ndo maana nimesisitiza kamati izunguke na kutafiti..watakuja na kitu.
Haina haja ya kuwa sceptical,eti uhakika utaalamu wa Wahaya bado upo ama la.. Halafu sikusema litatofautiana kulingana na hadhi ya mtu,someni vyema.. Au kaulize kwa Mnigeria yeyote gharama ya nguo yao ya kitaifa,amu mhindi yeyote muulize Sari hata huko kwao India inauzwaje,kaulize utasikia.. Halafu watu wanadhani ni kama nguo ya kuvaliwa ukienda sokoni au shopping,ni nguo ya heshima sana. Huenda ukaivaa mara moja katika miezi hata sita. Zaidi ni kwamba wataboresha ujuzi watakaojifunza wa njia za asili za kupata vitambaa hivyo.. Na wewe unashauri njia ya ujumbe kupiga kura,sidhani kama ni lazima,labda kama watashindwa kuja na kitambaa ama mshono wa aina moja.
kukubalika kwa vazi la taifa na kwenyewe ni shughuli tofauti na kuchagua! nadhani kwa sasa tukubali uhalisia wa mchakato huu - maana ulikuwa wazi kwa kitambo
Unajua bwana naipenda sana nchi yangu manake imekaa kikomed komed hivi huwa inanipa burudani kwa vituko. Haiishi vituko. Yaani nchi ina akili kama za sekondari tena form tu. AAAA Tanzania, Mambo yanayohusisha tuvikao na tukamati we are very good, eti kamati ya vazi la taifa. Kama tunataka kujulikana kuna vitu vingi vya kututangaza tumeviharibu sasa tunaibuka na vituko. Mfano, MICHEZO, TANZANITE, ML.KILIMANJARO, MBUGA ZA WANYAMA, MADINI, NK. Acheni usanii. Huo ni ulaji mwingine.
ulianza toka mwaka juzi kama siokosei, kulikuwa na shindano la wazi la mitindo/mavazi - hakikupatikana kitu kipindi kile. Ndio wanaendelea nadhaniuwazi huo unaodai ulikuwepo toka kitambo siuoni ndugu..au umeendeshwa kama ule wa vitambulisho vya taifa..?
1. Swala zima la vazi la taifa kupangwa kwa kamati lina matatizo. Vazi la taifa litatoka kwa watu.
2. Serikali inaweza kuchangia kwa kuweka mazingira ambayo yanaweza kustawisha kuwepo kwa vazi la taifa. Kwa mfano, kwa kufufua sekta ya viwanda vya nguo nchini, na kuacha designers wenyewe washindane, vazi litakalopendwa na wengi kama lina muonekano wa kitaifa automatically litakuwa la taifa. Hatukuwa na kamati ya kupanga wanawake wavae khanga au vitenge, ni vitu vinavyotokea organic tu. Huwezi kupanga mipango miingi ya vazi la taifa wakati huna hata viwanda vidogo vidogo tu vya nguo, achilia mbali textile mills.
Me nilivyosikia Joseph Kusaga yupo kwenye kamati nikajua kuna ulaji 2
Vazi la Taifa ni kanzu na kofia kwa wanaume, wanaotaka kulibadili hili wana agenda za siri na kwa kina mama Khanga mbili nje ndani chochote.
Vazi la Taifa ni National Identity kama ilivyo kwa bendera, sarafu n.k. Ni jambo zuri linalo ainisha utaifa wetu, tafadhali msibeze tu angalia na kwa jicho la tatu.