Jenerali Ulimwengu: Inanichosha kusikia sifa za Rais kila dakika

Ngurukia

JF-Expert Member
Feb 25, 2023
1,483
6,228
Ifikie wakati tuache kuona kila anachofanya Raisi ni msaada kwetu na si majukumu yake.

Hizi sifa za uongo zimekuwa nyingi mpaka kuondosha mantiki ya uhalisia wa utendaji wake.

Alichosema Jenerali Ulimwengu

"Mimi inanichosha kusikia sifa za rais kila dakika. Rais ni mtu mwema nadhani. Lakini sio lazima tukae tunamsifu! Tunamsifu!. Maana yake Mwisho kama hauna critical thinking juu ya mkuu wako na kila siku ni kumsifu. Naanza kuwa na shaka kwamba hata akikosea utamsifu tu. Na waswahili wanasema kufanya hivyo ni kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa au wanavyosema waswahili unamcheza shere"
 
Ifikie wakati tuache kuona kila anachofanya Raisi ni msaada kwetu na si majukumu yake.

Hizi sifa za uongo zimekuwa nyingi mpaka kuondosha mantiki ya uhalisia wa utendaji wake.
Wacha unafiki! Mbona watu wake Ulimwengu kwenye newsroom wanakutetemkia sana? Hiyo kumtukuza Boss ni very natural, essentially ni adabu njema, that's all.
 
Ni watu wachache wenye uwezo wa kumkosoa Rais huyu Jenerali ni mmoja wao.

Hana nia mbaya kwenye kukosoa kwake ila Machawa wa Mama sidhani kama watamuacha Salama.

Ilianza kama utani awamu ile, maana ilifikia wakati kuna Mhe. Mmoja alimsifia Mhe. RAIS hadi kufikia kumuita Mhe. MUNGU badala ya Mhe. RAIS 🙌
 
Back
Top Bottom