Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050

Machepele

JF-Expert Member
Jun 28, 2019
289
419
Wasaalam!

Mabibi na Mabwana kabla ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya, lakini pia kwa kuniwezesha kuandika machache hapa.

Pili niombe sana Mods msifute, wala kuunganisha uzi huu na uzi mwingine, ili pengine kwa pamoja kama jamii tuwe na kitu cha kujifunza kutokana na uzi huu.

Mwisho tena kwa umhimu mkubwa, niwakaribishe tujadili kwa pamoja kuhusu hiki kitu kinachoitwa DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050.

Nianze na kuchambua kupata maana ya muunganiko wa maneno (DIRA, MAENDELEO na TAIFA).

DIRA = Dira ni kifaa/chombo/nyenzo ya kutambua mwelekeo.

MAENDELEO = mabadiliko yanayoonekana kuboresha hali ya binadamu, miundombinu na ujumla wake.

TAIFA = kundi la watu walio na lugha moja, historia, utamaduni, na (kawaida) eneo la kijiografia.

Hivyo ukisikia "Dira ya maendeleo ya Taifa" maana yake ni nyenzo mhimu inayotuonesha mwelekeo (wapi tunaenda ama wapi tutatakiwa kufika), katika maboresho ya hali ya binadamu (mtu/watu) wa taifa kwa muda fulani.

Kwa ufupi kabisa maana yake ni vipaumbele gani taifa linaweka ili kuhakikisha hali ya watu na miundombinu ina imarishwa na boreshwa zaidi.

Upo winbo wa Proffesor Jay & Mwana FA
Unaitwa ni 'Jukumu letu' nadhani waliandika wimbo huu kuhamasisha wananchi kuchangia maoni jinsi gani mpango wa maendeleo uwe.

Nikiri kuwa mimi nilizaliwa miaka ya 90's, na pengine ninaweza nisiwe na uelewa mpana zaidi ya haya masuala, nimepitia ile 'The vission 2025' inayoelekea ukingoni nikajiuliza maswali nikasema, nije hapa niulize haya yafuatayo:-

1. Dira ya taifa ilianza lini kwa hapa kwetu Tanzania?
2. Dira ngapi mpaka sasa zimesha wekwa katika utekelezaji?
3. Ni nani anahusika kuandaa?
4. Ni mchakato upi unatumika kuandaa?
5. Ni nani anathibitisha dira hii?
6. Nani hukagua kagua itekelezaji?
7. Je kila mwisho wa dira moja kunakuwa na honest reflection ya kile kilichofanyika katika mpango uliopita?
8. Hii dira imetengwa katika maeneo yapi mhimu?
9. Je inagusa kila sector?
10. Je, budget ya ufuatiliaji ipo ofisi gani?
11. JE KIKATIBA IMEKAAJE?

Maswali yangu yatanipa mwanga wa kuandika au kueleza zaidi, kuhusu uelewa wangu juu ya suala hili.

Karibuni kwa michango yenu.
Wasalaam na kalamu ya
Machapele wa Tanzania.
 
Imeandaliwa na ccm hakuna jipya.mkukuta,mkurabita etc etc etc zote hatujui ziliishia wapi.
 
Dira ya maendeleo ni kichaka kingine Cha kutupiga. Kwa hapa kwetu dira halisi ipo kwenye mtazamo na utashi wa rais aliye madarakani kwa muda huo. Hakuna popote rais anapobanwa kutekeleza hiyo dira. Hivyo mleta mada dira ya maendeleo sio kitu serious kihivyo. Kama unajadili unaweza kujadili kwa kujifurahisha tu, but nothing serious.
 
Back
Top Bottom