Je, Unajua nini kuhusu "Psychological Manipulations",Jinsi ya kuziepuka Na sheria Ya Tanzania inasemaje kuzihusu?

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,586
17,705
Habari Za Muda huu wanajamvi!

Leo ni siku ambayo ningependa kushare kidogo kuhusu Aina ya mtu kuongozwa kiakili na kufikia kufanya maamuzi kinyume na matakwa yake (Psychological Manipulation).

Kwa kwa kuanza
Nini maana ya Psychological Manipulation?

Psychological Manipulation ni aina ya ushawishi ambayo hutumia Udanganyifu ama ulaghai,au mbinu nyingine yoyote kudhibiti mawazo, fikra,hisia au tabia za mtu mwingine kwa madhumuni mengi ikiwemo kupata Nguvu ,au udhibiti juu ya mtu mwingine,ili afanye jambo ambalo hataki kufanya au kumfanya ajisikie tu kufanya jambo hilo kwa namna moja ama nyingine....

Kuna aina nyingi Sana za Psychological Manipulation ila kwaeo nitadeal na Aina chache tu kwa siku ya leo..

Gaslighting hii inahusisha na kumfanya mtu atilie shaka hisia zake, Imani yake, atilie shaka fahamu wake wa jambo katika uhalisia wake ,mtazamo wake na hata kumbukumbu zake..

(Mtanisamehe kwa watu wa Dini maana mfano wa kwanza utakuwa wenu)
Hapo zamani waafrika walikuwa wakiamini katika dini zao kabla ya kuja kwa wakoloni (Waarabu na wazungu) na kuweka Mashaka mengi katika dini zao na Miungu yao na kuwafanya Wao waache dini zao za asili na kuanza kufata dini mpya...

Au mfano wa pili..

Zamani Tulikwa na Elimu Zetu ambazo watoto walirithi kazi na ujuzi kutoka kwa babu na baba zao nyumbani kwa mfano baba alikuwa mvuvi hivyo alimfundisha mwanae uvuvi au Baba akiwa mhunzi alimfundisha Uhunzi mwanae au baba au babu akiwa Mganga alimfundisha mwanae uganga na kila familia ilifahamika kwa ujuzi fulani kutkana na elimu ya kurithishana kabla ya kuja wazungu na kutuwekea mindset ya Gaslighting na wakaita elimu hiyo kuwa ni Informal Education na wakatuletea Pyramid Education na wakaiita Formal education...

INAENDELEA......

Soma hapa jwa muendelezo

Inaendelea

Guilt-tripping hii ni aina nyingine ambayo humfanya mkusudiwa kujihisi kuwa ana hatia kufanya au kutofanya jambo ili tu utimize matakwa yako ya udanganyifu...

(Nisameheni watu wa dini lakini n katika kuelewesha vizuri )

kwa mfano unaweza Kumwambia kuwa mtu akisema uongo ametenda dhambi hii itamfanya ajihisi ana hatia kila anaposema uongo na utampa suluhisho la kujikosha hiyo hatia...

au kumwambia kuwa akipenda watu wa jamii fulani ni kosa ilimradi tu apende jamii nyingine tofautu na hiyo...

aina nyingine ambayo hufanana na iliyopita ni Intimidation ambayo yenyewe huusika na kushawishi kwa kwa kumtishia au kufanya aogope kufanya kitu fulani..
kwa mfano kumwambia kuwa ukifanya hivi unakufa au utapatwa na kifu fulani hatari au utapoteza mali zako...

aina hizi mbili zote hutumiwa sana na Baadhi ya Askari wa kwetu wasio waadilifu na wanaokosa Taaluma na Skills za kuhoji watuhumiwa...

Covert persuasion hii nahisi ndo hutuniwa kwa ukubwa sana hasa mtu anapotaka kufanya biashara au kutafuta mwenza..
kwenye aina hii mtu hushawishiwa bila wao kujua kama wameshawishiwa hii hutumiwa hasa kwenye biashara katika Upande wa Masoko (Marketing), pia inaweza kufumika katika sehemu mbalimbali kama Kwenye siasa na Kwenye kupata mwenza au kweny mahusiano..

sasa mtu anashawishiwa vipi na Aina hii ya covert Persuasion hii ni kw kutumia Njia kama
subliminal Messaging hii hutokea katika sehemu muhimu ya ubongo (Subconcious Mind), na huanza kwa kasi sana kupokea Jumbe za Ushawishi huo kupitia Sauti uliyosikiliza, picha ulizoona na Video ulizoona na kuangalia au maandishi uliyosoma...Ubongo Taratibu huanza kuchambua na kuanza kupokea ushawishi huo bila kujua na mwiso wa siku kujikuta katika upands asioutaka...

kwa mfano..Hujawahi kukaa muda ukasikia nyimbo huipendi lakini baadae baada ya kupigwa sana ukahisi unaipenda hii ndo kazi ya Subliminal messaging...

au kwa wasichana unaweza ukatongozwa na mtu usiyemjua lakini baada ukaanza kupokea Picha zake sauti yake ubongo ukaanza kuchakata muonekano wake na Hata maneno yake ukajikuta unampenda bila wewe kujua hivyo ndivyo hutokea...

Inaendelea hapa
 
Inaendelea ....

katika covert persuasion Pia ukiacha Sublimal kuna Framing ambayo unapresent kile kitu ambacho mtu anataka kusikia ili tu kumvutia kwa mfano mfanya biashara unaweza ukasema kwa mteja hii nguo hawezi kuchanika au "hii simu mkuu inashika Mtandao kuliko zote"

pia kuna Social proof hii wanatumia wasanii wa Tanzania unanunua bidhaa kwakuwa tu msanii fulani anayo au alikuwa nayo na unashawishika kwakuwa tu kitu hichi ni populara wala kiuhalisia hukihitaji ila tu kwa sababu hizo..

Njia ya mwisho wa covert ni Scarcity hii huwa naisikia sana ni aina ya covert ya kutengeneza uchache wa kitu au bidhaa ili kufanya kionekana kichache ili kusababisha Ushawishi wa moyo kwa watu..Kwa mfano utamsikia mfanya biashara anasema wahi nafasi ni chache...

kwa leo hizi ,zinatosha japo ,inaweza kuongezeka kwenye comments

Sasa sheria ya Tanzania inasemaje kuhusu Psychological Manipulation... Kuna sheria kama tatu nitazipitia baadae
  • Penal Code (Cap 16):
  • Domestic Violence Act (No. 17 of 2004):
  • Children's Act (No. 21 of 2009)
 
Hii psychological manipulation ni jambo kubwa sana na linamhusu kila mtu dunia nzima, watu wote duniani watakuwa psychologically manipulated kwa namna moja au nyengine, ili binadamu aweze kuishi kwa Amani na wenzake ni lazima awe manipulated psychologically. Wanaotu-manipulate wanaamini hivyo

Kwa mfano hio aina ya gaslighting, inayomfanya binadamu atilie Shaka hisia na mawazo yake.
- Sote dunia nzima tumeaminishwa dunia inazunguka na tunaamini lakini hakuna mtu aliewahi kuihisi dunia ikizunguka, kwa maana hio hatuziamini hisia zetu kuwa haizunguki kwa sababu we have been manipulated kuamini kuwa hisia zetu haziwezi kunasa speed za dunia.

- pia tumeaminishwa kuwa kuwa jua lipo mbali sana lakini ukiinua uso jua lipo juu ya utosi na unaliona kabisa kuwa hakipo mbali lakini tumeaminishwa kuwa liko mbali sana, na tumebaki kuwa hatuziamini hisia zetu kwa sababu we’ve been manipulated ili tuamini tunavyoambiwa zaidi kuliko hisia zetu.

Au mfano mwengine uliotoa wa guilt-tripping inayomfanya mtu ajione Ana makosa fulani.

Hii aina ya manipulation inatuumiza sana binadamu sote, hii imekuja kupitia dini zetu, eti kuna mtu wa mwanzo Anaitwa Adam Aliambiwa asile tunda na akala baada ya kula watu wote duniani wakawa wana makosa kwa sababu yake, kwa hio watu wanaozaliwa duniani wote wamekosea na wanahitaji kuokolewa na kuna mtu mwengine anaitwa issa/Jesus/yesu yeye ndio anakuja kuwaokoa watu kutoka kwenye makosa hayo ya asili. Mtu umeanza kuzaliwa, umemkosea nani,lini kwa sababu gani? hata hujui maana ya kukosea ni nini unaaminishwa wewe ni mkosa, na unaamini kabisa unahitaji kuokolewa na kusafishwa makosa na unaisha miaka yako yote duniani unaamini wewe ni mkosa na unakuwa unahisi guilty aina Fulani hivi, yote kutokana na uongo tulioaminishwa kupitia psychological manipulation.

Haya yote sio kweli ni mambo ya kutunga tu ila kwetu sisi tusio jua tunaamini kuwa ni ukweli kwa sababu we have been psychological manipulated

Kwa ufupi misingi yetu ya kimaisha yote imejaa manipulation, kuanzia dini, elimu,science, pesa, n.k vyote hivyo vinatuingiza katika mfumo wa utumwa lakini kwa sababu tunaingia utumwani kupitia psychological manipulation tunakuwa hatujui na tunakuwa tuna furahia kuwa watumwa bila ya kujijua na tunahakikisha kuilinda mifumo ya utumwa proudly milele
 
Duuuh.....
Unaposema ishu ya jua na dunia kuzunguka..
Wanasema uwezi amini milango yako ya fahamu bila kufanya uchunguzi.

Mfano rula unapoiweka kwenye kopo la maji ukiangalia inaonekana kama imepinda.
Sasa mtu atakapokuambia ile rula haijapinda ila ni ni effect ya mwanga napo utasema kuwa amefanya gaslighting au ?
 
Hii psychological manipulation ni jambo kubwa sana na linamhusu kila mtu dunia nzima, watu wote duniani watakuwa psychologically manipulated kwa namna moja au nyengine, ili binadamu aweze kuishi kwa Amani na wenzake ni lazima awe manipulated psychologically. Wanaotu-manipulate wanaamini hivyo

Kwa mfano hio aina ya gaslighting, inayomfanya binadamu atilie Shaka hisia na mawazo yake.
- Sote dunia nzima tumeaminishwa dunia inazunguka na tunaamini lakini hakuna mtu aliewahi kuihisi dunia ikizunguka, kwa maana hio hatuziamini hisia zetu kuwa haizunguki kwa sababu we have been manipulated kuamini kuwa hisia zetu haziwezi kunasa speed za dunia.

- pia tumeaminishwa kuwa kuwa jua lipo mbali sana lakini ukiinua uso jua lipo juu ya utosi na unaliona kabisa kuwa hakipo mbali lakini tumeaminishwa kuwa liko mbali sana, na tumebaki kuwa hatuziamini hisia zetu kwa sababu we’ve been manipulated ili tuamini tunavyoambiwa zaidi kuliko hisia zetu.

Au mfano mwengine uliotoa wa guilt-tripping
Hii aina ya manipulation inatuumiza sana binadamu sote, hii imekuja kupitia dini zetu, eti kuna mtu wa mwanzo Anaitwa Adam Aliambiwa asile tunda na akala baada ya kula watu wote duniani wakawa wana makosa kwa sababu yake, kwa hio watu wanaozaliwa duniani wote wamekosea na wanahitaji kuokolewa na kuna mtu mwengine anaitwa issa/Jesus/yesu yeye ndio anakuja kuwaokoa watu kutoka kwenye makosa hayo ya asili.

Haya yote sio kweli ni mambo ya kutunga tu ila kwetu sisi tusio jua tunaamini kuwa ni ukweli kwa sababu we have been psychological manipulated

Kwa ufupi misingi yetu ya kimaisha yote imejaa manipulation, kuanzia dini, elimu,science, pesa, n.k vyote hivyo vinatuingia katika mfumo wa utumwa lakini kwa sababu tunaingia utumwani kupitia manipulation tunakuwa hatujui na tunakuwa tuna furahia kuwa watumwa bila ya kujijua
Dah Mkuu Umemaliza kila kitu Umeongea Ukweli mtupu sana🎉🎉
na Ubaya wa manipulation....The manipulated part huwa inajiona kuwa Inajua kile kitu ambacho imeaminishwa hata kukitokea Mtu wa kumwambia kuwa kile kitu sio sahihi bado atakubishiaa....

Nimewahi kusikia Mfano mmoja hivi sehemu (Nitauhadithia)

Kuna jamii fulani iliyoishi eneo fulani walikuwa na desturi ya kutumia Mapango kama nyumba na walikuwa wakitembea kwa kuinama waliamini kuinama ndo kutembea sahihi au kuinama kwao ilikuwa jadi kwani baadhi yao tangu wanazaliwa wakiona watu wakiinama au kutembea kwa kuchutama walikuwa wamejizoesha kiasi kwamba hakuna aliyewahi kujua kwamba kuna watu wanaishi kwenye nyumba na wanatembea bila kuinama na wanavaa nguo...

Walikuwa wakitaka chakula Wanaenda kwa wazee wanaita chakula.. kinatokea (Hii ilikuwa kama research project kwahyo walipokuwa wakiita Ma researcher walipeleka chakula bila wao kujua ila waliona kama kitu kinaleta wakaamini kuwa huyo ndo Mungu huwa anawaletea)...

Baada ya Miaka Takribani 120 kwenye Hio hali vilipita vizazi kama vinne na hiyo ilirithishwa kwa kizazi..

Sasa Reseachers (Waliokuwepo kwa wakti huo wa project) walituma mtu akaangalie ndani wale watu kwanza walishangaa kuona mtu anatembea bila kuinama ,Pili walishangaa kuona anatoa kavaa nguo na alipojaribu kuwaambia kwamba kuna sehemu kuna watu kama yeye walishangaa na aalimkatalia na wengine walimdhihaki wakiamini ni mzimu .....

Sasa hivyo ndo Manipulation hufanyika..
Ubaya wa Manipulation Huingia kwwnye subconsious na hurithiswhwa kwa vizazi mpaka vizazi kwahyo mtu kujua kama Kadanganywa ni vigumu sana kuamini..

Mkuu umemaliza kila kitu
 
Duuuh.....
Unaposema ishu ya jua na dunia kuzunguka..
Wanasema uwezi amini milango yako ya fahamu bila kufanya uchunguzi.

Mfano rula unapoiweka kwenye kopo la maji ukiangalia inaonekana kama imepinda.
Sasa mtu atakapokuambia ile rula haijapinda ila ni ni effect ya mwanga napo utasema kuwa amefanya gaslighting au ?
Mkuu umewahi kufanya uchunguzi ukagundua ulichosema au kuna watu walikuambia Hivyo..

Kuna aina moja ya psychological manipulation sikuitaja Inaitwa Brain washing..
Hii humfanya mtu kuamini kwamba kinachosemwa ni kweli kwa kutengeneza Facts ambazo ni za kweli kwenye kitu cha uongo..
Ndo maana mpaka leo kuna Watu bado wanadebate kuna wanasayansi wengine wanasema Dunia iko flat wanajiita Flat Earth scientis na kuna wanaosema iko round..
Na mkuu Hizo theory za Mwanga and everything it was brainwashing mechanism kukuandaa kwa ajili ya kukubali baadhi ya theory kubwa
 
""""Mkuu umewahi kufanya uchunguzi ukagundua ulichosema au kuna watu walikuambia Hivyo..""""
Kitu gani kwa mfano...?

"""Hii humfanya mtu kuamini kwamba kinachosemwa ni kweli kwa kutengeneza Facts ambazo ni za kweli kwenye kitu cha uongo.."""
Nini maana ya fact...?

"""Ndo maana mpaka leo kuna Watu bado wanadebate kuna wanasayansi wengine wanasema Dunia iko flat wanajiita Flat Earth scientis na kuna wanaosema iko round.."""
Unefuatilia kuwa hizo deabate mpaka leo zipo..???
 
""""Mkuu umewahi kufanya uchunguzi ukagundua ulichosema au kuna watu walikuambia Hivyo..""""
Kitu gani kwa mfano...?
Kwa mfano ulicho doubt kuhusu Alichosema mchangiaji kabla kuhusu dunia kuzunguka Jua..

Ndo nikauliza Umewahi kuprove wewe mwenyewe kwa uwezo wako?
Au Umesoma Walichoandka waliosema kufanya...?

"""Hii humfanya mtu kuamini kwamba kinachosemwa ni kweli kwa kutengeneza Facts ambazo ni za kweli kwenye kitu cha uongo.."""
Nini maana ya fact...?
Facts ni Kitu au hoja iliyokuwa proved kwamba ni ya ukweli...
Sasa hapa ndo kuna changamoto kuwa nini na nani ataprove facts hizo..

Kwa mfano siwezi nikasema kuwa Giza ni jeusi alafu nije mimi huyo huyo nikueleza weusi ni nini.. hapo nitakuwa natengeza Mazingira ya kuprove nilichosema mwanzoni na ndivyo ilivyotokea...

Kingine si kile kitu chenye ukweli kinaweza kuwa Proved na sio kila Facts Iliyokuwa Proved ni ya ukweli..

"""Ndo maana mpaka leo kuna Watu bado wanadebate kuna wanasayansi wengine wanasema Dunia iko flat wanajiita Flat Earth scientis na kuna wanaosema iko round.."""
Unefuatilia kuwa hizo deabate mpaka leo zipo..???
Yeah mpaka leo hii navyoongea na wewe zipo na kuna moja Juzi walikuwa wanabishana kuhus kutokea kwa thunder and thunderstorm kuwa kunaprove that dunia Ni Dom iliyoflat settled na sio Duara...

Kuna Jama mmoja aliweka Hizo hoja kwenye Ticktok pia ila ndiyo hoja zinazofanyiwa uchunguzi na moja ya sehemu walipofanya uchunguzi ni kwenye nuclear plant..
 
Habari Za Muda huu wanajamvi!

Leo ni siku ambayo ningependa kushare kidogo kuhusu Aina ya mtu kuongozwa kiakili na kufikia kufanya maamuzi kinyume na matakwa yake (Psychological Manipulation).

Kwa kwa kuanza
Nini maana ya Psychological Manipulation?

Psychological Manipulation ni aina ya ushawishi ambayo hutumia Udanganyifu ama ulaghai,au mbinu nyingine yoyote kudhibiti mawazo, fikra,hisia au tabia za mtu mwingine kwa madhumuni mengi ikiwemo kupata Nguvu ,au udhibiti juu ya mtu mwingine,ili afanye jambo ambalo hataki kufanya au kumfanya ajisikie tu kufanya jambo hilo kwa namna moja ama nyingine....

Kuna aina nyingi Sana za Psychological Manipulation ila kwaeo nitadeal na Aina chache tu kwa siku ya leo..

Gaslighting hii inahusisha na kumfanya mtu atilie shaka hisia zake, Imani yake, atilie shaka fahamu wake wa jambo katika uhalisia wake ,mtazamo wake na hata kumbukumbu zake..

(Mtanisamehe kwa watu wa Dini maana mfano wa kwanza utakuwa wenu)
Hapo zamani waafrika walikuwa wakiamini katika dini zao kabla ya kuja kwa wakoloni (Waarabu na wazungu) na kuweka Mashaka mengi katika dini zao na Miungu yao na kuwafanya Wao waache dini zao za asili na kuanza kufata dini mpya...

Au mfano wa pili..

Zamani Tulikwa na Elimu Zetu ambazo watoto walirithi kazi na ujuzi kutoka kwa babu na baba zao nyumbani kwa mfano baba alikuwa mvuvi hivyo alimfundisha mwanae uvuvi au Baba akiwa mhunzi alimfundisha Uhunzi mwanae au baba au babu akiwa Mganga alimfundisha mwanae uganga na kila familia ilifahamika kwa ujuzi fulani kutkana na elimu ya kurithishana kabla ya kuja wazungu na kutuwekea mindset ya Gaslighting na wakaita elimu hiyo kuwa ni Informal Education na wakatuletea Pyramid Education na wakaiita Formal education...

INAENDELEA......

Soma hapa jwa muendelezo

"Wazungu na na Waarabu" walianza kuja lini na wapi?

Unaelewa lini kuwa umefanyiwa "manipulation"?
 
Back
Top Bottom