Jedwali la RA: Nani hayumo?

awe kundi gani yeye au tuongeze jedwali la "wafadhiliwa"?


Kabisa nafikiri mkjj liongezewe la wafadhiliwa. Hivi mkjj kuna kipindi RA alikuwa anataka kutoa nafikiri hotuba kama sijakosea ama ripoti bungeni ikazuiliwa hivi ilikuwa na uzushi gani mpk ikazuiliwa au ndio zilikuwa sanaa? Hii bado imenikaa sana kichwani na sipati majibu maana niliona kama maspika wote walitoa sana macho ndio maana wakaipangua haikuwepo tena
 
nafasi yake ya Ubunge inaweza kuhusishwa kwa namna yoyote na ufadhili wa Rostam?

Habari zisizo rasmi ni kuwa huyu Ngereja kupelekwa kwenye ubunge ilifanywa purposely baada ya kuonyesha ni kijana mzuri kule vodacom. Hiyo ilikuwa stratergy ya kupanga timu ya mashambulizi ambayo imeingia virus kwa sasa labda watafute antivirus mpya kusafisha.
 
Wakuu heshima mbele!

Huyu RA amekuwa akitumiwa na CCM kusimaia shughuli zao za kiharamia kwa muda mrefu kiasi. Na ametumia nafasi hiyo kujinufaisha binafsi kwa ujanjaujanja.

Wale wanokumbuka vizuri, wakati RA anagombea Ubunge Igunga kwa mara ya kwanza mwaka 1994, alikuwa kapuku tu asiye na ushawishi kiasi hicho.

Huyu bwana ameingia kwenye picha kipindi cha kuelekea uchaguzi 1995 kutokana na connection zake na IRAN! na wakati huo kuna wanasiasa maarufu walikuwa wajaribu kupata ufadhili kuwania uongozi wa nchi. Hivyo basi kuna wazee wengine maarufu wa CCM nafikiria waongwezewe kwenye JEDWALI na si ajabu tukajikuta serikali nzima na chama tawala wamewekwa mfukoni.

TAHADHARI: hapa hatufanyi 'operesheni sangara' kwa sababu hata rafiki zetu wa 'chama mbadala' walisikika wakiitetea Dowans 'kwa maslahi ya Taifa!'
 
Mbona naona mnaanza kupoteza muelekeo, MKJJ amekwisha onya kama huna unalolijua kaa kimya, kwa sasa hatua iliyokuwepo ilikuwa ni kutaja tu hayo mengine yafuate baada ya jedwali.mfano
PETER SELUKAMBA (a) Mbunge Kigoma Mjini
SIRAJU KABOYONGA (a) Mbunge Tabora Mjini
 
Last edited by a moderator:
Msisahau dili ya ngeleja kupishwa ubunge kwenye jimbo lake-aliyempisha ubunge naye alielezwa offer akakubali kumpisha na yuko wapi? kapewa alichoahidiwa baada ya kumpisha kijana!
 
Katika jedwali category a msipoteze muda kutaja mtu mmoja mmoja. Chama Cha Mapinduzi kilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ufadhili wa RA.

Kwa wale wasiojua matusi ya RA katika kampeni za chaguzi ndogo waulize. Kule Kiteto RA alikodisha Helkopta kwa ajili ya kuishughulikia CHADEMA. Katika uchaguzi mdogo Tarime a,likodisha helkopta 2 kwa kusudi hilo hilo.

Itakapotakiwa tutaleta jamvini mambo ambayo RA amefadhili kwa ajili ya kuiwezesha CCM kushinda na kudumu madarakani kila mahali tutawashangaza hapa jamvini kwani tuna mengi mno ambayo masikio yakisikia yatawazsha. Inafahamika wazi kuwa amekuwa akifanya hivyo ili kupunguza au kuondoa kabisa uwezekano wa kushambuliwa dhidi ya ufisadi na wizi wake.

Lakini pia tusisahau kuwa huyu RA yeye ndiye anayeonekana mfadhili si kwa mali zake bali kwa mali walizoiba kutoka vyanzo mbalimbali na pia kwenye tender alizopewa kiupendeleo. Hivyo yeye ndiye mastermind ya CCM nzima ofcourse plus wengine kama Nimrod, msururu wa wahindi kibao etc.
 
Wakuu heshima mbele!

..........Huyu bwana ameingia kwenye picha kipindi cha kuelekea uchaguzi 1995 kutokana na connection zake na IRAN!........ '

Inasemekana hata maamuzi mengi kwenye ubalozi wa Iran nchini Tanzania yanafanywa kwa kumconsult RA.
 
Edward Lowassa --Mbunge wa Monduli--[a]

Peter Serukamba---Mbunge wa Kigoma Mjini--[a]

John Mwakipesile--RC Mbeya--[a]

Nchimbi --Naibu waziri Ulinzi na mbunge Songea [a]

Yusuf Makamba--Mbunge na Katibu Mkuu CCM [a]
 
Last edited:
Hivyo yeye ndiye mastermind ya CCM nzima ofcourse plus wengine kama Nimrod, msururu wa wahindi kibao etc.

NDIO MAANA WALIWAHI KUMPA UHAZINI WA CHAMA TAWALA KWA KIPINDI KILE!kuna transaction za msingi KWA CHAMA ambazo zilikuwa zinaendelea,zilihitaji uwepo wake.
 
I like this approach .Inavyoelekea watu wengi hawajui uhusiano na RA na uongozi wa Nchi na uhusiano kati ya umaskini wetu , uongozi wetu, na RA . Bila shaka tukichora hilo jedwali wengi watatambua zaidi.

Tunahitaji kupata data za jinsi RA amekuwa akifadhili CCM kwa miaka mitano iliyopita ili kuhakikisha viongozi anaowataka wanaingia madarakani. Tukiangalia hicho kiasi, pamoja na matokeo ya jedwali tunapata picha iliyo kamili.
 
Watanzania tusiwe wajinga kiasi hicho kufikiri matatizo ya Tanzania ni ya mtu mmoja badala ya system nzima ambayo ni mbovu na imeshindwa kutimiza majukumu yao. Hii ni tabia ya watu ambao wanashindwa kukubali part yao katika failures hizi mbalimbali na badala yake wanakimbilia kutafuta scapegoat.

Hata leo akifa RA ufisadi hautaisha Tanzania. Ni siasa za mufilisi kuamini kwamba nchi inayumba shauri ya mtu mmoja. Huyo RA hajaenda kuiba bank kwa mtutu au hajawafunga kamba viongozi wetu, amefanya anayofanya kwa kutumia watu ambao sisi wenyewe wengi wetu tukiwepo hapa JF tumewaweka serikalini pamoja na makosa yao mengi ya huko nyuma.

Miaka 20 iliyopita hakukuwa na ufisadi na bado nchi ilikuwa maskini pamoja na jitihada kubwa za watu kama Nyerere. Sasa badala ya kuelemisha jamii juu ya tufanye nini ili kuwasaidia wananchi wengi hasa wa vijijini ambao wanaishi kwa dhiki kubwa, kushuka kwa elimu, huduma mbovu za afya, mifuko iliyotoboka, sisi tunatumia zaidi ya 90% ya muda wetu kumjadili mtu mmoja tena with zero result.

Watu hao hao ambao kwa wakati mbalimbali walikuwa wakishirikiana na RA huku wakijua madudu yake, leo wanajifanya ni vinara wa kutuambia matatizo ya TZ ni RA.

Ili Tanzanzania iende mbele ni muhimu sisi sote nikiwemo mimi mtanzania, tujiangalie tena kwa kioo na kuona vipi tunaweza kubadilika na kutenda haki kwa watu wetu, kabla ya kummulika mtu mwingine kwa kioo hicho, tujimulike sisi kwanza. Tuna uwezo wa kubadili matendo yetu kabla ya kubadili matendo ya mtu mwingine.

Ni sawa ni vizuri kuweka pressure kupambana na madhambi mbalimbali katika jamii lakini sio kwa kiwango cha sasa cha upotoshaji kuonyesha kwamba kama sio RA nchi ingekuwa na mabomba yanayotoa maziwa. Nenda kwenye kampuni zozote za Tanzania au institutions za serikali au hata kwenye majumba ya wasomi, utagundua madudu lundo tu kwa muda mfupi. Je na huko nako RA ndiye anatutuma?

RA tumemtengeneza wenyewe shauri ya tamaa zetu za haraka haraka na kufikiri maisha bora yanakuja kwa ujambazi. Kuamua kusaliti mamilioni ya wananchi waliotupa nafasi ili tujilundikie mapema na kuishi kama tuko ahera. Leo sisi Watanzania wote tukiamua kutimiza wajibu wetu, hao akina RA hawatakuwepo.

Ni nani mbunge wa CCM ambaye anaweza kuapa kwa mungu kwamba hakufaidika na mapesa yaliyooza ya Rostam na genge lake? Mtu akisema hivyo atakuwa anadanganya tu kama wanavyodanganya kwenye mambo mengi.

Ndio maana watu wengine tumepunguza kuchangia JF kwasababu mwelekeo sasa umeanza kuwa mtu badala ya system au fikra. Tumeanza kugeuza fikra zetu na kuanza kuwa mimi na yule au sisi na wale. Tunajaribu kwa nguvu zote bila mafanikio kuingiza pumba kwenye vichwa vya Watanzania ili waweze kuamini kwamba tatizo letu ni mtu mmoja.

Binafsi naamini mawazo kama haya hayamsaidii mtu yeyote na badala yake yanazidi tu kuligawa taifa. Lazima tutengeneze principles ambazo tuko tayari kuzisimamia na kuzilinda bila kujali aliyekiukwa na RA au Mengi. Vinginevyo na sisi wengine tunageuka kuwa vikaragosi vya hawa wababe ambao wameitumia system kufika pale walipofika na sasa wameamua kugeukana.
 
naona bado uko kwenye vitendawili na hadithi

na narudia mwacheni Mwamvita Makamba peke yake kama alivyo

Duh mbona wewe unapinga tu lakini utoi alternative? Huyo Mwamvita nani wako? Watu wanadiscus ili kupata trend ya kuendelea na mada wewe unasema umwacheni who are you?
 
Edward Lowassa --Mbunge wa Monduli--[a]

Peter Serukamba---Mbunge wa Kigoma Mjini--[a]

John Mwakipesile--RC Mbeya--[a]

Nchimbi --Naibu waziri Ulinzi na mbunge Songea [a]

Yusuf Makamba--Mbunge na Katibu Mkuu CCM [a]

Mtandao mzima upo ndani kwani unashirikiana RA ndiye kiongozi.
 
Mbona tunajibu swali kinyumenyume!!!! Mwnkjj ameuliza nani hayumo, sie tunajikita kuwataja waliomo... ndio tutapata jibu sahihi kwa sababu baada ya kuwafahamu waliomo, hatimaye tutawajua wale ambao hawamo. lakini nadhani tutajizungusha sana kwa njia hii (ingawa ina faida kubwa). Mimi naomba nijibu swali moja kwa moja, kwa kumtaja mmoja tu ambaye nafahamu kuwa hayumo-Dr Ali Mohammed Shein
 
Mbona tunajibu swali kinyumenyume!!!! Mwnkjj ameuliza nani hayumo, sie tunajikita kuwataja waliomo... ndio tutapata jibu sahihi kwa sababu baada ya kuwafahamu waliomo, hatimaye tutawajua wale ambao hawamo. lakini nadhani tutajizungusha sana kwa njia hii (ingawa ina faida kubwa). Mimi naomba nijibu swali moja kwa moja, kwa kumtaja mmoja tu ambaye nafahamu kuwa hayumo-Dr Ali Mohammed Shein

Hayumo CCM au Serikalini!
 
Back
Top Bottom