Uchaguzi 2020 Je, Uchaguzi utakuwa huru na wa haki hata kama vyombo vya habari vitaendelea na katazo la kutangaza habari kampeni za vyama mbadala?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
Vyombo vya habari kutangaza kwa usawa kampeni za vyama vya siasa ni moja ya vigezo vya uchaguzi ulio huru na wa haki.

Siyo sawa hata kidogo kwa CCM kuvikataza vyombo vya habari kutangaza kampeni za vyama vingine vya siasa.

Tume ya Uchaguzi inapaswa kuingilia kati suala hili.
 
Mkuu Joka Kuu, Uchanguzi Mkuu wa October, utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Hakikisho hili limetolewa na Amiri Jeshi Mkuu wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Tanzania tuna Tume huru ya uchaguzi na tuna vyombo huru vya habari, ikitokea vyombo vya habari kwa kuutumia uhuru wake, vikaona habari ni ya CCM tuu, then be it huo ndio uhuru wenyewe.

Unless kama una ushahidi wowote hata wa kimazingira tuu, kuthibitisha CCM imevikataza vyombo vya habari kutangaza kampeni za vyama vingine, lakini siamini kama hoja hii ina ukweli.

Tuna vyombo vya habari vya umma na vyombo binafsi. Vinavyotakiwa kutoa haki sawa kwa vyama vyote ni vyombo vya habari vya umma tuu, lakini kwa vyombo binafsi viko huru kufanya upendeleo watakavyo.

Kuelekea Octoba 2015: Je, Sasa ni Wakati wa Media Zetu Kufanya Endorsement ya Wagombea?.

Uchaguzi Mkuu ni Kipindi Cha Neema kwa Media!. Ni Kipindi cha Mavuno!. Jee Bahasha Hizi Ni Halali?!.

P
 
..vyombo vya habari kutangaza kwa usawa kampeni za vyama vya siasa ni moja ya vigezo vya uchaguzi ulio huru na wa haki...
Kikubwa vyama vya upinzani vihakikishe vinaweka ushahidi wote wa interaction yao na vyombo vya habari (barua za maombi, barua za kukataliwa, recorded audio clips za mawasiliano ya simu, recorded video clips zinazothibitisha kukataliwa, nk, nk.).

Bila kuwa na ushahidi wowote, upinzani utakosa mahali pa kusimamia legally & legitimately.

Cc
Zitto
John Mnyika
CHADEMA
ACT Wazalendo
 
'Freedom of press' kwenye awamu hii sio kipaumbele.

Huu mhimili wetu wa nne (4) umehujumiwa sana awamu hii, hii sio haki hata kidogo na kinyume na katiba.
 
..vyombo vya habari kutangaza kwa usawa kampeni za vyama vya siasa ni moja ya vigezo vya uchaguzi ulio huru na wa haki.

..siyo sawa hata kidogo kwa CCM kuvikataza vyombo vya habari kutangaza kampeni za vyama vingine vya siasa.

..Tume ya Uchaguzi inapaswa kuingilia kati suala hili.
Nini uthibitisho wako?
 
Mkuu Joka Kuu, Uchanguzi Mkuu wa October, utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Hakikisho hili limetolewa na Amiri Jeshi Mkuu wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Tanzania tuna Tume huru ya uchaguzi na tuna vyombo huru vya habari, ikitokea vyombo vya habari kwa kuutumia uhuru wake, vikaona habari ni ya CCM tuu, then be it huo ndio uhuru wenyewe...
Wewe P toka Wajumbe wamwkufyeka naona hata uwezo wa kufikiri Umepungua Hakuna Uchaguzi huru Tanzania Suala la kuzuia Vyombo vya Habari tu ni Ushaidi Tosha Watanzania sio Wajinga Kama TBC ambayo ni Ya Walipa Kodi Inabagua Vyama unatarajia Nini?
 
Mkuu Joka Kuu, Uchanguzi Mkuu wa October, utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Hakikisho hili limetolewa na Amiri Jeshi Mkuu wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Tanzania tuna Tume huru ya uchaguzi na tuna vyombo huru vya habari, ikitokea vyombo vya habari kwa kuutumia uhuru wake, vikaona habari ni ya CCM tuu, then be it huo ndio uhuru wenyewe..
Pascal wa sasa siyo yule mwandishi nguli aliyekuwa objective. Wa sasa ni lackey wa ccm, hivyo sitarajii kuona hoja yenye substance kutoka kwako kuhusiana na uchaguzi ulio huru na haki
 
Ingekuwa vyema kanuni za mchezo kuwekwa wazi na hadharani:

wale ambao ni washabiki wa mpira wanafahamu kuwa kila mchezo lazima 'kanuni za mchezo ziwe wazi kwa timu zote' ili kuwa na 'Fair Play'
 
Vyombo vya habari kutangaza kwa usawa kampeni za vyama vya siasa ni moja ya vigezo vya uchaguzi ulio huru na wa haki.

Siyo sawa hata kidogo kwa CCM kuvikataza vyombo vya habari kutangaza kampeni za vyama vingine vya siasa.

Tume ya Uchaguzi inapaswa kuingilia kati suala hili.
Hakuna uchaguzi kabisa..thats my prediction!

Plus,kuna damu za watu kadhaa zitamwagika,atleast mikoa yote tutakua na death toll....maana kuna wajinga wengi wenye madaraka na maamuzi yao yataleta haya,Ole Sabaya ni vivid example ya hili..

Thats my prediction!
 
Vyombo vya habari kutangaza kwa usawa kampeni za vyama vya siasa ni moja ya vigezo vya uchaguzi ulio huru na wa haki.

Siyo sawa hata kidogo kwa CCM kuvikataza vyombo vya habari kutangaza kampeni za vyama vingine vya siasa.

Tume ya Uchaguzi inapaswa kuingilia kati suala hili.
Nakuunga mkono. Dalili zingine ambazo zinafanya uchaguzi huu usiwe huru na haki ni pamoja na:

1: Wajumbe wa Tume ya uchaguzi, wasimamizi, na watendaji (ma-Ded, DAS, n.k.) wote ni makada wa CCM. Hawatakubali kuona chama chao na mwajiri wao akigaragazwa na wapinzani. Watafanya lolote lile kuepusha shari hiyo.

2: Mwajiri wao ambaye ndiye mgombea urais na m/kiti wa CCM alishawaagiza kufanya lolote lile na popote pale kuhakikisha CCM inashinda. .."ninakupa mshahara mzuri, gari zuri, na maisha mazuri halafu utangaze mpinzani kashinda"....Kauli hiyo bado ipo na haijakanushwa.

3: Baadhi ya vifungu vya kanuni ya maadili ya uchaguzi vilivyokubaliwa na wapinzani kwa shinikizo (on gun point) vinalenga kunajisi mchakato wa kutangaza mshindi. Vifungu hivyo vinatamka wazi kuwa hakuna lazima kwa mawakala wa vyama ndani ya vituo vya kupiga na kuhesabu kura kupewa nakala ya matokeo.

4: Polisi wanaendelea kunyanyasa wapinzani pindi wanapoenda kuchukua fomu wakisindikizwa na wapambe wao kwa kisingizio cha kufanya maadamano bila kibali.
 
Pascal wa sasa siyo yule mwandishi nguli aliyekuwa objective. Wa sasa ni lackey wa ccm, hivyo sitarajii kuona hoja yenye substance kutoka kwako kuhusiana na uchaguzi ulio huru na haki
Mhurumieni. Mwenzetu huyu anapalilia fursa ikiwa JPM atashinda. Kwao kuna msemo: "Ka-nkila ka mbuli kakihyagulilaga bulalo wako". Tafsiri isiyo rasmi ni kuwa: Ka-mkia ka mbuzi kanajisafishia malazi yake.
 
kikubwa vyama vya upinzani vihakikishe vinaweka ushahidi wote wa interaction yao na vyombo vya habari (barua za maombi, barua za kukataliwa, recorded audio clips za mawasiliano ya simu, recorded video clips zinazothibitisha kukataliwa, nk, nk.)...
Halafu huo ushahidi waupeleke wapi?
 
Hakuna uchaguzi huru na wa haki penye kuminya uhuru wa vyombo vya habari! Dhana ya uchaguzi huru na wa haki ni pana sana kuliko ccm wanavyofikiri! Huwezi kusema kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki wakati chama kimoja kimesha hodhi vyombo karibu vyote vya habari! Huwezi kusema uchaguzi utakuwa huru na wa haki wakati chama kimoja kimeshafanya kampeni miaka 5 kabla ya wakati huku vyama vingine vikiwa vimezuiwa!

Huwezi kusema kutakuwa na uchaguzi huru na haki wakati chama kimoja kinanunua wanachama wa vyama vingine! Huwezi kusema uchaguzi utakuwa huru na wa haki wakati wa wapinzani wakiongea watendaji wakuu wa majeshi wanajitokeza hadaharani kutoa matamko ya kuwatisha! Huwezi kusema uchaguzi utakuwa huru na wa haki wakati kuna chama kinatuma vikundi vya vijana kuchoma ofisi na kushambulia msafara wa mgombea wa chama kingine!

Huwesema kutakuwa uchaguzi huru na haki wakati vijana wasanii wanashawishiwa na hata kujenga mazingira ya Huwezi sema kutakuwa na uchaguzi huru na haki wakati hadi viongozi wa dini wanaogopa kuongelea haki au kutoa elimu ya uraia kwa wananchi! Huwezi sema kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki wakati kuna wagombea wa upinzani wanatekwa au kukamatwa kisa kwenda kuchukua form ya kugombea jimbo flani ambalo kuna chama kinataka mgombea wake apite bila kupingwa!

Huwezi sema kutakuwa na uchaguzi huru na haki wakati serikali haipo tayari kufanya dharura ya kurekebisha baadhi ya vifungu vya sheria ya uchaguzi visivyoendana na mfumo halisi wa siasa za vyama vingi ambamo uchaguzi huo unafanyika!

Infact Uchaguzi Huru na wa Haki ni zana pana sana, na utimilifu wake upo katika matendo na mazingira yaliyoandaliwa kwa shughuli nzima ya uchaguzi huo!
 
Back
Top Bottom