Jenerali Ulimwengu: Kuhusu Mfumo wa Serikali,Tuna jidanganya Hatuoni Tatizo

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,319
24,218
25 November 2023

Jenerali Ulimwengu - "Kuhusu Mfumo wa Serikali,Tuna jidanganya Hatuoni Tatizo"

View: https://m.youtube.com/watch?v=PWrarDLQBCA
Kuongezeka mikoa na wilaya kila siku Jenerali Ulimwengu anasema kuwa kwa kumulika kurunzi yake kwa wakuu wa mikoa 29, wakuu wa wilaya 123, wakurugenzi wa wilaya 123, wakurugenzi wa mawizara 52 na 'wateule' wengine wa rais, wateule hao wote rais hawajui maana siyo Mungu wa waHindu mwenye vichwa kadhaa na miguu isiyo na idadi kuwa na uwezo wa kuwafikia wateule wake kuwatathmini utendaji kazi wao, ripoti zao wanazomsomea akiwa wilayani ktk ziara. Teuzi hizi zimeanzia tangu kina Mzee Joseph Butiku wakiwa wanatumia awamu ya kwanza na kuendelea hadi sasa ...

Jenerali Ulimwengu asisitiza ili tupate maendeleo makubwa katika nyanja zote lazima tubadilishe utaratibu wa kujitawala na pia kuwashirikisha wananchi kuamua kwa kuchagua viongozi ktk maeneo badala ya kumtwisha rais majukumu hayo wakati hao maRC na maDC pia maDED hawafahamu .....

Hayo yamejiri leo katika paper zilizowakilishwa leo katika shughuli ya tatu iliyoandaliwa na Taasisi ya Maalim Seif Foundation ambayo imeandaa mkutano Zanzibar katika kuuenzi mchango wa Maalim Seif Hamad katika uongozi Tanzania. Kauli mbiu ya mkutano huu ni Siasa, Uongozi na Utawala:Tumekosea Wapi, Tujisahihishe Vipi? Kiongozi wa chama cha upinzani cha South Afrika Build One South Africa, Mmusi Maimane ni mgeni mwalikwa katika tukio hili...

Fuatilia paper hizo zinazoweza kusaidia mfumo wa Siasa, Uongozi na Utawala nchi Tanzania kubadilishwa kuwa wa manufaa kwa wananchi wote

Source : The Chanzo
 
Fuatilia paper hizo

Source : The Chanzo

asante baba!
 
Balozi Ali Karume ashindwa kujizuia anyanyuka

View: https://m.youtube.com/watch?v=kuTBi5UhKIs

The imbecilization ni noun na adjective inayomaanisha kujiweka katika hali ya kuwa hamnazo. Wanaposema sheria imetungwa kwa hiyo ni halali na imeidhinishwa na bunge, je bunge hilo ni halali au wanajifanya hamnazo....

Je kila kitu kinachoamriwa na mtawala kinakuwa sawa? Lazima tutafakari maamuzi ya viongozi, wabunge n.k siyo kukubali kila jambo ...
 
Mwalikwa kutoa Afrika ya Kusini anena mazito - Wakoloni weusi walioleta uhuru ambao wanafilisi nchi, wakati umefika waondolewe madarakani

Kiongozi wa chama cha upinzani cha South Afrika Build One South Africa, Bw. Mmusi Maimane ni mgeni mwalikwa katika tukio hili.

View: https://m.youtube.com/watch?v=f05tzmVoHTk

Maimane said its time to liberate Africa from the former liberators who have become corrupt.

Build One South Africa is a South African political party. It is led by Mmusi Maimane, the leader of the One SA Movement and the former leader of the Democratic Alliance. The deputy leader is Nobuntu Hlazo-Webster, founder and convener of the South African Women’s Commission.
 
Prof. Kitila Mkumbo ndio habari ya mjini aise...

anajua ku constract na ku deconstract hoja kwa hoja kwa umahiri wa kipekee sana.

Na kwa stahili ile hawezi pendeka kabsaa mbele za wasio na hoja
 
25 November 2023
Arusha, Tanzania

WANANCHI WALALA NJE OFISI ZA MKOA WAKIFUATILIA HAKI ZAO

View: https://m.youtube.com/watch?v=nYjIduljyEw
Viongozi wajuu wa serikali na chama walioteuliwa na Rais aliye pia mwenyekiti wa CCM wawapiga chenga wananchi na hivyo mamia ya wananchi waamua kulala ktk ofisi za CCM Mkoa Arusha kushindikiza haki yao ...
 
Kitila Mkumbo: CCM ni Chama cha Siasa Ambacho Kinaingia Katika Uchaguzi Kusaka Dola
Sentensi ya hovyo sana hii kwa kila namna utakavyotaka kuiangalia.
CCM hawaingii katika uchaguzi kusaka Dola, bali wanatumia Dola kuvuruga chaguzi.
Ni aibu kwa mtu anayetumia cheo cha hadhi ya u-profesa kutamka maneno ya hovyo namna ile bila kujali tafsiri hasi mbalimbali zinazoendana na maneno hayo.

Hakutumia kichwa kuyatamka/kuyaandika maneno hayo.
 
BUNGE LILONGOLEWA MENO NA MFUMO MBOVU WA KISIASA,

Siasa sasa zinafanywa mitaani badala ya bungeni, sababu bunge lisilo halali haliwezi kuibana serikali au waziri na limekuwa bubu.

Mfano wafanyakazi wanaodai mafao yao huko Arusha hawana mbunge bungeni wanayemuamini, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa wala waziri na sasa wanadhani sarakasi za Paul Makona 'kutatua' kero kwa mikutano isiyo rasmi barabarani itawasaidia.

1701004252919.png
 
Ombwe la mfumo wa kiuongozi na utawala katika kuwezesha matokeo chanya Tanzania

Ipo siku bunge la wananchi ambalo halikai Dodoma litaamua kuwa na vikao vyao mitandaoni, vijiweni na chini ya mti vijijini na kuwa linasikilizwa zaidi kuliko bunge butu la kugonga, kusifia na kutukuza lililopo Dodoma chini ya CCM

Ni kufuatia sarakasi za mfumo wa uongozi butu wa serikali ya CCM unavyodumaza uhuru, haki na maendeleo ya watu katika maeneo yao.

1701004611925.png

Picha: Paul Makonda akiwasalimia wananchi matatizo yao.

Ukiona kuwa bunge linalotakiwa kufanya kazi ya kufuatilia matatizo, changamoto na shughuli za maendeleo kwa kuihoji, kuibana na kuiagiza serikali ichukue hatua lakini bunge lipo kimya kama limepigwa ganzi haliwezi kumuagiza waziri au kumbana likitegemea Paul Makonda au rais wa Jamhuri atekeleze maamuzi hadi ngazi ya mafao ya wafanyakazi wa kiwanda au tatizo la maji kijiji fulani katika nchi hii kubwa kieneo basi kuna tatizo kubwa la ki mfumo wa kiuongozi na kiutawala.

1701005054751.png

Picha : Paul Makonda, Katibu itikadi na mwenezi wa CCM akielekea kwenda kusikiliza kero za wananchi .
 
09 November 2023
Kagera, Tanzania

MAKONDA AONGEA Kama JPM AKIWABANA WAZIRI MBARAWA, WAZIRI wa UJENZI ....

1701006279565.png

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi, Paul Makonda, ametoa maagizo mbalimbali kwa Mawaziri wa wizara nne hapa nchini ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuwapigia simu mawaziri hao na kutoa majibu ya changamoto na kutatua changamoto hizo.

Mawaziri waliopigiwa simu ni pamoja na waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, Waziri wa mambo ya ndani Hamad Massaun, waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa.

Makonda ametoa maagizo hayo leo Novemba 9, 2023 wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara akiongea na wananchi mkoani Kagera uliofanyika uwanja wa mashujaa Mayunga.

“Waziri Mchengerwa nakupa miezi mitatu uwe umekanyaga kagera, nataka kuona mpango wa ujenzi wa soko, tafuta pesa kokote soko lijengwe, nataka kuona stendi ya kisasa ya kimataifa inajengwa Kagera pamoja na changamoto ya mto wa Kanoni imalizwe kwa kujenga kingo za mto huo.” alisema Makonda.

Makonda akizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mchengerwa alisema ameyapokea maelezo hayo na ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
 
26 November 2023

maoni na ushauri yanayotolewa kupitia kwa style ya monologue exclusive ndani ya media house ya the Chanzo, Nini kifanyike

Hali ya kiSiasa Tanzania

Jenerali Ulimwengu : Tulikotoka, Tulipofika, na Tunapoelekea Chini ya Rais Samia Suluhu

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZSwQsNgyeF0

Hali tuliyonayo sasa nchi ........ watu kushangilia mtu ... nani anamdhibiti nani ..... taratibu standing orders ..... rais kisheria / kikatiba hana mamlaka ya kuanzisha michakato mingi ..... kudra ya Mwenyezi Mungu ... Gari lisilojulikana kufuatafuata mtu ..... terror and atmosphere of fear .... mashaka ya vyeti ...... hakuna maelezo mpaka sasa kutoka kwa ofisa wa serikali ..... vyombo vya habari mass media vilihasiwa ...

Lakini sasa, tuliliwazwa ......
 
25 November 2023

Jenerali Ulimwengu - "Kuhusu Mfumo wa Serikali,Tuna jidanganya Hatuoni Tatizo"

View: https://m.youtube.com/watch?v=PWrarDLQBCA

Jenerali Ulimwengu asisitiza ili tupate maendeleo makubwa katika nyanja zote lazima tubadilishe utaratibu wa kujitawala na pia kuwashirikisha wananchi kuamua kwa kuchagua viongozi ktk maeneo badala ya kumtwisha rais majukumu hayo wakati hao maRC na maDC pia maDED hawafahamu .....

Source : The Chanzo

Hii ya teua tengua imelenga zaidi kuwapa popularity wateuaji hamna kitu kingine
 
Back
Top Bottom