Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
na siku akiwepo, ndipo nchi itakapouzwa! meaning hata mbowe asiote kuwa rais, alishindwa mrema then mbatia au prof shao/yo waote urais???

Claopa Mpare yule babu

kwani kuna tofauti kati ya wapare na wachaga? si wote wanatokea moshi...
 
...kwa hiyo na rais aruhusu waajiri wakwere, wamasai, waha, wahadzabe na wengineo ambao hawana qualifications ili tu kuwaeliminate wachagga?

Mwanakijiji umekuwa ukitetea Wachaga all along tokea controversy la Uchaga wa CHADEMA liibuke, unasema wako targeted.

Naomba tafadhali utetee hao wanne waliotandikwa dongo baya kama la nguoni hapo juu.
 
kwani kuna tofauti kati ya wapare na wachaga? si wote wanatokea moshi...

hiyo mada ingine kabisa, maana huko kuna wapare na wachaga. Ujue sumu ya ubaguzi haiishi katika wapare kuna wambughu sijui, wachome, wasangi na katika wachaga waorombo, wakibosho, wamachame, wamarangu, wauru, wamarangu. Kwenye wamarangu kuna wakilema, wakirua, wa vunjo, wa mamba, wa marangu mtoni, wa samanga, wa himo. Kazi ipo.
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.

Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.

Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".

Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.

Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.

Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.

Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.

Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.

Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.

Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.

Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.

Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.
wewe huna mpango na dhidi siku zinavyozidikenda ndio jinsi uwezo wa upeo wako unavyozidi kujionyesha na kwamba wewe si lelote zaidi ya limbukeni na uliyejaa chuki kwa kwa watu wenye asili ya kiafrika ambao kwa bahati mbaya au nzuri wewe umetokea kuwa mmoja wapo....
Si zamani sana hapa watu walikuwa walikuwa wanongelea juu ya ms tz kuwa mhindi na wewe ulikuwa wakwanza kumteteta na kuwaita woote waliokuwa wanampinga wabaguzi, sasa cha ajabu ni kwamba leo hii unawaona wachaga ambao ni watu wenye asili ya kiafrika ambao asili yao ktk sehemu ambayo leo inajulikana kama tanzania inarudi miaka mingi sana, hawafai na wapigwe vita kutokana na maneno yako wakati kila mtu anafahamu mchango mkubwa wa wachaga ktk taifa letu baadhi yetu hata tusingeweza kusoma bila shule za wazazi zilizojengwa na hawa watu, baadhi yetu tusingepata kazi bila makampuni yaliyoanzishwa na kuendeshwa na wachaga, mchango wa wachaga kwa taifa kiuchumi ni mkubwa sana kiasi kwamba nashangaa mtu ambaye anjifanya ni mpigania haki ya watz anshindwa kuliona hilo na kuanza kuwapiga vita....
Kwa taarifa yako wachaga wanaotorosha mali ya tz nje ya nchi niwachache sana ukilinganishwa na hao wahindi unaowatetea...
Jikomboe ndugu, tatizo lako wewe SI LINGINE BALI CHUKI BINAFSI UNACHUKIA KILA KITU CHEUSI NA CHA KIAFRIKA NA KUTUKUZA KITU CHECHOTE KISICHO CHA KIAFRIKA NAJUA BADO HAUJAWEZA KUJIKOMBOA KUTOKA KTK FIKRA ZA CHUKI BINAFSI ULIZOPANDIKIZWA KWENYE SHULE YA MISHENI ULIHUDHURIA (sina uhakika lkn nahisi ulisoma shule za misheni za wazungu), NA SASA NAAMINI KWAMBA ADUI YETU MKUBWA HAYUPO MBALI BALI NI HAPA HAPA KWETU NA NI LAZIMA TUANZE KUSAFISHA NYUMBANI KWETU KWANZA NA INABIDI TUANZE NA WATU KAMA WEWE KAMA KWELI TUNATAKA KUPIGA HATUA MBELE......
 
na siku akiwepo, ndipo nchi itakapouzwa! meaning hata mbowe asiote kuwa rais, alishindwa mrema then mbatia au prof shao/yo waote urais???

Claopa Mpare yule babu


Mama,
Na hizi fikra ndizo tunajaribu kuzibadilisha sasa.Ila sidhani kama utakua uanawatendea haki.
 
Mama,
Na hizi fikra ndizo tunajaribu kuzibadilisha sasa.Ila sidhani kama utakua uanawatendea haki.

maana thread inasema waachie ngazi, kwani hao sio wachaga na wao waachie ngazi, what so exceptional with uchaga wao hadi useme hawatendewi haki?
 
hiyo mada ingine kabisa, maana huko kuna wapare na wachaga. Ujue sumu ya ubaguzi haiishi katika wapare kuna wambughu sijui, wachome, wasangi na katika wachaga waorombo, wakibosho, wamachame, wamarangu, wauru, wamarangu. Kwenye wamarangu kuna wakilema, wakirua, wa vunjo, wa mamba, wa marangu mtoni, wa samanga, wa himo. Kazi ipo.

Ayayayayayaaaa.....wewe ndio umefungua kopo la nyungunyungu sasa....mwenzio hata nilikuwa sijui wapi wanatokea wapi zaidi ya Moshi....kumbe hata wao kwa wao wamegawanyika hivyo....I give up....sote ni Watanzania tu....
 
hivi na Kimei yule managing director wa CRDB ni mchaga eeh, bahati mbaya Mgonja katibu mkuu wa wizara ya fedha sijui ni Mpare.
 
maana thread inasema waachie ngazi, kwani hao sio wachaga na wao waachie ngazi, what so exceptional with uchaga wao hadi useme hawatendewi haki?

Mama,
Namaanisha huwatendei haki wachaga ukisema kama akiwa rais mchaga ndio nchi itauzwa.
 
Mama,
Namaanisha huwatendei haki wachaga ukisema kama akiwa rais mchaga ndio nchi itauzwa.

ahaaaaaa, ok! lakini unakubali kuwa mchaga yeyote hafai kugombea urais kwa jinsi walivyoonyesha mbegu ya ukabila ka ilivyoelezwa kwenye thread hii?
 
Ni kweli Kilmanjaro wachagga pia ni tofauti na kulikuwa na mapigano sana kati yao kipindi cha nyuma na sasa wanaishi pamoja tu.
Hata hawa wamarekani wenyewe walishapitia civil wars karne nyingi zilizopita!
Hatuna haja ya kupitia huko kama tutajifunza kutokana na makosa ya wenzetu!
Hivyo basi Taifa zima lijifunze kutoka KILIMANJARO kwani ni makabila ambayo yalishapigana sana na sasa yameamuwa kukaa pamoja!
Hata wapare na Wachagga walizipiga sana tu!
Na hata kabila la Mbowe la machame nao walizipiga sana tu na Wakibosho!
NI MUHIMU TAIFA LIKAJIFUNZA NA LIFUATE MFANO WA WAZALENDO WALIOAMUA KUKAA PAMOJA LICHA YA OTAFAUTI WA LUGHA NA UTAMADUNI!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom