Kitu kimoja ambacho CCM, CHADEMA na karibu vyama vyote wanakubaliana vyema ni kutotaka uwepo wa mgombea binafsi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,783
13,723
Sias zina unafiki sana. Siku zote wanasiasa wanatanguliza maslahi yao, wasikudanganye vinginevyo. Suala la kuruhusu mgombea binafsi liliamuliwa na mahakama kuwa ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi. Bahati mbaya CCM wakalipindisha. CHADEMA nao katika kupigania kote tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi hawajawahi kugusia suala a mgombea binafsi.

Ukweli ni kuwa mgombea binafsi ni mwiba mkali sana kwa vyama vyote vya siasa. Mgombea binafsi itavipunguzia nguvu vyama hivi, matokeo yake wameona ni bora wakalie kimya ukiukwaji wa haki ya kikatiba. Mahakama inabidi ikazie utekelezwaji wa haki hii ya kiraia.
 
Aisee, umeleta uzi wa maana mno. Hiyo hukumu inapaswa kukaziwa lakini pia hapa ndo tuvipime vyama vyetu kama kweli vinahubiri demokrasia kwa kumaanisha.
 
Sias zina unafiki sana. Siku zote wanasiasa wanatanguliza maslahi yao, wasikudanganye vinginevyo. Suala la kuruhusu mgombea binafsi liliamuliwa na mahakama kuwa ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi. Bahati mbaya CCM wakalipindisha. CHADEMA nao katika kupigania kote tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi hawajawahi kugusia suala a mgombea binafsi.

Ukweli ni kuwa mgombea binafsi ni mwiba mkali sana kwa vyama vyote vya siasa. Mgombea binafsi itavipunguzia nguvu vyama hivi, matokeo yake wameona ni bora wakalie kimya ukiukwaji wa haki ya kikatiba. Mahakama inabidi ikazie utekelezwaji wa haki hii ya kiraia.
Aise Umepiga kwenye mshono 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Let say Simba la Masimba agombee, na Chawa wake wampigie kampeni. Siyo CCM siyo Chadema wategemee zaidi ya nusu ya Wafuasi wao Kumeguka maana % kubwa ya wapiga kura wa Nchi yetu hawajui chochote kuhusu nchi inavyoenda wao wanajua tu kushabikia kama Team za mpira na muziki.
 
Mapema sana zaidi ya nusu ya wapiga kura wanaweza kwenda kwa mgombea binafsi bila kutegemea nafasi yake 😂
 
Sias zina unafiki sana. Siku zote wanasiasa wanatanguliza maslahi yao, wasikudanganye vinginevyo. Suala la kuruhusu mgombea binafsi liliamuliwa na mahakama kuwa ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi. Bahati mbaya CCM wakalipindisha. CHADEMA nao katika kupigania kote tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi hawajawahi kugusia suala a mgombea binafsi.

Ukweli ni kuwa mgombea binafsi ni mwiba mkali sana kwa vyama vyote vya siasa. Mgombea binafsi itavipunguzia nguvu vyama hivi, matokeo yake wameona ni bora wakalie kimya ukiukwaji wa haki ya kikatiba. Mahakama inabidi ikazie utekelezwaji wa haki hii ya kiraia.
Asante sana kwa kuuibua hii issue, kiukweli kabisa issue ya mgombea binafsi, nchi haina katiba bali kuna ubatili!. Serikali yetu tukufu imetunga sheria batili ya uchaguzi inayokwenda kinyume cha katiba, Bunge letu goi goi likaipolitisha hiyo sheria batili, Mahakama Kuu ikaitengua, serikali ikakata rufaa ikashindwa, ukiuchukua huo ubatili na kuupenyeza kwenye katiba kiubatili hivyo kuinajisi katiba yetu!. Mahakama Kuu ikasimama kidete na katiba, ikatoa uamuzi mabadiliko hayo ya katiba ni batili, Mahakama ya Rufani ikakabariki!. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Haya ni madudu yalifanyika!, kitu cha ajabu kabisa, tumeyarudia madudu yale yale kwenye hili sheria mpya ya uchaguzi iliyopitishwa juzi!. Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

P.
 
Bahati mbaya vyama vyote vinafaidika na huu ubatili. Huji kuona vinaupigia kelele. Unafiki.
 
Sias zina unafiki sana. Siku zote wanasiasa wanatanguliza maslahi yao, wasikudanganye vinginevyo. Suala la kuruhusu mgombea binafsi liliamuliwa na mahakama kuwa ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi. Bahati mbaya CCM wakalipindisha. CHADEMA nao katika kupigania kote tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi hawajawahi kugusia suala a mgombea binafsi.

Ukweli ni kuwa mgombea binafsi ni mwiba mkali sana kwa vyama vyote vya siasa. Mgombea binafsi itavipunguzia nguvu vyama hivi, matokeo yake wameona ni bora wakalie kimya ukiukwaji wa haki ya kikatiba. Mahakama inabidi ikazie utekelezwaji wa haki hii ya kiraia.
Kitu kingine ambacho chadema na ccm wanakubaliana ni kuzuia kuanzishwa chama chochote kipya maana chadema na ccm wanaogopa legacy ya JPM kutokea upinzani mpya vinajua wazi hiyo legacy ikipata chama basi ndiyo mwisho wa chadema ....kwa sasa legacy ya jpm ni kama nguvu kuu zisizo na mmiliki maana hata ccm ya sasa imezikataa hizo nguvu maana wanajijua ni wahuni...ni lazima msajiri wa vyama aruhusu kusajiri vyama vipya
 
Asante sana kwa kuuibua hii issue, kiukweli kabisa issue ya mgombea binafsi, nchi haina katiba bali kuna ubatili!. Serikali yetu tukufu imetunga sheria batili ya uchaguzi inayokwenda kinyume cha katiba, Bunge letu goi goi likaipolitisha hiyo sheria batili, Mahakama Kuu ikaitengua, serikali ikakata rufaa ikashindwa, ukiuchukua huo ubatili na kuupenyeza kwenye katiba kiubatili hivyo kuinajisi katiba yetu!. Mahakama Kuu ikasimama kidete na katiba, ikatoa uamuzi mabadiliko hayo ya katiba ni batili, Mahakama ya Rufani ikakabariki!. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Haya ni madudu yalifanyika!, kitu cha ajabu kabisa, tumeyarudia madudu yale yale kwenye hili sheria mpya ya uchaguzi iliyopitishwa juzi!. Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

P.
Wewe si ndiyo huwa unadai siku zote kuwa sheria ndiyo haki ...vipi tena leo unasema sheria batili
 
Ndio maana naona bado Mtikila alikuwa mpinzani tofauti, hata wale walioungana naye kwenye kesi ya mgombea binafsi walifanya wapate umaarufu.

Mgombea binafsi alishapitishwa na hata wakati wa kukazia hukumu utetexi wa serikali ilikuwa swala la mgombea binafsi limeingizwa kwenye mchakato wa katiba lakini Hadi Sasa. Mchakato umekuwa ukipigwa danadana.
Hivi tujiulize mgombea binafsi ni haki ya mtu kuzaliwa kwanini watu wachache wahodhi haki hiyo.
Sababu ya CCM na Chadema kukataa kuunga mkono mgombea binafsi ni miundo ya vyama vyao kutaka kudhibiti wagombea wao pamoja na ruzuku kwa kifupi hivyo vyama vipo kimaslahi zaidi.
 
Duuuh
 
Hii nchi hata Miso Misondo wanaiweza, tuwape Ikulu kila siku tuish kujiuliza wamepigaje hapo🤣
Hii ndio kitu Wanasiasa wanaogopa sana.
 
Back
Top Bottom