Natafuta Shule nzuri ya Udereva Dar es Salaam

Jan 23, 2020
13
6
Hello!

Habari za usiku wakuu, poleni na hongereni kwa mapambano ya kila siku.

Leo nimekuja kwenye jukwaa hili niombe ushauri ambao unaweza ukanisaidia mimi na watakaokuja huko baadae.

Mimi ni kijana umri miaka 24 elimu yangu niyakawaida tu baada ya secondary chuo cha umeme (VTC) na kwabahati nzuri nilipata cheti cha level 2 (Vc²).

Sasa baada ya hapo nikafanya kazi na kampuni moja ya kufunga cctv camera kwa mwaka 1 na kisha kufanya kazi na kampuni moja ya sola hapa mjini dar es salaam kwa takribani miaka 2½.

Maslai kwenye hio kampuni yalikuwa mazuri tu lakini kuna wakati ukafika mambo yakabadilika kabisa nikawaza kwa muda unavyozidi kwenda huko mbele hakutakuwa kuzuri kabisa basi nikajidunduliza ili nisome driving kisha nipate cheti ili niweze kupata leseni.

To make story short napenda sana kazi ya udereva, toka zamani nakuwa. Kila nikiwa barabarani hizi gari zimeandikwa (IT) natamani siku moja nifanye kazi ya kusafirisha hizi gari na mimi.

Je, Chuo gani bora naweza pata nikasima na baada ya kusoma nikapata usaidizi wakupata connection nikafanya kazi na hizi (IT) its my dream yani kuna muda huko barabarani nikama naonaga hizo gari zenyewe tu kila wakati.

Ahsante sana wakuu!
 
Vyuo vyenye reputation hapa bongo ni NIT na VETA, hapo hata ukitaka kuwa dereva wa Mabasi ya Mikoani au Malori yanayoenda Nchi jirani haukosi ajira, ila ukitaka hizi driving schools za mitaani pia ziko nyingi sana ushindwe wewe tu
 
Lkn nasikia veta imetoa leseni kwenye hivi za mtaani ama hakuna ukweli?
 
Ada yao ikoje kaka?
Hiyo mlimani kuna ya mwenge, tegeta, na bagamoyo, mimi nafahamu kwa tegeta ada yao ni 270K gari ya manual na 300K gari ya auto kwa mwezi labda kama wamepandisha siku hizi, angalia ambayo ni rahisi kwako kulingana na unapokaa
 
Mkuu usije ukahitimu huko halafu ukachukua it usafiri. Kusanya kwanza uzoefu haswa wa safari ndefu mdogo mdogo.

Kwanza kwa driving school zetu za bongo gari 1 inatumika kufundishia wanafunzi 20 kuna uwezekano mkubwa ukatoka huko bado gari hujaijua vizuri, maana kujifunza kwa vitendo utakuwa unaendesha umbali mfupi unampisha mwenzio.
 
Hiyo mlimani kuna ya mwenge, tegeta, na bagamoyo, mimi nafahamu kwa tegeta ada yao ni 270K gari ya manual na 300K gari ya auto kwa mwezi labda kama wamepandisha siku hizi, angalia ambayo ni rahisi kwako kulingana na unapokaa
Na tabata pia ipo.
 
Back
Top Bottom