Dira ya maendeleo 2050 na Katiba Mpya

EMACHA

Senior Member
Jul 16, 2021
147
187
Ni hivi karibuni serikali imezindua mchakato wa kuandika Dira ya maendeleo ya mwaka 2025 - 2050 (au pendine zaidi, kadiri itakavyopendekezwa).

Jambo hili ni jema kwa sababu, kama Taifa, mipango ya maendeleo ya muda mrefu ni muhimu ili kujenga uelewa wa pamoja wa nini tunahitaji na wapi tunapenda kufika. Jambo jipya katika mchakato huu, ni ushirikishwaji mpana wa wananchi kwa makundi mbalimbali katika kutoa maoni yao.

Katika kudodosa hadidu za rejea zitakazotumiwa na Tume ya kukusanya maoni kuhusu Dira ya Maendeleo 2050, nimebaini kuwa Tume hii itakumbana na maoni yanayowiana na maoni ya kuandika Katiba mpya!

Tufahamu kuwa Katiba mpya iliyokuwa ikikusudiwa kuandikwa hapa nchini, ndiyo iliyokusudiwa kutoa dira ya Taifa gani tunapaswa kulijenga kwa kipindi kirefu kijacho.

Kwa mfano Dira 2050 inakusudiwa kuweka maadili ya kitaifa, ambalo ni moja ya mapendekezo yaliyokusudiwa kuwemo katika Katiba mpya (rejea Rasimu ya Tume na Katiba pendekezwa).

Kwa kifupi tulipaswa kuanza na Katiba mpya (kama Sheria kuu) na kisha kuendelea na Dira 2050 au zaidi). Katiba mpya pia ingetupatia msingi wa kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi (ambayo tayari muswada wa sheria hii upo Bungeni). Lakini pia Watanzania tuna bahati kuwa tuliwahi kuwa na Azimio la Arusha, mbayo ilikuwa ni Dira ya Taifa hili kwa miaka yote.

Azimio hili ndilo liliweka misingi ya Utu, Usawa, Maadili na hata kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho.

Azimio hili ndilo liliweka misingi ya Umoja na Utaifa tulionao leo. Japo si kila kilichopo ndani ya Azimio kinakidhi mahitaji ya leo; lakini angalau tunalo andiko (document) muhimu la kuweza kurejea.

Kwa kuhitimisha, niombe tuendelee kushiriki mchakato huu kwa kadiri ya mtu/kundi watakavyoguswa. Lengo ni kuhakikisha mchakato unakuwa shirikishi na jumuishi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mnapenda kila kitu kizuri mkichanganye na siasa zenu. Maendeleo na katiba ni vitu viwili haviusiani kabisa, ingekuwa hivyo Dubai ingekuwa maskini wa kutupwa.
Maendeleo ni brain tu.
 
Mnapenda kila kitu kizuri mkichanganye na siasa zenu. Maendeleo na katiba ni vitu viwili haviusiani kabisa, ingekuwa hivyo Dubai ingekuwa maskini wa kutupwa.
Maendeleo ni brain tu.
Huwezi kutenganisha maendeleo na katiba katika ulimwengu wa leo.
 
Back
Top Bottom