Jenerali Ulimwengu afunguka kuhusu Rais Mkapa

Ulimwengu ni kati ya watu muhimu sana hasa kwenye sector ya habari, tatizo ana chuki kubwa sana na walio madarakani, huwa nahisi kuna vitu personal vinaendelea kati yao ambavyo hatuvijui.

Tatizo ni kwamba wote wamesoma wakati mmoja wakiwa shuleni hivyo wanafahamiana nani ni nani na yule yuko vipi.

Kuna watu mkisoma wote halafu kesho wabadilika na kujifanya humjali hiyo ni shida.

Au unaamua kumdharau mtu ambae unafahamu wazi kabisa kuwa ana uwezo kuliko wewe kwenye maeneo fulani kwa kumuona yeye ni tishio kwako.

Kwa mfano Jenerali na marehemu Mkapa ni wajuvi wa lugha ya kiingereza hivyo hawawezi kubishana kwa hoja na mmoja akubali kushindwa.

RIP Mzee Ben.
 
Mkuu nchi yetu bado ni koloni la Tanganyika kiukweli hatujawahi kuwa na rais zaidi ya nyampara linalosubiri maelekezo kutoka kwa malkia Elizabeth wa Tanganyika
hahahaha😄 umeona sasa ? na kuna uwezekano hayo mauaji unayolalamikia huenda maelekezo alitoa nyampara na sio malkia elizabeth mweusi
 
Ulimwengu ni kati ya watu muhimu sana hasa kwenye sector ya habari, tatizo ana chuki kubwa sana na walio madarakani, huwa nahisi kuna vitu personal vinaendelea kati yao ambavyo hatuvijui.
Alipokwa uraia mpaka akaomba upya! Kabla ya hapo alimfanyia kampeni Mkapa na kumpamba kama Mr Clean
 
Jenerali kaonyesha immaturity kubwa kwenye hii Interview.

Mkapa kipindi cha utawala wake Alidhibiti mfumuko wa bei, hata nauli ya daladala ilibaki shilingi 150 kwa muda mrefu sana kwenye utawala wake

Alipandisha kipato cha mtanzania kutoka dola 170 kwa mtu hadi 500 kwa mtu kwa mwaka.

Alijenga Taasisi imara, TCU, NHIF, NSSF, TANROADS, LOANSBOARD.

Alikuwa na Programmes za maendeleo kama vile MKUKUTA, Mkakati wa kuondoa umasikini Tanzania, MMEM Mpango wa Elimu ya Msingi, MEMKWA, MKURABITA

Ni Mkapa ndiye aliyewaita wenye magazeti ya Mwananchi na The Citizens waje wawekeze Tanzania

Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha TV ya Taifa (TBC1)

Ni Mkapa ndiye aliyetujengea uwanja bora kabisa na wa kisasa wa mpira hapa Dar

Pia alikuwa Jasiri kukiri makosa na kurekebisha, Serikali yake ilipounda Bodi ya Parole na kuweka wakiristo watupu, alikuwa wa kwanza kuona tatizo na immediately kuamua kuivunja na kuiunda upya.

Mitihani ya kidato cha nne ilipovuja kama njugu mwaka 1998, Aliifuta mitihani na kuleta mingine.

Waislamu walipolalamika kuwa hawajanufaika ipasavyo na matunda ya uhuru katika elimu, aliwapa majengo ya Tanesco wajenge chuo chao lakini wakati huohuo pia akabalance kwa kuwarudishia makanisa baadhi ya shule zao zilizochukuliwa na Nyerere

Sasa Jenerali Ulimwengu asilete chuki zake binafsi kwenye msiba wa mzee wetu.

Na kabla ya kuwa rais, Benjamin Mkapa alifanya kazi nzuri sana kama waziri wa. mambo ya nje kipindi cha Vita vya Kagera na pia alifanya kazi nzuri sana kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika

Mzee Mkapa katutoa mbali, Jenerali akae na chuki zake lakini tunayo rekodi nzuri ya kutukuka ya mzee wetu
Upo kwenye urithi wa mzee wako!?
 
kujenga mifumo ya kiserikali,hii TRA tunayoiona leo
Kabla ya TRA kulikuwa na nini na walikuwa wanafanya nini?

Anyhow, Ulimwengu angetoa hizo shutuma kabla marehemu hajafa ingekuwa vema zaidi
 
Ulimwengu simshangai.... ameteseka sana na masuala ya "uraia" wake. Na tabu zake zilianza wakati wa Mkapa.
 
Namkumbuka Bwm vizuri kwa makubwa manne, Mkazo katika elimu na mkurabita, mkakati wa kupunguza deni la taifa nje, kesi ya Dibagula na mauaji ya zanzibar, UBINAFSISHAJI.
 
Duh!Naona Jenerali Ulimwengu na marehemu Rais Mkapa walikuwa hawapikiki chungu kimoja!
Rais Mkapa hawakupika hasa baada ya ile hoja kwamba Jenerali si Raia wa Tanzania.
Mkapa alijua ni Raia, kwa bahati mbaya 'intelligence ' walimshauri afanye fyongo na akakubali fyongo.

Kwa upande mwingine, Jenerali anajaribu kubadili mitazamo ya watu kuhusu marehemu.
Tumezoea kuwasifu marehemu hata watu kama akina Nkurunziza wenye '' mapipa ya damu' mikononi

Kwasasa tubadilike, watu waelezwe wasifu wao kama walivyotenda wakiwa hai. Jenerali anamuongelea Mkapa kama alivyomfahamu, hizi habari za sugarcoat si zama zake. Tumechoka kusifu hata wasiostahili kisa wametangulia.

Kwangu mimi bado narudia, kiongozi wa kitaifa ni Nyerere. Huyu alisimama kama baba wa Taifa hata baada ya kustaafu. Hawa waliofuata baada ya kuondoka Ikulu wamebaki kuwa makada wakereketwa bila faida kwa Taifa

Eti Rais Mwinyi anataka katiba ibadilishwe kisa mtoto wake ashinde Urais Zanzibar, halafu ipo siku kizazi kitatakiwa kiongelea mema yake na kufumbia macho uozo kama huo.!!! Hapana tutasema tu wakati ukifika

JK hasemi kwasababu kuna watu wana masilahi na chama. Ipo siku tutazungumzia ukimya wake

Kwa ufupi, mtu aelezwe kama alivyofanya wakati akiwa hai! halafu matendo na kauli zake zitapimwa na busara za wanaosoma au kusikiliza habari zake. Big up Jenerali
 
Nimependa maoni yako. Ana mazuri na mabaya pia. Alipenda sana kugomba wakati anahojiwa. Hakuheshimu wanahabari na vyombo vya habari. Alikuwa scholastic sana. Hakupandisha mishahara ya wafanyakazi kwa kipindi kirefu sana huku akihimiza kufunga mikanda. Kwa upande wa mifumo ya kiserikali alifanya kazi kubwa.
Nimesikiliza mpaka mwisho wa mahojiano na Jenerali amejibu kile alichoulizwa hasa kuhusu maoni yake.Hayo ni maoni yake na nakumbuka kuwa kwa kipindi chote cha utawala wake hakuwahi kufanya mahojiano ya mwandishi wa habari mzawa.

Mimi binafsi kuna mazuri ambayo alifanya na mojawapo ni kujenga mifumo ya kiserikali,hii TRA tunayoiona leo,kisomo kwa watoto waliokosa nafasi (MEMKWA) na alimudu kudhibiti inflation kwa miaka yote kumi.

Pia aliweza kutoa pesa kwenye mifuko ya watu binafsi na kuirudisha serikalini kimya kimya (Enzi za Mwinyi pesa ilikuwa mifukoni mwa watu tena wengeine kwa ujanja ujanza).Ukiondoa ujeuri wa Kimakua naona alijitahidi sana kulijenga Taifa.Mengineyo alishatubu kwenye kitabu chake.
 
Rais Mkapa hawakupika hasa baada ya ile hoja kwamba Jenerali si Raia wa Tanzania.
Mkapa alijua ni Raia, kwa bahati mbaya 'intelligence ' walimshauri afanye fyongo na akakubali fyongo.

Kwa upande mwingine, Jenerali anajaribu kubadili mitazamo ya watu kuhusu marehemu.
Tumezoea kuwasifu marehemu hata watu kama akina Nkurunziza wenye '' mapipa ya damu' mikononi

Kwasasa tubadilike, watu waelezwe wasifu wao kama walivyotenda wakiwa hai. Jenerali anamuongelea Mkapa kama alivyomfahamu, hizi habari za sugarcoat si zama zake. Tumechoka kusifu hata wasiostahili kisa wametangulia.

Kwangu mimi bado narudia, kiongozi wa kitaifa ni Nyerere. Huyu alisimama kama baba wa Taifa hata baada ya kustaafu. Hawa waliofuata baada ya kuondoka Ikulu wamebaki kuwa makada wakereketwa bila faida kwa Taifa

Eti Rais Mwinyi anataka katiba ibadilishwe kisa mtoto wake ashinde Urais Zanzibar, halafu ipo siku kizazi kitatakiwa kiongelea mema yake na kufumbia macho uozo kama huo.!!! Hapana tutasema tu wakati ukifika

JK hasemi kwasababu kuna watu wana masilahi na chama. Ipo siku tutazungumzia ukimya wake

Kwa ufupi, mtu aelezwe kama alivyofanya wakati akiwa hai! halafu matendo na kauli zake zitapimwa na busara za wanaosoma au kusikiliza habari zake. Big up Jenerali
Uko sahihi kabisaaaaah
 
Jenerali inaonekana bado ana hasira za kunyang'anywa uraia na kunyimwa uwaziri wa habari na utangazaji!

Hakuna binadamu asie na kasoro .. mtu akifa tunatoa sifa njema, tunaondoa vinyongo banaa
Huo ndio unafiki!!! Yaani mtu unitese, upelekee niisha maisha ya mateso, kisa wewe una madaraka kesho ufariki eti kwakuwa umekufa niondoe kinyongo?!!! Huu ndio unafiki wa mtu mweusi!!!
 
Alikiri makosa na kuomba msamaha.

Hata Magufuli ipo siku ataomba msamaha kwa kazi zake za chini chini.
Msamaha atawaomba huko ahera wahusika wenyewe nna imani atakutana nao. Then atajua km kasamehewa au laaah
 
Jenerali kaonyesha immaturity kubwa kwenye hii Interview.

Mkapa kipindi cha utawala wake Alidhibiti mfumuko wa bei, hata nauli ya daladala ilibaki shilingi 150 kwa muda mrefu sana kwenye utawala wake

Alipandisha kipato cha mtanzania kutoka dola 170 kwa mtu hadi 500 kwa mtu kwa mwaka.

Alijenga Taasisi imara, TCU, NHIF, NSSF, TANROADS, LOANSBOARD.

Alikuwa na Programmes za maendeleo kama vile MKUKUTA, Mkakati wa kuondoa umasikini Tanzania, MMEM Mpango wa Elimu ya Msingi, MEMKWA, MKURABITA

Ni Mkapa ndiye aliyewaita wenye magazeti ya Mwananchi na The Citizens waje wawekeze Tanzania

Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha TV ya Taifa (TBC1)

Ni Mkapa ndiye aliyetujengea uwanja bora kabisa na wa kisasa wa mpira hapa Dar

Pia alikuwa Jasiri kukiri makosa na kurekebisha, Serikali yake ilipounda Bodi ya Parole na kuweka wakiristo watupu, alikuwa wa kwanza kuona tatizo na immediately kuamua kuivunja na kuiunda upya.

Mitihani ya kidato cha nne ilipovuja kama njugu mwaka 1998, Aliifuta mitihani na kuleta mingine.

Waislamu walipolalamika kuwa hawajanufaika ipasavyo na matunda ya uhuru katika elimu, aliwapa majengo ya Tanesco wajenge chuo chao lakini wakati huohuo pia akabalance kwa kuwarudishia makanisa baadhi ya shule zao zilizochukuliwa na Nyerere

Sasa Jenerali Ulimwengu asilete chuki zake binafsi kwenye msiba wa mzee wetu.

Na kabla ya kuwa rais, Benjamin Mkapa alifanya kazi nzuri sana kama waziri wa. mambo ya nje kipindi cha Vita vya Kagera na pia alifanya kazi nzuri sana kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika

Mzee Mkapa katutoa mbali, Jenerali akae na chuki zake lakini tunayo rekodi nzuri ya kutukuka ya mzee wetu
Mbona mapungufu yake hujsyaonyesha mkuu?!! Kiongozi wa siasa tena za kiafrika awe na mazuri tu?!! Never!!!! Kuna mambo ambayo mkapa aliyafanya hata baba wa taifa hakuyapenda, mfano kwenye ubinafushishaji wa mashirika ya umma!!! Mfano bank ya nbc, unajua kilichotokea?!! Kwenye migodi,
 
Duh!

Naona Jenerali Ulimwengu na marehemu Rais Mkapa walikuwa hawapikiki chungu kimoja!

Huyu ni mnafiki tu kwanza alikuwa ni ragfiki yake kwani alikuwa ndio campaign manager wake wakati ule marehemu akiwa kateuliwa kuwa mgombea uraisi ,kwa sababu anazozijua yeye akaondolewa ndio ikawa mwisho wa uraisi,hata magazeti yake na yeye wakaanza bifu ya kumsakama marehemu ndipo akageuziwa kibao cha uraia na ndio ukawa mwanzo wa magazeti yake kuanza kutetereka. Ulimwengu nae ana matatizo kuna wakati aligoma kuachia ukatibu mkuu wa umoja wa vijana wa Afrika kule Algiers ili kumpisha Kabudi ,pia aligombana na Mzee Edo na hata pia alianza kumwandama aliyekuwa waziri wa ujenzi na mawasiliano kwa kuandika habari mbaya kwa sababu anazozijua mwenyewe,alilitumia vibaya gazeti lake la Rai kama kuwatisha baadhi ya viongozi,Jenerali Ulimwengu si msafi hata kidogo,ni mjivuni na kiburi,alipopewa ukuu wa wilaya hakufurahishwa na huo uteuzi tatizo alijifanya nae kama mtu wa karibu wa baba wa Taifa. Wenzake wengi ambao walikuwa viongozi wenzake walianza kumkimbia au kumuacha mmoja baada ya mmoja.
 
Nimesikiliza mpaka mwisho wa mahojiano na Jenerali amejibu kile alichoulizwa hasa kuhusu maoni yake.Hayo ni maoni yake na nakumbuka kuwa kwa kipindi chote cha utawala wake hakuwahi kufanya mahojiano ya mwandishi wa habari mzawa.

Mimi binafsi kuna mazuri ambayo alifanya na mojawapo ni kujenga mifumo ya kiserikali,hii TRA tunayoiona leo,kisomo kwa watoto waliokosa nafasi (MEMKWA) na alimudu kudhibiti inflation kwa miaka yote kumi.

Pia aliweza kutoa pesa kwenye mifuko ya watu binafsi na kuirudisha serikalini kimya kimya (Enzi za Mwinyi pesa ilikuwa mifukoni mwa watu tena wengeine kwa ujanja ujanza).Ukiondoa ujeuri wa Kimakua naona alijitahidi sana kulijenga Taifa.Mengineyo alishatubu kwenye kitabu chake.
TRA gani!? Hiyo ni kazi ya Mwinyi
 
Kusema kweli kifo cha Mkapa hakijaniuma hata kidogo. Nakumbuka tu ushenzi aliofanya Mwembechai kwa watu wasio na hatia. So far Kiongozi pekee kama ikitokea akatangulia itaniuma kiasi fulani ni Kikwete peke yake! Nasema Kikwete peke yake! Labda aje atokee mwingine!
Mkapa alifanyaje hapo Mwembeyanga
 
Asante kwa kukumbusha ,Net group solutions sijui waliishia wapi. Nakumbuka mkapa Alienda Buzwagi akapewa bonge dhahabu na kwenye tv tukaona. Mambo ya kampuni za kuchimba dhahabu ndo kipindi cha Mkapa. Resolute wametuachia mashimo tu pale Nzega.

Nyumba za serikali ndo usiseme. Sasa wanahangaika kujenga nyumba mpya wakati pale Dodoma Uzunguni waliuziana. Nilishangaa juzi Magufuli anasema atoe pesa za kujenga nyumba za wafanyakazi. Wamesahau kabisa waliuziana nyumba za umma nchi nzima.
Nyumba masaki waliuziana kwa 33m enzi hizo,nw wao wameuza kwa mabillioni ya pesa...hizi awamu tatu za mwisho ni hovyohovyo tu
 
Jenerali ulimwengu nimesahau jina halisi ila punguzu chuki.
 
Back
Top Bottom