Inawezekana ubepari uliopitiliza ulimgharimu sana Lowassa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,264
Edward Lowassa limekuwa jina kubwa sana katika siasa za nchi hii kwa muda akihusishwa na kutafuta kuikalia ofisi namba bila mafanikio mpaka anaondoka duniani.

Lowassa amekuwa mjadala mkubwa kuanzia kwa Nyerere mpaka leo hii ambapo hayupo duniani. Haijawahi kuwekwa wazi hasa na yeyote wa chama chake kwa nini siku zote alionekana na vigogo wa chama chake kutofaa kwa nafasi hiyo ili hali akiwa na ushawashi mkubwa mno kwa wanachama wengine wa chama chake.

Jambo kubwa ambalo limekuwa likizungumzwa sana na watu wasio vigogo wa chama chake ni ufisadi, kukosa uadilifu au kujilimbikiza mali lakini huu nao bado ni mjadala wenye kuacha maswali mengi kuliko majibu ya kueleweka.

Sijui uadilifu wa Lowassa au kama kweli alikuwa fisadi na kwa kiwango gani cha kutisha kuliko mafisadi wengine ila naamini huenda jambo lingine kubwa kumuhusu ni kwamba labda alikuwa na mawazo ya ubepari uliopitiliza.

Nchi yetu kwa muda mrefu ilikuwa ya kijamaa na hata baada ya kufunguliwa kwa uchumi wa soko huria siasa zetu hasa za kiuchumi zimeendelea kujikita katika aina fulani ya ujamaa uchwara na mabepari sio watu waliotazamwa kwa jicho zuri sana.

Sasa Lowassa inaonekana hakuwa na muegemeo wa ujamaa kabisa. Tofauti na viongozi kama Mwinyi au Mkapa ambao ubepari wao unaonekana kusukumwa zaidi na taasisi za kimataifa na hali ya halisi za nyakati Lowassa ubepari wake unaonekana ni wa kutoka moyoni kabisa au wa imani. Huenda jambo hilo ni mojawapo ya mambo ambayo yalimletea mgogano mkubwa na wafahidhina ambao ni gate keepers wa mfumo wakihofu mabadiliko makubwa ya kimfumo endapo angekamata madaraka makubwa zaidi ya nchi.
 
Kiukweli mkuu, nchi hii ukiwa bepari unaonekana mdhambi wakati ndio kitu sahihi
Fikiria inasemekana Lowassa alianza kujilimbikizia mali au kuwa bepari enzi Nyerere akiwa bado ana "call the shots" kwenye chama, hapo si kama kitimoto kukatiza karibu na msikiti.
 
Soma hiyoo!!
20240213_180134.jpg
 
Hizo pesa alizovuna ziko wapi? Yaani viongozi wa Tanzania ni watu wa kipekee kwelikweli yaani biashara zao ni kiza tu, hazionekani katika macho ya kawaida...uwekezaji wao ni wa mashaka sana, wamekaa ki ujanja ujanja sana.

Leo hii ukiingia goodge na kuandika Jina la Majaliwa Majaliwa Kasimu...utapata tu kuwa ni waziri mkuu wa Tanzania wala hakuna biashara ata moja anayofanya.
Swali ni je afanyi biashara? Na kama anafanya mbona hazifamiki au hataki tuwachukue kama roll modal msemo wa waswahili.
 
Edward Lowassa limekuwa jina kubwa sana katika siasa za nchi hii kwa muda akihusishwa na kutafuta kuikalia ofisi namba bila mafanikio mpaka anaondoka duniani.

Lowassa amekuwa mjadala mkubwa kuanzia kwa Nyerere mpaka leo hii ambapo hayupo duniani. Haijawahi kuwekwa wazi hasa na yeyote wa chama chake kwa nini siku zote alionekana na vigogo wa chama chake kutofaa kwa nafasi hiyo ili hali akiwa na ushawashi mkubwa mno kwa wanachama wengine wa chama chake.

Jambo kubwa ambalo limekuwa likizungumzwa sana na watu wasio vigogo wa chama chake ni ufisadi, kukosa uadilifu au kujilimbikiza mali lakini huu nao bado ni mjadala wenye kuacha maswali mengi kuliko majibu ya kueleweka.

Sijui uadilifu wa Lowassa au kama kweli alikuwa fisadi na kwa kiwango gani cha kutisha kuliko mafisadi wengine ila naamini huenda jambo lingine kubwa kumuhusu ni kwamba labda alikuwa na mawazo ya ubepari uliopitiliza.

Nchi yetu kwa muda mrefu ilikuwa ya kijamaa na hata baada ya kufunguliwa kwa uchumi wa soko huria siasa zetu hasa za kiuchumi zimeendelea kujikita katika aina fulani ya ujamaa uchwara na mabepari sio watu waliotazamwa kwa jicho zuri sana.

Sasa Lowassa inaonekana hakuwa na muegemeo wa ujamaa kabisa. Tofauti na viongozi kama Mwinyi au Mkapa ambao ubepari wao unaonekana kusukumwa zaidi na taasisi za kimataifa na hali ya halisi za nyakati Lowassa ubepari wake unaonekana ni wa kutoka moyoni kabisa au wa imani. Huenda jambo hilo ni mojawapo ya mambo ambayo yalimletea mgogano mkubwa na wafahidhina ambao ni gate keepers wa mfumo wakihofu mabadiliko makubwa ya kimfumo endapo angekamata madaraka makubwa zaidi ya nchi.
Tuna changamoto ya siasa za hadithi za kufikirika zisizo na facts hata kidogo.
Huu waweza kuwa uthibitisho wa umasikini wa fikra (siyo kwako, bali kitaifa) unaokuwa msingi wa ule wa mali/uchumi.
Ufisadi huthibitishwa kwa kuonesha mali ambazo zimepatikana wakati akiwa mtumishi wa Uma na kipato kikijulikana (rekodi za tume ya maadili ya viongozi wa Uma), au zile ambazo hazijarekodiwa lakini kuna uthibitisho ni za mtuhumiwa (lazima zitajwe).
Sasa kama wote huimba kama kasuku tu (ufisadi, ufisadi.... ) ni unafiki na upumbavu.
Ushuhuda wa upumbavu na unafiki unaonekana kwenye msiba wa Edward Lowasa.
Apumzike kwa Amani.
 
Lowassa alichukia umasikini waziwazi, kuna wanasiasa wanachukia umasikini kwa kificho ingawa wameingia kwenye siasa ili kuchuma mali.
Kwa vyovyote vile Umasikini siyo kitu cha kujivunia.
Kwamba Lowassa alichuma mali zake kwa njia gani hilo ni lake yeye mwenyewe.
 
Kiukweli mkuu, nchi hii ukiwa bepari unaonekana mdhambi 😂😂😂 wakati ndio kitu sahihi
Ukweli ni kwamba lowasa hakuwa bepari yeye alikuwa Mwizi wa Mali za Umma Na pia mla. rushwa mkubwa.
Hakuna bepari muajiriwa
 
Lowassa alichukia umasikini waziwazi, kuna wanasiasa wanachukia umasikini kwa kificho ingawa wameingia kwenye siasa ili kuchuma mali.
Kwa vyovyote vile Umasikini siyo kitu cha kujivunia.
Kwamba Lowassa alichuma mali zake kwa njia gani hilo ni lake yeye mwenyewe.
Alichuma Mali zake Kwa :-
1. kuiba Mali za umma Na kuzifanya zake,
2.kuomba Na kupokea rushwa
 
Kwa nini waliendelea kumteua kuwa waziri hadi waziri mkuu?

Mali gani za umma alizoiba na kuzifanya zake?
Kuna skendo aliiba wapi na shillingi ngapi?
Mfano visa vya rushwa alivyohusika au kuhusishwa navyo ni vipi?
 
Ukweli ni kwamba lowasa hakuwa bepari yeye alikuwa Mwizi wa Mali za Umma Na pia mla. rushwa mkubwa.
Hakuna bepari muajiriwa
Kiasi gani cha mali za umma anatuhumiwa kuiba na mali zipi? Rushwa alizokula ni zipi na kwa nini aliendelea kushika madaraka makubwa ya nchi wakijua ni mla rushwa?
Nimezungumiza ubepari kwa maana ya philosophia yake ya maisha aliyokuwa anaikubali na kuihusudu, pia kama unafikiria mabepari ni matajiri wakubwa tu basi Shabiby, Mo na Rostam wote wamekuwa waajiriwa bungeni na kwenye chama.
 
Ukitaja tu neno FISADI, jina la Lowassa linakuja kwenye maelezo.
Kumuita Lowassa fisadi zilikuwa ni kampeni na majungu ya CCM tuu, hakukuwahi Kuwa na ushahidi wowote wa hizo tuhuma, zaidi ya tuhuma za bunge zilizomuondoa nafasi ya PM hakuwahi kuchunguzwa, kushitakiwa au kufikishwa mahakamani, alijitahidi kuanzisha shule za kata nchi nzima ingawaje hazikuwa nzuri lakini sasa wananchi Wana nafasi ya kuziendeleza na kupelekea nchi nzima Kuwa na shule za sekondari mpaka vijijini, pia alisaidia sana maji ya lake Victoria kusambazwa mikoa ya kati na sasa ni swala ya kuendeleza tuu na mikoa yote ya kati sasa wanaweza Kuwa na maji mpaka ya umwagiliaji, hakuwahi malaika lakini alikuwa na afadhari na mikakati na mchapa kazi kuliko viongozi wengi wa CCM, hakuwahi na roho ya kimaskini
 
Tutabishana huku lakini yeye huko aliko keshatambua kama aliyofanya yalikuwa haki na sahihi au la. Kuna mdau kaandika humu kuwa kwa Mungu hakuna rushwa wala connection.
 
Back
Top Bottom