Je, umesikia habari za Uhakiki wa Leseni na Cheti Uliposomea Driving kwa Madereva ?

Samatime Magari

Senior Member
Feb 10, 2017
103
388
Fs70vPCWYAA3B4l

Je unajua kwamba kwa sasa ukitaka kurenew leseni ni mpaka uwe na cheti cha udereva, Yani cheti cha uliposomea udereva, sasa kama leseni ilikufata nyumbani jiandae. Sasa naweza jiuliza hii issue imetokea wapi, iko hivi..
.
Duru zinasema kuna mwamba mmoja maarufu kwenye ndondi alikua anapiga mvinyo, Hilo eneo walikuwepo pia wakuu wa vitengo nao wakipiga mvinyo soo jamaa mvinyo ulivyopanda akajimwambafy [akaropoka] alivyopata leseni, mind you jamaa ni muongeaji na anasauti kubwa..
.
Fs70-8mWcAAiIb9

So akawa anajisifu kuwa Yeye alitoa mipunga leseni ikamfata chumbani akiwa amelala, Wakuu wa vitengo walivyosikia hizi kauli hawakupenda, zilikua zinalichafua geshi, Sasa ikatolewa order kwamba kuanzia sasa utaratibu/sheria ifatwe kwa usahihi Yani ukihitaji leseni lazima uwe umepitia driving school inayotambulika, umegraduate/pass na umevaa joho..

Na hapa ndo Mwanasheria wa police Ndg Deus Sokoni [pichani hapo juu] akatoa taarifa kwamba kwa sasa watafanya uhakiki wa leseni na madereva na kama hauna cheti basi itakulazimu urudi shule ili uendelee kuendesha gari yako na Inasemekana watafanya ukaguzi so unatakiwa kutembea navyo..

Fs704QPWIAE7phx
Fs71bOJWwAApldm

Pia wamewapiga biti wamiliki wa driving school kutokuuza vyeti, Yani ikigundulika kuna cheti kimeuzwa na chuo flani wanafunga hicho chuo, So this is to say wako na database ya vyuo vyote nchini wanavyovitambua, Sasa mtoto wa dada anza kuandaa ada mapema urudi shule..

Binafsi nilikua naangalia applicability ya hili jambo bado naona chenga tu, Isije kuwa mwanya tena wa raia flani kujifanyia ustupid na pesa za watu. Anyway muda huwa ni mwalimu mzuri ngoja tuone hii itakavyokua Wachaga huwa wanamsemo unasema Time will tell ngoja tuone.

Fs712FMXgAAVFCS
Fs70lF6WIAEPlSD

Sasa Samatime Car Dealers kama kampuni kwa mwezi huu wa 4 tutatoa OFA ya kukupeleka Driving school BURE, Na hii itakua ni kwa wateja 2 tu watakao order gari kwa mwezi wa 4, Yani unaagiza gari, wakati gari inakuja wewe uko zako shule unasoma.

Uzuri hii haihitaji boarding, unless otherwise una Mahitaji maalumu au unahitaji nguvu za ziada kuelewa, Sasa lengo la hawa Jamaa [Police] wanasema ni kuhakikisha madereva wote wanasoma, Yani madereva wazijue sheria za barabarani na matumizi sahihi ya barabara, Ndugu nikutakie maandalizi mema unapojiandaa kurudi chuo.

Na kama uko interested na madini kuhusu magari basi follow kurasa zetu za jamii twiter, Instagram, facebook na tiko tok Ili next time usipitwe na madini tunayotoa hapa kwa ajili yako, Pia tuna free coaching groups za magari WhatsApp na telegram. Hapo ni kwa wapenda magari tu kama huyapendi pita kushoto mtu wa Mungu.

Fs72RCVXoAEhtx6
Fs7zpyVXsAEHIaQ
Fs7zOuHWcAAtl70
.
Hapo utakutana na wadau wa magari, wanasema wanazi + madini kwa undani zaidi kuhusu magari, Kama uko interested Bofya hii link [https://wa.me/message/FSJ6DHIDTAVDA1……] itakuleta WhatsApp then share jina lako na unako patikana, tutasave number yako then utaungwa..
.
Pia Kama unahitaji kuagiza gari Japan/Singapore/Uk etc karibu tutaku assist, Tuko na network ya trusted dealers kwa Japan, UK, Singapore, Thailand etc Dealers wanaotupa gari zenye ubora wa juu kwa bei safi.. . Tutafanya mchakato wako wa kupata gari kuwa rahisi + salama.
.
Simply bofya link kwenye Bio njoo WhatsApp au ofisini Posta Mpya Phoenix House mkabala na Mkapa tower tutaku assist + kukushauri, Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari utatupa hitaji lako tutakupa Ushauri pia then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice.
.
Fs75JXHXsAE3KBK
Fs753TDXwAAbz42
Fs75ivXXwAIYQQk
.
Utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo Plus utakua unapewa updates za gari yako on daily basis gari itafika itasajiliwa na utakabidhiwa ikiwa na BIMA 3rd part, Fire Extinguisher na Triangle.

Asante
Samatime Magari
0714547598
 
Leo nmepigwa mkono nikaombwa cheti

Nkabaki namshangaa traffic cheti cha nini wakati leseni mlitoa wenyew kushirikiana na TRA

basi nkawamwambia waanze kujihakiki wao kwann walitoa leseni bila cheti labla ya kuja kwetu tuone hatua gani za ndani wamechukua.

Mwsho nkamwambia sheria inataka niwe na leseni hii hapa swala la uhakiki nyie mnatakiwa muwe na database ingiza number au jina langu ikuletee chuo nlichosoma

Kama hamwezi hilo basi andika fine niondoke

Akabaki ananiangalia hana majibu
Maana hajui aniandikie kwa kosa lipi..

Baasi baada ya muda akaona akshtuka akaniambia pole kwa usumbufu kazi njema!
 
Hapo kwenye mtu alikua analewa akaropoka mbele ya wakuu ndo sehem ulipoharibu uzi hivi mtu huwezi kutoa taarifa bila kuweka uongo?
Alie sababisha itokee huo ukaguzi ni vehicle inspector wa huko huko alikua mkoa x ambae aliuza lesen class C kwa madereva wa mabus karibu lesen 700 na kila lesen kala 500k
 
MI nadhani cha msingi madereva tukubaliane kwamba ukikamatwa bila cheti bei elekezi iwe ni shilingi ngapi? Kama jinsi tulivyojipangia kiwango cha 5,000 kwa kuzidisha mwendo na kikapita nchi nzima, nadhani na hili tukubaliane tu isiwe tabu.

Mi napendekeza 2,000 maana hili ni kosa lisilo na kichwa wala miguu.
 
Ya chenji kabisa
 
Nimeenda jana Trafik kuwapelekea Cheti kimvuli chake na Leseni maana nisije siku naingia na gari Tunduma naanza kuulizwa mambo ya Cheti wakati Leseni ipo Nchi kiboko wao Polisi wanatumia madaftari kutunza kumbukumbu zetu yaani wanapekua daftari kubwa kujua ulisoma Intake ya ngapi hicho Chuo kama ni Veta au NIT nashangaa wao hawataki kabisa kwenda na wakati kwenye Dunia ya Technology na hii yote kutengeneza mazingira ya upigaji sio kwamba hawajui...
 
Hahaaaaa wanapekua counter quire4

Vp mkuu ulifanikiwa kweli
 
Yaani nisome driving miaka zaidi ya 40 imeshapita najiendeshea kwa class D unaniuliza cheti Leo? Wawaulizeni vijana Sisi wazee tuachwe. Labda wanataka hizo class C
 
Hahaaaaa wanapekua counter quire4

Vp mkuu ulifanikiwa kweli
Nifanikiwe wapi mkuu nimewaacha bado wanapekua madaftari yao na mimi muda wowote nasafiri wapo wengine wanadonoa donoa kwenye Computer wakimaliza kupekua daah nikasema nikirudi SA ntaikuta aisee Mungu atusaidie tuu aisee jambo la Jumatano hadi jana hatuna majibu na mimi sio mtoa Rushwa kwenye haki yangu ngoma inogile hapo...wasipotoa ntatembea na Cheti Chao huko siendi mpaka wapige simu...
 
Kuna kitu sikielewi kuhusu huu ukaguzi

Kwani wakishathibitisha una certificate wanakupa nini ambayo traffic yeyote akiona leseni ajue uko verified

Au kila traffic lazima apekue madaftari?
Je kuna namna au online system ambayo watakuwa wanaangalia leseni zetu zilizohakikiwa kama wanavyofanya faini na bima?

Ambaye amehakikiwa atupe feedback
 
Wanakupa barua ambayo chini inakua na muhuri hakuna kitu cha maana mkuu ni kupotezeana muda tuu maana hata wasiokua na vyeti hao hao ndio waliwapa Leseni tena hao hao ndio watakaowapa vyeti...
 
Back
Top Bottom