Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

hivi hilo vazi la taifa ndilo vazi atakalotakiwa kuvaa kila mtanzania? ina maana kama ukuvaa inakuwaje? ama umuhimu wake vipi? miaka yote 50 ya uhuru lilikuwa halina umuhimu vipi tena ghafla hii ndiyo linatafutwa
 
Kwani Tanzania hususan Bara hamjapata tu vazi la taifa mpaka leo?

Kulikoni?
 
Sitashangaa wakiibuka na vigauni vya ngozi kama anavyovaa Mpoto kutuambia ndo vazi la taifa.
Kihistoria hatuna vazi la taifa. Kuna baadhi ya makabila yana mavazi ya desturi; mfano wazee wa kihaya wanavaa kanzu na kofia za pama, wamasai, wamang'ati n.k wanavaa rubega, watu wa pwani wanafunga msuli, wamama wanatanda kanga n.k.

Narudia tena, kinachofanyika sasa hivi ni usanii tu wa akina Kusaga kula kodi zetu. na Mungu atawalaani.
??????? Hivi maendeleo ya nchi yanaletwa na vazi la nchi au ulaji tuu huo.
 
Nimekuwa nikifuatilia mjadala unaoendela sasa wa kupata vazi la Taifa. Jambo hii limekuwa likipewa 'air time' ya kutosha kunako vyombo vya habari kwa kutmumia pesa za wavuja jasho tena kwa kuhusisha viongozi wa juu wa wizara husika.

Wakati juhudi hizo zikiendelea, naomba tujiulize na kujipa majibu kwa maswali machache haya:

1. Nini hasa lengo la kuwa na hili vazi la taifa?
2. Lina umuhimu wowote ktk utatuzi wa matatizo yanayotukabili watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii?
3. Je inawezekana hii ikawa ni janja ya kuwazuga watanzania waachane na mijadala muhimu inayoathiri maisha ya watz kama vile ya katibi, ufisadi na ombwe la uongozi?
4. Nini hasa faida ya kuwa na vazi la Taifa?

Kuna mengi ya kujiuliza, lakini tuanzie na haya machache?
 
watu wazima wanakalia mambo ya kitoto badala ya kujadili really issue zinazogusa maisha ya watu wengi nchi hii!
 
Ni bora tungeshughulika na maswala ya msingi yanayotukabiri kama taifa, mfano, mfumuko wa bei, elimu ya vijana wetu, kupambana na ufisadi na kuimarisha mshikamano wa taifa. Kuliko kudeal na irrelevant issues, kwani mtu akitaka kujua nationality yangu si ataniuliza, kwani lazima nivae mavazi. wasilaghai watu, washughulike na masuala ambayo seriously yanaathiri nchi.
 
eti kila kitu kimetushinda,kuanzia mpira wa kiume,mpira wa kike, basketi n.k bora tujikite kwenye vazi la taifa tuonekane tuko busy na vazi la taifa.
 
eti kila kitu kimetushinda,kuanzia mpira wa kiume,mpira wa kike, basketi n.k bora tujikite kwenye vazi la taifa tuonekane tuko busy na vazi la taifa.

"Tuonekane tuko busy" I love it.

Hiki ndicho wanachofanya. Bonge la smokescreen ili mradi waonekane wanafanya kitu.
 
Kuna tangazo la vazi la taifa ,
Maana nasikia design ya maua rangi za bendera ya taifa
Kwa hiyo wa TZ sasa tutakuwa na sare ?!
 
HIVI HUU MCHAKATO WA VAZI LA
TAIFA : kuna umuhimu gani kwenye hii
jamii ya sasa??hivi hili swala
linaumuhimu zaidi ya wale hawanga
wa mafuriko na mambomu ya mbagala
na gongola mboto??TUNATUMIA VYOMBO VYA HABARI MUDA MWINGI
KUSISITIZA KUHUSU VAZI LA TAIFA
WAKATI LIKIWEPO NA LISIPOKUWEPO
HAKUNA EFFECT,,HII BAJETI YA VAZI LA
TAIFA INGETUMIKA KWA MAMBO
MUHIMU YENYE MANUFAA KWA NCHI ZAIDI YA HILO VAZI LA RANGI 4 ZA
BENDELA YA TAIFA...!AMBALO VIJANA
HAWATA VAA,,KOZ TUNAIONANA
MIDOSHO KIBAO INABENDELA YA TZ NA
HAKUNA MTU ANA BANG NAYO...!Dear
Mr TOP HUSIKA...!PLZ UPIGAJI SASA BASI..!
 
hili swala la vazi la taifa ni kuonyesha jinsi gani viongozi wa hii nchi wanapenda kufanya vitu vidogovdogo,wanang'ang'ania swala la vazi la taifa huku mambo mengine yanakwenda mrama,
kwani ni nchi ngapi duniani zina vazi la taifa?na kuna faida gani za kuwa na vazi la taifa?kama si matumizi mabaya ya hela za umma haya
 
Linchi lisiliokuwa na dira , limekufa. Tanzania ina priorities nyingi za msingi laikini kama watoto wadogo vile. Wanakimbilia mambo yasiyo ya msingi. Wanatufuta ulaji tuuuuu. Wanatangaza maredio yote na matv kuhusu vazi la Taifa as if we have nothing else to do. Halafu wasivyokuwa na akili hata kidogo wameshasema kitambaa cha rangi ya bendera ya TZ kitu ambacho kila mtu anajua. Sasa watanatufuta dizaini huku wanasema ni vazi. Ushenzi mtupu. Nawashauri wamtafute disigner proffessional na sio kutupigia mikelele isiyoisha wakati tuna njaa.
 
Linchi lisiliokuwa na dira , limekufa. Tanzania ina priorities nyingi za msingi laikini kama watoto wadogo vile. Wanakimbilia mambo yasiyo ya msingi. Wanatufuta ulaji tuuuuu. Wanatangaza maredio yote na matv kuhusu vazi la Taifa as if we have nothing else to do. Halafu wasivyokuwa na akili hata kidogo wameshasema kitambaa cha rangi ya bendera ya TZ kitu ambacho kila mtu anajua. Sasa watanatufuta dizaini huku wanasema ni vazi. Ushenzi mtupu. Nawashauri wamtafute disigner proffessional na sio kutupigia mikelele isiyoisha wakati tuna njaa.

Mi mwenyewe nashangaa,afu watu wapo kimya,wakiiba ndo utawasikia.
 
posho wankula wao,eti watu washindane kudesign vazi lataifa...wao wamechukua hela kwa ajili gani?
 
wazo la vazi la taifa lilikua wazo zuri; lakini masharti yaliyowekwa; eti watakaobuni vazi hilo watumie rangi za bendera ya taifa au nembo na alama za taifa; yamefanya wazo lenyewe kufa hata kabla ya kujaribiwa. Unataka kuwavisha watu mavazi ya rangi ya bendera ya taifa; kwani tumekua wanafunzi wa chuo cha itikadi? Kwa nini waziri asiwaachie uhuru wabunifu wa mavazi wakatumia ubunifu wao; yeye akateua tu watakaochagua hilo vazi la taifa? Je, hilo vazi la bendera, itabidi tulazimishwe kulivaa? Maana sidhani kama ni wengi ambao wangependa kutembea wamevaa bendera ya taifa lao, hata kama ni wazalendo kiasi gani!
 
Back
Top Bottom