Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 738
- 478
Akitoa salamu za rambirambi Waziri Stergomena Tax aliwasilisha salamu za pole toka kwa Amri Jeshi Mkuu Daktari Samia Suluhu Hassan, kwa kusema kuwa Serikali pamoja na jeshi limepoteza Kamanda na Kiongozi muhimu kwani wakati wa uhai wake marehemu alitumikia jeshi katika nafasi mbalimbali kwa mafanikio makubwa ambapo ametoa wito wa kuiga yote mambo mema na uchapakazi aliounyesha Marehemu Meja Jenerali Gimonge (Mstaafu).
Viongozi wengine waliohudhuria tukio hilo ni pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Majenerali, Maafisa Wakuu, Maafisa Wadogo, Askari pamoja na waombolezaji, ambapo mwili wa Meja Jenerali Gimonge umesafirishwa leo kwenda Mkoani Mara kwa maziko.