Changia maoni yako kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025-2050 ili serikali ichukue mapendekezo yako

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na utekelezaji wa dira ya maendeleo unaoishia 2025.

Kuna mengi yataelezwa leo pale ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma mafanikio na changamoto kwa Dira ya maendeleo inayoishia 2025 na uzinduzi wa ukusanyaji wa maoni juu ya uundwaji wa Dira mpya ya maendeleo 2025-2050.

Dira ya maendeleo inayoishia 2025 serikali imejitahidi kwenye elimu na maji kwa asilimia 75 kufikia 2025 nadhani watakuwa wamefika asilimia 85,nyanja zingine bado sana.

Dira ya maendeleo 2025-2050 michango ni kama ifuatavyo:

1,Sekta ya kilimo bado sana,wakulima wengi wa nchi hii wanategemea kilimo cha jembe la mkono na mvua za msimu,Profesa Kitila hii ni aibu sana ,tunataka kufikia 2050 asiwepo mwananchi anayelima kwa jembe la mkono na msimu bali mashine na umwagiliaji na hapa ndo tatizo la ajira litapungua,vijana watapenda kilimo kuliko ilivyo sasa (Kilimo cha kijima hiki)

2,Viwanda bado sana na hii ni kutokana na kilimo cha kijima,boresha sekta ya kilimo automatically Viwanda vitakuja,wawekezaji watakuja wenyewe ikiwa kilimo kitaboreshwa ipasavyo.

3, Mazingira,tunataka kwenye Dira ya maendeleo 2025-2050 matumizi ya nishati mbadala yawe yamefikia asilimi 100,weka mkakati wa kila kaya kutumia gesi,umeme wa sola na kupunguza bei ya nishati hiyo ilingane na kuni na mkaa kama ilivyo mtaani katika matumizi ya kupikia ili kupunguza kiwango kikubwa cha kupikia mkaa na kuni ili kutunza mazingira.

4. Tuangalie pia population na rasilimali zilizopo kama vinaendana, watu wanazaliana kwa kasi lakini hatuoni mipango ya kuwawezesha watu hao kuajirika, tunaona vijana wengi wanakimbilia boda boda na jobless ni wengi sana mtaani hii ni hatari kwa usalama wa nchi.

5. Makazi ya watu bado ni duni sana,watu wanaishi kwenye nyumba za makuti, nyasi na tope, tunataka mkakati wa kuondoa makazi duni kwa kila Mtanzania kufikia 2050, mje na mkakati namna ya kuboresha makazi ya watu.

6. Matumizi ya ardhi bado sana, thamani ya ardhi kwenye hii nchi ipo chini sana, kasi ya upimaji ipo chini na ni gharama sana, na pia ondoa kipengele cha kwenye katiba kinachomilikisha ardhi ya nchi kwa Rais badala yake umiliki uwe kwa mwananchi moja kwa moja.

Ongezea mengine, Mheshimiwa Profesa Mkumbo atayaona.
 
Kwanza Disemba 9 kuna maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika. Na siyo Uhuru wa Tanzania Bara.

Halafu chini ya huu utawala wa CCM, sidhani kama nchi ina dira yoyote ile ya maendeleo. Zaidi naona kuna dira ya kuifanya CCM kuendelea kubakia madarakani, na pia viongozi wake kuendelea tu kufaidi keki ya Taifa! Huku mamilioni ya wananchi wengine wakiendelea kuishi katika dimbwi la umasikini.

To me, dira bora kabisa ya maendeleo nchini mwetu; ni ile ya kuiondoa tu CCM madarakani.
 
Sawa mkuu
 
Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na utekelezaji wa dira ya maendeleo unaoishia 2025.

Kuna mengi yataelezwa leo pale ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma mafanikio na changamoto kwa Dira ya maendeleo inayoishia 2025 na uzinduzi wa ukusanyaji wa maoni juu ya uundwaji wa Dira mpya ya maendeleo 2025-2050.
Hatutaki mbona mengine wanapitisha wao kimya kimya.
 
Nadhani kwa haya mabadiliko ya mtaala wa Elimu uliofanywa kama utakuwa Kama ulivyo kwenye makaratisi Basi tutapiga hatua Sana ila Kama utakuwa tofauti basi tutalia Kama tulivyo lia kwenye BRN na BBT
 
Mpk leo bado hamjaunganisha Kwa lami barabara zinazounganisha wilaya nyingi mfano mtwara-Tandahimba-N ewala-Newala.Liwale-Nachingwea.Mtama-Newala.Ruangwa-Nachingwea.

Kuhusu maji mleta mada ni muongo hiyo 75% labda ya kwenu na bibi Yako.

Elimu nako hali tete madawati hamna walimu pungufu..

Kwahiyo ni wazi taifa halina dira
 
Maoni yako ni muhimu sana kutengeneza Dira ya maendeleo ya Taifa
 
Yaani bila KATIBA MPYA ni yaleyale huwezi kuwa na sheria za kikoloni za miaka 58 zifanye kazi kwenye hiyo mipango,maana sheria za watu masikini Tanzania zinafanyakazi vizuri lakini zile za viongozi hazifanyikazi,sarakasi za CAG nafikiri wote tumeona zinavyogeuzwa kama chapati za kihindi
 
Kujitahidi kwenye elimu ni kutoa elimu ya kisasa na bora inayomkomboa yule anaeipata na jamii yake, yaani elimu inayotatua changamoto za jamii. Elimu iliyopo ni ile inayozalisha wasomi vilaza na wasiojitambua. Pili kama ndani ya miji mikubwa kuna tatizo la maji ni dhahiri hiyo shida ya maji ni kubwa na pana. Hiyo 75% umeipata kwa kuzingatia factor zipi?
 
Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na utekelezaji wa dira ya maendeleo unaoishia 2025.

Kuna mengi yataelezwa leo pale ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma mafanikio na changamoto kwa Dira ya maendeleo inayoishia 2025 na uzinduzi wa ukusanyaji wa maoni juu ya uundwaji wa Dira mpya ya maendeleo 2025-2050.

Dira ya maendeleo inayoishia 2025 serikali imejitahidi kwenye elimu na maji kwa asilimia 75 kufikia 2025 nadhani watakuwa wamefika asilimia 85,nyanja zingine bado sana.

Dira ya maendeleo 2025-2050 michango ni kama ifuatavyo:

1,Sekta ya kilimo bado sana,wakulima wengi wa nchi hii wanategemea kilimo cha jembe la mkono na mvua za msimu,Profesa Kitila hii ni aibu sana ,tunataka kufikia 2050 asiwepo mwananchi anayelima kwa jembe la mkono na msimu bali mashine na umwagiliaji na hapa ndo tatizo la ajira litapungua,vijana watapenda kilimo kuliko ilivyo sasa (Kilimo cha kijima hiki)

2,Viwanda bado sana na hii ni kutokana na kilimo cha kijima,boresha sekta ya kilimo automatically Viwanda vitakuja,wawekezaji watakuja wenyewe ikiwa kilimo kitaboreshwa ipasavyo.

3, Mazingira,tunataka kwenye Dira ya maendeleo 2025-2050 matumizi ya nishati mbadala yawe yamefikia asilimi 100,weka mkakati wa kila kaya kutumia gesi,umeme wa sola na kupunguza bei ya nishati hiyo ilingane na kuni na mkaa kama ilivyo mtaani katika matumizi ya kupikia ili kupunguza kiwango kikubwa cha kupikia mkaa na kuni ili kutunza mazingira.

4. Tuangalie pia population na rasilimali zilizopo kama vinaendana, watu wanazaliana kwa kasi lakini hatuoni mipango ya kuwawezesha watu hao kuajirika, tunaona vijana wengi wanakimbilia boda boda na jobless ni wengi sana mtaani hii ni hatari kwa usalama wa nchi.

5. Makazi ya watu bado ni duni sana,watu wanaishi kwenye nyumba za makuti, nyasi na tope, tunataka mkakati wa kuondoa makazi duni kwa kila Mtanzania kufikia 2050, mje na mkakati namna ya kuboresha makazi ya watu.

6. Matumizi ya ardhi bado sana, thamani ya ardhi kwenye hii nchi ipo chini sana, kasi ya upimaji ipo chini na ni gharama sana, na pia ondoa kipengele cha kwenye katiba kinachomilikisha ardhi ya nchi kwa Rais badala yake umiliki uwe kwa mwananchi moja kwa moja.

Ongezea mengine, Mheshimiwa Profesa Mkumbo atayaona.
Kwani Dira hadi ya2050 ni ya kuboreshwa ama ndio tunaifikiria.Lucas tafadhali popote ulipo tupelo hint.
 
Hiyo yenyewe ya 2000 to 2025 wengi hawaijui inasemaje, imetekelezekaje, imefanikiwa nini, imefeli nini, kwanini, halafu tunakimbilia ya 50
 
Dira izingatie kuweka Branding moja au mbili za nchi, Ethiopia ni Anga, Kenya Utalii, Tanzania ingefaa ijiuze na kilimo kikubwa,endelevu na cha kisasa kuilisha Afrika Mashariki na Kati. Hivyo ijulikane unapotaja Tanzania popote ijulikane kwa kilimo kwa soko la ndani na nje kupandisha GDP. Uchumi wa kilimo uchukue nafasi ya kwanza kwetu.
 
Back
Top Bottom