chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,009
- 20,683
Taifa linatarajia kuwa na mpango wa maendeleo wa miaka 25, 2025-2050. Mpango huu naona kama haupati kutangazwa vya kutosha kwa wananchi ili wajue mkoa/wilaya yao inatakiwa kuwa namna gani katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Wakijua ndipo watahoji kwa nini miaka 25 imepita na hakuna lililofanyika.
Kwanza nilitarajia mjadala wa kisomi ungeendeshwa na wasomi wetu kuujadili mpango wa maendeleo unaokwisha muda wake ili kujua ulivyofanikiwa, na ulipata changamoto zipi, na zinatatuliwaje na mpango mpya wa maendeleo.
Bahati mbaya hakuna mjadala wowote ule, hata REPOA kwa sasa imepoa, watu wa elimu, vyama vya wakulima, NGO na wengine "hawasemi" sana siku hizi. Vyama vya siasa vyenyewe vinawaza madaraka tu, vinaimba katiba kama vile itachapisha hela.
Binafsi ningependa kila mkuu wa mkoa afanye presentation katika television au media ya mkoa, lengo iwe kuonyesha katika mkoa wake na wilaya zake, wamepanga dira gani katika miaka 25, na waivunjevunje katika miaka mitano mitano.
Na kila waziri pia afanye hivyo.