Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Kumsikiliza mtoto kunaaminika kuwa ndio ngao muhimu zaidi ya kumlinda mtoto. Wataalamu wa malezi wanatuambia kuwa mtoto anayesikilizwa huwa jasiri na muwazi kwa mzazi au mlezi kwa yote anayoyapitia yawe mema au mabaya kwani wanaamini kuwa watachukua hatua kwa ajili yao.
Mara nyingi mtoto asiyesikilizwa, pindi anapopitia changamoto ya kufanyiwa udhalilishaji au ukatili wa aina yoyote, hukosa mahali pa kueleza ili apatiwe msaada kwani huhisi kutokuaminika kabisa hali inayompa maumivu ya kudumu na kuendelea kuwa mtumwa wa udhalilishaji huo.
Ndugu mzazi/mlezi hakikisha unamsikiliza mwanao kila mara, weka mazingira ya yeye kukuamini na wewe kumuamini ili awe salama wakati wote.
Sema Tanzania