Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,186
- 56
Kuna documentari moja inatayarishwa na waandishi wa habari wa kiafrika wanaofanya kazi kwenye mashirika makubwa ya habari ya uropa na amerika. Documentari hii ilisimama kwa muda baada ya mmoja wa wataarifu habari (reporter) maarufu kutoka nchi moja ya afrika mashariki kuacha/chishwa kazi katika mazingira yasiyo na kueleweka kabisa.
Katika documentary hii, kumeonyeshwa maisha ya wananchi wa nchi zilizoamua kuwa za kibepari afrika baada ya uhuru ikilinganishwa na zile zilizoamua kuwa za kijamaa (au kutofungamana na upande wowote). Niliguswa sana na clips toka kwa majirani zetu wa Kenya, Uganda, na Congo.
Ilionyeshwa kuwa, Kenya kulikuwa na watoto ombaomba (chokoraa) karibu milioni moja wanaoishi maisha ya kubahatisha. Ilionyeshwa pia kuwa Kuna watu zaidi ya milioni nne wanaoishi katika slums na hali mbaya ya kiafya na kimazingira. Uganda kulionyeshwa maelfu ya watoto wanaotembea kilomita nyingi kila siku kwenda kulala kwenye miji mikubwa kwa sababu hawana pa kulala. Kuna watoto zaidi ya milioni moja Congo wasiokuwa na hakika ya kula mlo mmoja wa siku. Habari imekuwa mbaya kwa Malawi ambayo baa la njaa la miaka michache iliyopita limeacha watu wengi taabuni.
Nchi za kijamaa nazo wameonyesha Ghana, Tanzania, Zambia (sijui ni vigezo gani wametumia) zimepitia matatizo haya haya na hakuna mwenye nafuu kidogo ingawa waandishi hawa wote wanakiri kuwa Slums za Kibera nk za kenya ndizo kubwa kabisa katika nchi yoyote Afrika (sijui bado vigezo). Hii documentary imeonyeshwa kwa wanachama wa chama cha waafrika hapa chuoni kwangu ili kupata mawazo yao kabla haijaanza kusambazwa.
Kilichonishangaza ni kuwa, wengi walioiona hawakupinga kuwa iko biased ila walianza kulaumu ubepari na ujamaa. Wote tunajua kuwa ujamaa wa russia uliporomoka na kushindwa wakati wanaojiita mabepari - marekani wakionekana kufanikiwa. Swali ni je, hali mbaya ya wananchi wa nchi za "kibepari" afrika ni dalili ya kushindwa kwa ubepari Afrika?