Jenerali Ulimwengu afunguka kuhusu Rais Mkapa

Jenerali Ulimwengu afunguka kuhusu Rais Mkapa

Jenerali ulimwengu nimesahau jina halisi ila punguzu chuki.
Chuki hawezi kukosa kwa sababu alimvua uraia huku akijua niraia halali wa Tz. Nisawa na wewe hapo uambiwe nimkongoman huku anaekuambia nirafiki yako wakaribu ambae ulimpigia kampeni mpaka akawa raisi nahuku anakufahamu fika wewe nimtanzania.
 
Kusema kweli kifo cha Mkapa hakijaniuma hata kidogo. Nakumbuka tu ushenzi aliofanya Mwembechai kwa watu wasio na hatia. So far Kiongozi pekee kama ikitokea akatangulia itaniuma kiasi fulani ni Kikwete peke yake! Nasema Kikwete peke yake! Labda aje atokee mwingine!
Mimi pia,yaani sijui naona aje. Kitu pekee positive nakiona ni alivyowapatanisha kina Mwai Kibaki na Raila. Hapa nchini sio au kwa vile alitawala tukiwa ma teenagers ?
 
Duh!

Naona Jenerali Ulimwengu na marehemu Rais Mkapa walikuwa hawapikiki chungu kimoja!


Umiliki wa makaa ya mawe Kiwira, kashfa ya ununuzi wa Radar, mtakula majani ila ndege ya rais itanunuliwa, NBC kubinafisishwa kwa bei ya kutupwa, mauaji zanzibar na Mwembechai .......
 
Jenerali ulimwengu nimesahau jina halisi ila punguzu chuki.
Jenerali kafanya chuki gani? Ningeelewa kama watu wangejibu hoja zake kuonyesha chuki, Hakuna!
Yeye alikuwepo na alifanya kazi na Mkapa na anamweleza kama alivyomfahamu.

Tubadilike ili viongozi watambue kuwa sasa si muda wa kusifiwa bali kuchambuliwa mazuri na mabaya

Nyerere watu walieleza pande zote, lakini, majority walikubaliana kwamba mengine hayakuwa ya kukusudia

Kiongozi akifanya jema tutaeleza, akifanya fyongo tutaeleza. Hililitasaidia wajue umma unawatazama vipi, si wakati wakiwa hai hata siku ya kuondoka.
 
Duh!

Naona Jenerali Ulimwengu na marehemu Rais Mkapa walikuwa hawapikiki chungu kimoja!


Walikuwa marafiki sana ila baadaye wakatofautiana na mmoja kupewa Unyarwanda! Nakumbuka kama wakati wa harakati za Ben kugombea Urais, Jen alikuwa kwenye timu ya kampeni. Siasa hazina rafiki wa kufumu ama adui wa kudumu.
 
Nimesoma karibia yote, mi nauliza NBC yetu, viwanda vyetu vilivyouzwa na kwenda kufanywa magodown mfano ceramic mbeya aliyonunua nsa kaisi na ni gofu, na viwanda vyote viko wapi ben, Nyerere wetu yuko wapi ben?

Ulimwengu aliteseka sana na uraia alikuwa na kiwanda cha magazeti pale sinza njiani sijui hata kiliishia wapi.

Benjamin ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyie wapemba acheni kulia lia,kwani mkapa alikuwa rais wa Zanzibar ? ,kosa ni lenu ,kwani rais wenu alikua na kazi gani ?
Inaonekana wkt yale mambo yanatokea kule Pemba ulikua mdogo sana au bado hujazaliwa.
 
Ukweli lazima usemwe. Mkapa alikuwa kiongozi mkatili sana ambae hakujali raia bali maslahi ya CCM tu.
Alikuwa rahisi sana kutoa amri za watu wauawe au wapotezwe kwa maslahi ya CCM na mfano ni mwembechai na Zanzibar mwaka 2001.

Hata mie kiongozi pekee akipatwa na jambo nitaumia sana labda Kikwete ambae ingawa nae alikuwa na mapungufu ila at least ana ubinadamu sana
 
Hivi Generali anaiva na nani?
Jakaya aliiva naye siku chache sana za mwanzonimwanzoni mwa utawala wake.
Labda JPM anaiva nae.
Alisha mchana live JPM kuwa amelirudisha nyuma taifa kwa miaka 100 kwenye femokrasia, pale alipo sema siasa zifanyike wakati wa uchaguzi.
 
Jenerali kaonyesha immaturity kubwa kwenye hii Interview.


Mkapa kipindi cha utawala wake Alidhibiti mfumuko wa bei, hata nauli ya daladala ilibaki shilingi 150 kwa muda mrefu sana kwenye utawala wake

Alipandisha kipato cha mtanzania kutoka dola 170 kwa mtu hadi 500 kwa mtu kwa mwaka.

Alijenga Taasisi imara, TCU, NHIF, NSSF, TANROADS, LOANSBOARD.

Alikuwa na Programmes za maendeleo kama vile MKUKUTA, Mkakati wa kuondoa umasikini Tanzania, MMEM Mpango wa Elimu ya Msingi, MEMKWA, MKURABITA

Ni Mkapa ndiye aliyewaita wenye magazeti ya Mwananchi na The Citizens waje wawekeze Tanzania

Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha TV ya Taifa (TBC1)

Ni Mkapa ndiye aliyetujengea uwanja bora kabisa na wa kisasa wa mpira hapa Dar

Pia alikuwa Jasiri kukiri makosa na kurekebisha, Serikali yake ilipounda Bodi ya Parole na kuweka wakiristo watupu, alikuwa wa kwanza kuona tatizo na immediately kuamua kuivunja na kuiunda upya.

Mitihani ya kidato cha nne ilipovuja kama njugu mwaka 1998, Aliifuta mitihani na kuleta mingine.

Waislamu walipolalamika kuwa hawajanufaika ipasavyo na matunda ya uhuru katika elimu, aliwapa majengo ya Tanesco wajenge chuo chao lakini wakati huohuo pia akabalance kwa kuwarudishia makanisa baadhi ya shule zao zilizochukuliwa na Nyerere

Sasa Jenerali Ulimwengu asilete chuki zake binafsi kwenye msiba wa mzee wetu.

Na kabla ya kuwa rais, Benjamin Mkapa alifanya kazi nzuri sana kama waziri wa. mambo ya nje kipindi cha Vita vya Kagera na pia alifanya kazi nzuri sana kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika

Mzee Mkapa katutoa mbali, Jenerali akae na chuki zake lakini tunayo rekodi nzuri ya kutukuka ya mzee wetu
Rekodi yako ukiulizwa uijibu tu wala hakuna tatizo. Ila yeye Ulimwengu amejibu rekodi aliyonayo yeye. Hatuwezi kila mtu kufanana mtazamo na wengine.
 
Ni Rais mzuri kama wengine, alijenga nidhamu kwenye serikali, aliharibu uchumi kupitia uwekezaji wa kukurupuka hili ameandika mwenyewe anakiri kwenye kitabu chake!!

ila Mkapa alichangia kufanya nchi kuwa masikini kupitia sera ya ujamaa, huyu alikuwa mjamaa kama Nyerere na Mkulu, i doubt if these excellencies understood/ understand what is ujamaa maana hata wazungu hawakuelewa falsafa ya Nyerere badala ya kuandika socialism wazungu waliacha ibaki Ujamaa!!

Mkapa Ni katika genge la viongozi lile lenye mawazo ya kikoloni mimi ninaloamini ni kikwazo cha maendeleo na litakwisha in 30 years na nchi hii itahamia CAPITALIS and english from chekechea to university na kupaa kiuchumi!!

Mkapa Ni mbaguzi wa kidini wa wazi manake hata Waziri Mkuu aliweka mkristo mwenzake!!

By the way amekufa kwa ugonjwa gani? tuambieni wanaojua.

Mungu amuweke mahali panapomstahili!!
Duhh mkuu ,English ndo inaleta maendeleo??
 
Back
Top Bottom