Jedwali la RA: Nani hayumo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jedwali la RA: Nani hayumo?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 28, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna wimbo mmoja uliimbwa na kwaya ya Bulyankulu Barabara ya 13 uitwao "Samson". Sehemu ya wimbo huo nikikumbuka inasema:

  "Tafadhali niambie asili ya nguvu zako, tafadhali niambie waweza kufungwa na nini?" alilalamika mwanamke wa Kifilistina. Sasa, simlinganishi RA na Samson Mnadhiri wa Mungu ila kwenye hili suala la nguvu ambazo inaonekana hazidhibitiki!

  Nikiwa nafikiria hilo nikakumbuka mambo ya kuchora majedwali ambamo unaweka makundi ya vitu mbalimbali na ndipo wazo limenijia. Yawezekana ili kuweza kuelewa nguvu za RA ni lazima tuchore jedwali moja hivi na kujaribu kuweka ndani yake watu ambao wanahusiana au wamehusiana moja kwa moja na RA na sasa watu hao wako madarakani au kwenye nafasi fulani za maamuzi.

  a. Wale aliowafadhili na kuwasaidia kushika au kudumisha nafasi za kisiasa.

  Kundi hili litakuwa na wale wote ambao aliwasaidia wakati wa kampeni au kuwafadhili na kuwasaidia kushika nafasi za kisiasa. Wabunge, Wagombea wa Urais n.k Yaani hapa ni jumla ya wanasiasa ambao wamepata ufadhili kwa RA.

  MATOKEO:
  1. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2.Benno Malisa - (a) - Makamu Mwenyekiti- TAIFA, UVCCM
  3.Sofia Simba - (a) - Mwenyekiti Taifa- UWT(CCM)
  4. Prof. Juma Kapuya - Waziri wa Kazi & Maendeleo ya Vijana (Mbunge Urambo Magharibi)
  5. Adam Malima - (a) - Naibu Waziri, NISHATI NA MADINI (Mbunge, Mkuranga)
  6. Emmanuel Nchimbi, alikuwa Mwenyekiti wa Vijana, sasa Naibu Waziri Ulinzi
  7. Dr. Peter Kafumu, aliacha kugombea Ubunge Igunga kumpisha Rostam, sasa Kamishna wa Madini
  8.
  9. Abdulaziz - RC.
  10. Lukuvi - RC.
  11.J Mongella - DC.
  12. Membe - Ubunge, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
  13.Mzindakaya - Ubunge.
  14.Nyami - Ubunge.
  15.Sita - Ubunge & U-spika.
  16.Mahanga - Ubunge.
  17. Guninita - CCM Mkoa.
  14. Kamala - Ubunge.
  15. Marmo - Ubunge.

  16. PETER SELUKAMBA (a) Mbunge Kigoma Mjini
  17. SIRAJU KABOYONGA (a) Mbunge Tabora Mjini
  18. John Mwakipesile--RC Mbeya--[a]
  19. Yusuf Makamba--Mbunge na Katibu Mkuu CCM [a]

  b. Wale ambao wamewahi kuwa watumishi wake kwenye Vodacom.
  Akiwa ni mmoja wa wenye hisa kubwa pale Vodacom (ingawa nasikia alikuwa na mpango wa kuuza hisa hizo) kuna watu ambao wamewahi kufanya kazi Vodacom au kupewa mkataba wa kazi Vodacom. Watu hao wengine wameenda na kuwa na nafasi za kisiasa (yawezewa kuwa kwenye "a" hapo juu). Kama mtu anatokea kwenye "a" na anatokea kwenye "b" basi wawekwe vile vile.

  MATOKEO:
  1.Pius Msekwa - Vodacom B. - Makamu wa Mwenyekiti CCM (Bara)
  2. William Ngeleja - Vodacom - Waziri wa Nishati na Madini
  3. Dr. Idris Rashid (Vodacom) - Mkurugenzi Mtendaji Tanesco

  c. Wale ambao wametumika kwenye vyombo vyake vya habari
  Hawa ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wamewahi kuwa na ubia pamoja au utumishi wa vyombo hivyo vya habari na sasa hivi wako kwenye nafasi fulani fulani za kisiasa au za kiserikali. Hapa ninawaondoa watumishi ambao wanafanya kazi tu kwenye vyombo vyake vya habari. Msisitizo ni wale waliovuka toka kwenye vyombo vya habari kwenda kwenye serikali au siasa.

  MATOKEO

  - Badra Masoud, Afisa Mawasiliano Tanesco, alikuwa Mhariri HCL
  - Salva Rweyemamu, Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu, alikuwa Mhariri HCL
  -

  d. Wale wenye ushirikiano wa kibiashara.
  Kundi jingine ni la wale ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mahusiano ya kibiashara na RA au makampuni yake mengine na hawa nao wametoka huko na sasa wana nafasi serikalini (idara, wizara au wakala mbalimbali). Na nafasi zao kwenye idara hizo.


  Jinsi ya kufanya:
  Bila kuweka maelezo mengi, linatajwa
  Jina (Salva Rweyemamu);
  kundi lake (c)
  na nafasi yake ya sasa (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais).

  Nitaendelea kuupdate tunayoyapata labda tunaweza kuona pattern ya aina fulani hivi ikijitokeza. Ukiweza kuweka na some kind of the story behind ya chaguo lako that will help too to make sense.

  Baada ya hapo tutachora majedwali ya watu wengine wawili halafu tutaona hiyo picha inayotokea inatuonesha nini. Yawezekana kuna kitu ambacho tumekimiss kwa muda mrefu juu ya RA na nadharia niliyonayo yaweza kuthibitika kisayansi juu ya "asili ya nguvu yake".

  Kama huna lolote unalojua; sit down and enjoy!
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  1. Msekwa - Vodacom B.

  FMES!
   
 3. B

  Bi Tarabushi Member

  #3
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngeleja- Vodacom b
   
 4. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ngeleja - (b) - Waziri, NISHATI NA MADINI

  SALVA Rweyemamu - (c) - Mkurugenzi wa Habari, IKULU
   
 5. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Benno Malisa - (a) - Makamu Mwenyekiti- TAIFA, UVCCM

  Sofia Simba - (a) - Mwenyekiti Taifa- UWT(CCM)
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  2. Kapuya - A. (alisaidia kumfunga Rage, asigombee ubunge jimbo la jirani yake Kapuya & Patners kwenye migodi).

  FMES!
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hon. H.E Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (a) - President of URT and Chief of the Army.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nafasi yake ya Ubunge inaweza kuhusishwa kwa namna yoyote na ufadhili wa Rostam?
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Jakaya M Kikwete :-A rahisi wa wadanganyika
   
 10. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Adam Malima - (a) - Naibu Waziri, NISHATI NA MADINI
   
 11. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Katika jedwali category a msipoteze muda kutaja mtu mmoja mmoja. Chama Cha Mapinduzi kilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ufadhili wa RA.

  Kwa wale wasiojua matusi ya RA katika kampeni za chaguzi ndogo waulize. Kule Kiteto RA alikodisha Helkopta kwa ajili ya kuishughulikia CHADEMA. Katika uchaguzi mdogo Tarime a,likodisha helkopta 2 kwa kusudi hilo hilo.

  Itakapotakiwa tutaleta jamvini mambo ambayo RA amefadhili kwa ajili ya kuiwezesha CCM kushinda na kudumu madarakani kila mahali tutawashangaza hapa jamvini kwani tuna mengi mno ambayo masikio yakisikia yatawazsha. Inafahamika wazi kuwa amekuwa akifanya hivyo ili kupunguza au kuondoa kabisa uwezekano wa kushambuliwa dhidi ya ufisadi na wizi wake.
   
 12. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2009
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Lowassa anafit vipi kwenye hili jedwali?
  au atakuwa na lake ?
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  hhaahaha.. usiwe na wasiwasi.. kuna wengine tutachora kuweza kuona strategic alliances..
   
 14. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kabisa, maana alikuwa mwanasheria wa Vodacom wakati Rostam akiwa shareholder na alipopata tu ubunge akapendekezwa kwa mkulu kuwa naibu waziri kabla hajawa waziri kamili.
   
 15. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  mimi nadhani siyo Fedha zake za mfukoni ni za Kagoda ambazo tunajua zimetokea wapi.
   
 16. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  b. Wale ambao wamewahi kuwa watumishi wake kwenye Vodacom.  Umemsahau Idrisa Rashid - sasa MD wa Tanesco
   
 17. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa ndo utajua kwanini rashid alitetea dowans!
   
 18. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Sijui na hii nayo itapata nafasi gani katika Jedwali hilo,Nawafahamu baadhi ya Mabinti ,ambao wamepata nafasi mbalimbali huko Vodacom kwa sababu ya nafasi za Wazazi wao serikalini..wengi wameingia hapo si kwa Elimu/Uwezo wao..bali wamekwenda na Memos kutoka kwa Wakuu...Mabinti hao ni watoto wa:

  1: Makamba (Katibu Mkuu wa CCM)
  2:Mwapachu.(Mbunge Tanga Mjini/Waziri wa zamani mambo ya katiba)
  3:Maj.Gen Kombe (RIP) - (Aliwahi kuwa Boss kwenye TISS)
   
 19. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nadhani kwa sasa ni haki ya rostam kutamba kuwa nchi yake!! si tumempa wenyewe.
   
 20. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Makamba inajulikana kuwa yeye ndio mbeba maboksi ya pesa kutoka kwa RA na kwenda kwa wakulu, anakata panga njiani

  Meghji aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa kagoda pamoja na kuwa kagoda iliuzwa kwa manji baadae.

  Its seems huyu jamaa ni kichwa cha waarabu na wahindi wa Tanzania mpaka wanakubali kumbebebea mzingo wa lawama ili yeye hawe huru.

  Manji aliyesaidiwa kupata pesa za import support kutoka BOT
   
Loading...