambazo zinampambanua na wengine, sifa zinazowafanya raia na wanajamii wengine wamwone kama mfano wa kuiga, kama funzo la kujifunza, kama njia ya kufuata.

Hii ina maana kwamba ana hulka, tabia, mwenendo, na lugha ya uungwana; anao uadilifu mkubwa katika kufuata maadili yanayoiongoza jamii; hana ubinafsi na yuko tayari kujitolea kuwasaidia wanajamii wenzake, hata kama kufanya hivyo kutamtwisha gharama, kumpotezea muda au kumsababishia matatizo mengine.

Pia ni mjuzi wa mambo, kwa kuwa anajibidiisha kujielimisha na kujipatia taarifa ambazo zinamwezesha kujua mwelekeo wa jamii yake, nchi yake na dunia nzima, na sifa hii inamwezesha kuwa na msaada kwa jamii yake. Kuongoza ni kuonyesha njia, na ili mwanajamii aweze kuwaonyesha wenzake njia, hana budi kuwa na ari na uwezo wa kutaka kujua na kuweza kukieleza hicho alichokipata kwa ufasaha ili wenzake wamwelewe na, kwa kumfuata, wanufaike nacho.

Pamoja na ujuzi wake na uwezo mkubwa wa kupata taarifa na maarifa kiongozi wa asili hajengi kiburi kinachotokana na kujua, na wala hawaonyeshi dharau wenzake kwa sababu anajua kwamba hata mwanajamii asiyejua mambo mengi naye anao mchango wa kutoa.

Kwa hakika busara kubwa za kijamii zimesinzia ndani ya wanajamii wenye akili za kawaida tu, ambazo zinasubiri kiongozi wa kweli azitambue, azitekenye na kuzileta nje, kisha aziunganishe pamoja ili kujenga busara ya pamoja ambayo haiwezi kulinganishwa na busara za mtu mmoja, hata zingekuwa kubwa kiasi gani.

Kiongozi asilia hapendekezi jina lake, wala hajitokezi kusema anataka kuwa kiongozi. Kiongozi wa kweli huonekana na kutambulika ndani ya jamii yake, na akiisha kutambulika, hubebeshwa majukumu ya uongozi, na mara nyingi atasita kuyakubali majukumu hayo, kimsingi kwa sababu anajua kwamba ni mzigo anabebeshwa, si nafasi ya kula anayopewa. Anajua kwamba uongozi rasmi, tofauti na ule wa kujitolea bila kuwa na ofisi, una maana kwamba atakuwa na muda kidogo zaidi wa kushughulikia mambo yake binafsi, na biashara zake zinaweza zikaathirika.

Aidha kiongozi ni mtu mwenye misimamo inayoeleweka na kutabirika. Kutokana na jamii anayoiongoza, kiongozi anakuwa na misimamo kuhusu mambo yote makuu na muhimu yanayoihusu jamii yake, na misimamo hii haina budi kutabirika, ili anaowaongoza wasilazimike kubahatisha au kupiga ramli ili kujua msimamo wake utakuwa upi kuhusu suala la msingi.

Katika umoja wa majizi, mathalan, wezi wote watajua kwamba kiongozi wao akipewa taarifa kwamba mmoja wao amevunja benki na kuchota mamilioni ya shilingi, atampongeza na kumpandisha cheo, kumfanya jambazi mfawidhi.

Lakini akijua kwamba mmoja wao anawasiliana na polisi ili kuusaliti umoja wake wa wezi, atamchinja.Huyu ni kiongozi. Anatabirika.

Katika umoja wa watu walioapa kuitumikia nchi yao na watu wake na wakasema "Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie", iwapo kiongozi atapewa taarifa kwamba mmoja wa watu wake walioapa hivyo anafanya mambo yanayohujumu nia yao ya pamoja ya kuitumikia nchi, kisha watu wasijue atachukua hatua gani dhidi ya msaliti huyo (kwa kuwa msaliti mmoja aliwahi kufungwa lakini wasaliti wengine wakapandishwa vyeo) huyo si kiongozi, kwa sababu hatabiriki, ni kigeugeu, hana msimamo.

Kutabirika huku kunakwenda sambamba na ujasiri. Mtu asiyetabirika ni mwoga anayebadili msimamo wake kila mara kutegemea amekabiliwa na nani na ana maslahi gani kwa wakati huo. Kutokana na woga atasema maneno tofauti katika nyakati tofauti kwa watu tofauti ili kumpendeza kila mmoja. Tofauti yake na malaya ni biashara wanazofanya, lakini mwenendo ni sawa sawa.

Katika mazingira yetu nchini na barani Afrika ni dhahiri tunahitaji uongozi wa aina fulani, lakini imekuwa vigumu mno kuupata. Tunahitaji uongozi wa kujitoa mhanga, kwa sababu hali yetu ni mbaya, kama nilivyosema mapema, na inazidi kuwa mbaya; watu wetu wanateseka na umsikini ambao hauelezeki tukiangalia raslimali zilizowazunguka; ipo hatari ya kweli ya watu wetu kufikia hatua ya kusema, "Ah, liwalo na liwe, tumechoka na hali hii!"

Dalili zinajitokeza taratibu, lakini watawala wetu, kwa ustadi wao wa kubeza, uliochanganyika na "shibe mwanamalevya" hawatambui alama za nyakati.Wanabeza bila kujua kwamba wanaibeza Historia. Wakija kulitambua hilo, jua litakuwa limekuchwa.

Nchini mwetu utapeli, ubazazi na ubabaishaji vimo ndani ya vyama vyote vya siasa, kama ulivyo ndani ya shughuli nyingine nyingi za kitaifa: biashara, michezo, mapenzi, hata imani za kiroho. Kwa hiyo ninapozungumzia utapeli wa kisiasa nisije nikaeleweka kwamba nataka kukisema chama tawala pekee.

Hata vyama vya upinzani vinao matapeli wengi tu, na baadhi yao ni hao popo wanaohama kila uchao, leo wapinzani wakali wanaokitukana chama tawala kama samaki waliooza, kesho ndio hao hao "wanaorejea" chama tawala (hata kama hawakutoka huko awali) na kupokelewa kwa nderemo na kuwa "makada waandamizi" wa chama hicho wanaogeuzia matusi yao upande ule ule walikokuwa wakitambia jana. Na wala hawaoni haya.

Hapana, matapeli wako kote katika vyama vyetu. Lakini chama tawala hakina budi kukubali kubeba jukumu zito zaidi kuliko vyama vingine; hivyo iwapo katika maandishi yangu haya nitakitaja mara nyingi ieleweke kwamba CCM ndiyo chama kikongwe kuliko vyote na ndicho kilichotafuta na kufanikiwa kupewa dhamana ya kuliongoza Taifa hili.

Aidha chama hicho kimejenga tabia ya kutamba kwa jeuri ya "chama tawala", na kinayo haki ya kutamba, sawa sawa na baba alivyo na haki ya kutamba kwa kuwa mkuu wa familia. Pamoja na haki hiyo ya kutamba, chama hicho hakina budi kuelewa kwamba kina majukumu makubwa ya kulipa Taifa hili uongozi makini, sawa na baba alivyo na majukumu mazito ya kuiongoza familia yake na kukidhi mahitaji yake.

Iwapo baba atashinda klabuni akitambia ubaba wake, akasahau kushughulikia chakula, matibabu na elimu ya mkewe na wanawe, kuna siku atajikuta si mume wala baba tena, na familia yake inahudumiwa na mababa wengine, ambao anaweza baadaye akawaita "wafadhili".

Si tofauti kwa chama kinachoshinda katika ulevi wa mikutano ya kujisifu na karamu za kusherehekea nini sijui, huku nchi inateketea kwa umasikini usioelezeka katikati ya utajiri mithili ya El Dorado, halafu nchi nzima inawekwa chini ya "ufadhili" wa mababa tusiowajua.

Mnamo mwaka 1993 nilijikuta katika kundi dogo lililokuwa likijadili masuala mbali mbali ya kisiasa na muasisi wa Chama Cha Mapinduzi, Mwalimu Julius Kambarage.

Siku moja Mwalimu alitusimulia yaliyomkuta miaka ya 1986 na 1987 alipokuwa katika zoezi aliloliita "Mradi wa Kuimarisha Chama," baada ya kuwa amestaafu urais mwaka 1985.

Anasema baada ya kutembelea wilaya zote nchini na kukutana na viongozi wa ngazi zote za uongozi wa chama, na kuwaangalia vizuri wale viongozi, na kuwasikiliza wakitoa taarifa, wakijenga hoja au wakijibu maswali yake, anasema alifika mahali akajiuliza swali: "Hivi hawa, pamoja na mimi, tumo ndani ya chama kimoja?"

Hali aliyoiona Mwalimu haijabadilika isipokuwa kama ni kuwa mbovu zaidi.
 
Asante Kitila kwa hii article ya Ulimwengu.
Kwa kweli bado naendelea kuipitia maana inaonekana kweli Jenerali amerudi ulingoni!

Thanks!
 
Niliisoma jana na nilivutiwa na mawazo ya kiongozi aweje. Binafsi nina maoni tofauti kidogo kwani sifa za kiongozi anazozisema ni zile ambazo watu wataziona matokeo yake. Binafsi ninaamini kuna kitu kimoja tu kinachomfanya kiongozi awe kiongozi na kutoka hapo vingine vyote hufuata. Kwa hakika siyo elimu, siyo kuwa mkweli, siyo kujali watu n.k kuna kitu kimoja..
 
Niliisoma jana na nilivutiwa na mawazo ya kiongozi aweje. Binafsi nina maoni tofauti kidogo kwani sifa za kiongozi anazozisema ni zile ambazo watu wataziona matokeo yake. Binafsi ninaamini kuna kitu kimoja tu kinachomfanya kiongozi awe kiongozi na kutoka hapo vingine vyote hufuata. Kwa hakika siyo elimu, siyo kuwa mkweli, siyo kujali watu n.k kuna kitu kimoja..

Mzee wa kijiji bwana! kipi hicho? mbona watuweka roho juu??

Kwa Ulimwengu Bravo Mkuki umerudi mahali pake! Hapa ni kumkoma nyani hadi uswahilini si mtandaoni tu!

Kumekucha Bongo!.
 
Back
Top Bottom