Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
ahaaaaaa, ok! lakini unakubali kuwa mchaga yeyote hafai kugombea urais kwa jinsi walivyoonyesha mbegu ya ukabila ka ilivyoelezwa kwenye thread hii?

Mama,

Mimi nasema wanafaa kwani kuna wachaga ambao wana maadili mema na wanachukia hii dhambi ya ukabila and they dont entertain it ata all.So ukisema hawafai utakua umefanya collective judgement mama
 
Mama,

Mimi nasema wanafaa kwani kuna wachaga ambao wana maadili mema na wanachukia hii dhambi ya ukabila and they dont entertain it ata all.So ukisema hawafai utakua umefanya collective judgement mama

Ben, hebu nipe mfano wa kiongozi wa juu mchaga ambaye ni safi. Maana umekuwa mpole kama mtetezi wa Mbowe maskini.
 
Sowing the seeds of selfdestruction.......

However nadhani makala kama hii ikitoka katika gazeti kama la Nipashe ama Tanzanianjema itasaidia watanzania kuamka......

Ni hatari lakini important strategy kuamsha jamii ya watanzania....

Tanzanianjema
 
Mimi siyo Mchagga lakini Mzazi wangu moja ni Mchagga. Watanzania inabidi tuache mipango ya ukabila na tufikirie zaidi uwezo na elimu ya mtu. Wachaga hawapendelewi bali wanafanya kazi kwa bidii mfano angalia idadi ya Wachaga na Wapare wenye CPA,PHD, LAWYERS kupita huko kila mtu ana nafasi sawa hivyo kama unataka kufanikiwa soma na faulu kama hawa wachaga badala ya kulalamika. Kama mnaomba kazi watu wanne na Wachaga ni watatu kunauwezekano mkubwa wa mchaga kuchukuliwa na si kwa ukabila lakini kwa qualifications. Biashara je inaupendeleo nayo!! tukianza kutoa kazi kikabila ufanisi utapungua.Je tungekuwa na raisi Mchaga tungesema nini?
 
Na wewe nawe....sio subutu bana ni thubutu....we kabila gani wewe?

Mi mchagga...na nimeandika hivyo makusudi kabisa ili kutia 'vionjo' vya kichaga

On a serious note,

Nawaomba mamods hii thread ifunguwe, itupwe kapuni for good. Na Mwanakijiji afungiwe walau kwa wiki moja. Hii party ya huko sijui Columbus naona imembadili 'fikra' zake na sasa hivi amekuja na mawazo ya ukabila...sio watu wot wataweza kuelewa maudhui ya hii thread na kama walivosema wengine , hapa watu watatumia emotions tu

Hapa JF nina hisia kuwa wengi ni wachagga pia ( si ndo 'wamefanikiwa zaidi' so wana access ya komputer etc..) au la wana GF/BF wa kichagga..so kwa kuanzia walioa na unasaba wowote na wachagga wasiingie JF kuanzia kesho.

Mwanakijiji, pamoja na kupendekeza ufungiwe bado hutatakiwa uingie JF manake najua uchagani haoakwepeki.....bisha..!

mamod hilo ndo wazo langu jamani......
 
Mimi siyo Mchagga lakini Mzazi wangu moja ni Mchagga. Watanzania inabidi tuache mipango ya ukabila na tufikirie zaidi uwezo na elimu ya mtu. Wachaga hawapendelewi bali wanafanya kazi kwa bidii mfano angalia idadi ya Wachaga na Wapare wenye CPA,PHD, LAWYERS kupita huko kila mtu ana nafasi sawa hivyo kama unataka kufanikiwa soma na faulu kama hawa wachaga badala ya kulalamika. Kama mnaomba kazi watu wanne na Wachaga ni watatu kunauwezekano mkubwa wa mchaga kuchukuliwa na si kwa ukabila lakini kwa qualifications. Biashara je inaupendeleo nayo!! tukianza kutoa kazi kikabila ufanisi utapungua.Je tungekuwa na raisi Mchaga tungesema nini?

he he heeee, yaani kabila laanza kukanwa hivi hiviiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mimi nasema wanafaa kwani kuna wachaga ambao wana maadili mema na wanachukia hii dhambi ya ukabila and they dont entertain it ata all.So ukisema hawafai utakua umefanya collective judgement mama

Lakini hapa naona 'collective judgment' si inakubalika, kwamba Wahaya mambo fulani, Waha wabishi, Wachaga stingy, Wakyura wakorofi, Wamachinga hawakuchimba, Wanyakyusa wakabila, na Wasukuma wanga...

Ooh, na Wahehe ma-house girl.

Au?
 
Kuhani.. suala la mimi kupinga ukabila halikuanza kwenye mada hii... kwa miaka miwili nimekuwa nikikemea waziwazi hizi sentiments za kuchukia wachagga. Imefika mahali jina la Mchagga likitajwa kwenye nafasi fulani watu vinyweleo vinasisimka! Na yote haya yako based siyo na kitu ambacho kimefanywa na jamii ya Wachagga.. hapana, bali kwa sababu ya idadi yao kwenye nafasi au vyeo fulani.

Ndio maana hili pendekezo ni "modest" lingekuwa kali ningependekeza kitu kingine kabisa. Tunapovumilia ukabila hasa mtu anapotoa kauli za "fulani Mchagga" basi ujue mbegu za chuki ya kikabila zimo.

Kuna watu wana chuki dhidi ya Wachagga kama vile waliopo wenye mawazo ya kujiona bora kwa wahaya au wanyakyusa. Kama hamuamini ninachosema fanyeni jaribio hili halafu mniambie:

a. Zungumza na rafiki zako na zungumzia jinsi ulivyopata shida kupata nafasi ya kazi ya TRA au taasisi fulani na ya kuwa bosi wa pale ni mchagga na hujui ni kwanini hukupewa hiyo nafasi". Utashangaa majibu ya watu.

Lengo langu ni kuwaamsha ndugu zangu kuwa adui ya Watanzania siyo kabila la Wachagga au dini ya mtu fulani. Kama fisadi wa kichagga yupo basi siyo uchagga wake unaomfanya awe fisadi kama vile siyo Usukuma, au Uzaramo wa mtu unaomfanya awe fisadi.
 
Ben, hebu nipe mfano wa kiongozi wa juu mchaga ambaye ni safi. Maana umekuwa mpole kama mtetezi wa Mbowe maskini.

Wengi lakini hawavumi kutokana na humble lifestyle zao.....si unajua ulimbukeni wetu, we dont notice wasio na makeke.....

Tanzanianjema
 
Mwanakijiji hapa imebidi nicheke..

kule kwetu milimani mtu akijitahidi kuteremka akaingia mji kasoro bahari tayari watu wanaanza kumshughulikia..eti atawapiku wenzie kimaisha kwa kwenda mjini.

Nadhani mkakati wa kuwaweka minority kama decision makers unaweza ukawa tatizo kwani ethnic group yangu tunaweza kumalizana kwa kupewa nafasi adimu kama hiyo.
 
Ben, hebu nipe mfano wa kiongozi wa juu mchaga ambaye ni safi. Maana umekuwa mpole kama mtetezi wa Mbowe maskini.

Mama,

Kuna kama akina Dk.cyril Chami aliyekua deputy wa Bernard Membe,kuna akina Aggrey Mwamri ambae hata watu kutoka opposition walimkubali huyu jama ni mzalendo kweli kweli,rejea post ya Zitto kwenye ile thread iliyokua inawajadili akina Dk.Salim.

wengine walioko kama wangekua wachafu ni lazima wangekua wameshatangazwa kama Mramba.
 
Mi mchagga...na nimeandika hivyo makusudi kabisa ili kutia 'vionjo' vya kichaga

On a serious note,

Nawaomba mamods hii thread ifunguwe, itupwe kapuni for good. Na Mwanakijiji afungiwe walau kwa wiki moja.
Mwanakijiji, pamoja na kupendekeza ufungiwe bado hutatakiwa uingie JF manake najua uchagani haoakwepeki.....bisha..!

mamod hilo ndo wazo langu jamani......

teh teh teh teh tehhhhhhhhhhhhheeeeeeeeeeeeeeee. Report ndio mamod wataona, keleuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Yesu na Maria na Yosef, ha ha hahaaaaaaaaaaaaa. Jamani raha.........raha tupu JF, no wonder addicted.
 
uzuri wa mada hii ni kuexplore our ouw sentiments kuhusu makabila mengine. Je unafikiri wewe ni mkabila unapowafikiria watu wa makabila mengine in general terms? Well, wakati mnaendelea kujadiliana nakimbia kuwaletea taarifa ya habari ya saa mbili kupitia KLH News.. be the first to know, what people will be talking about tomorrow!
 
Wengi lakini hawavumi kutokana na humble lifestyle zao.....si unajua ulimbukeni wetu, we dont notice wasio na makeke.....

Tanzanianjema

kweli mkuu,

Kwa mfano Mramba msemo wake wa kutoa wito kwa watanzania kula majani ili ndege ya Rais inunuliwe ulimfanya awe celeb sana.Bado nailaaani kwa nguvu kubwa ile kauli yake ya roho mbaya na kiburi cha shetani!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom