Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Mimi nafikiri Ulimwengu angesema kuwa hajazisoma au hakubaliani na itikadi za vyama vya siasa vilivyopo sasa TZ. Kusema kwamba vyama havina itikadi ni dharau na wakati mwingine ni kujaribu prove a self fullfilling prophecy. Kuna watu hapa duniani hawawezi kuona jambo la maana linafanyika hadi wawe wameshiriki wao. Ninaogopa kusema kwamba Ulimwengu ni moja wao. Moja ya uthibitisho wa hili ni ukweli kwamba Ulimwengu ni mwandishi mzuri lakini baada ya Rai kutekwa nyara hakuandikia gazeti lolote hadi alipoanzisha gazeti lake tena. Hapa maanake ni kwamba hakuona gazeti lolote la maana baada ya Rai.