Je, Tunahitaji Vazi la Taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Tunahitaji Vazi la Taifa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sr. Magdalena, Dec 29, 2011.

 1. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Je vipao mbele vyetu kama taifa viko wapi? kwa nchi kama Tanzania je ni muhimu kuwa na vazi la Taifa leo?

  1. Badala ya kuunda tume ya kusaidia wakulima wa Pamba ili pamba yao iwe katika kiwango bora tunaunda tume ya kutafuta vazi la Taifa?
  2. Wakati hadi sasa tunashindwa kuongeza thamani ya pamba yetu ili tuiuze kama mali ghafi nje leo tunaunda tume ya kutafuta vazi la taifa?
  3. Badala ya kufufua viwanda vyetu vya nguo vilivyokufa, leo tunaunda tume ya kutafuta vazi la Taifa?

  Hivi kama vazi hilo likipatikana ni kiwanda gani hapa nchini kitashona nguo hizo za vazi la Taifa, au tutaanza tena mchakato wa kutafuta mzabuni wa kutushonea vazi la Taifa, nchini China, India na Pakistani.

  Halafu njoo kwenye wajumbe wa hiyo tume, tunajifunza nini kutoka kwao juu ya vazi hili la taifa, mbona tume imejaa wanahabari ni vigezo vipi vilivyo tumika?

  Kweli kuna umuhimu wa kutafuta vazi la Taifa sasa?  Gazeti la Mwananchi.

  WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi ameitaka Kamati Maalum ya Kupendekeza Vazi la Taifa kutimiza wajibu wake ipasavyo ili kukamilisha mchakato huo kwa muda uliokusudiwa.

  Akizungumza ofisi kwake jana wakati akizindua kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga, Waziri Nchimbi alisema hakukurupuka katika uteuzi wake wa wana kamati kwani alipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali.

  "Napenda niwaaeleze wananchi kwamba sikukurupuka kuteua wajumbe wa kamati hii, nilipata ushauri toka kwa watu mbalimbali, wajumbe mnayo kazi kubwa kwani ni lazima tufike mwisho na tuwape Watanzania kile ambacho wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu,"alisema Nchimbi.

  Alisema,"Vazi hilo likishapatikana mtasaidia kulitangaza ili wananchi walijue na lianze kutambulika rasmi kama nembo mbalimbali za Taifa,"alisema.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Kusaga pamoja na kushukuru kwa kuteuliwa huko alisema kamati yake itafanya kazi hiyo kwa nguvu zote kuhakikisha vazi hilo linapatikana.

  Alisema hatua inayofuata sasa ni kuwashirikisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyopo na hatimaye kupendekeza vazi mahsusi linalotambulisha utaifa wa Watanzania.

  Mbali na Kusaga kamati hiyo inaundwa pia na Angela Ngowi (Katibu), Habibu Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Absaloom Kibanda, Makwaiya Kuhenga na Ndesambuka Merinyo ambao ni wajumbe.

  Serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilianzisha mchakato wa kupata vazi la Taifa mwaka 2004 na mwaka huu wazo hilo limerudishwa tena.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Vazi la taifa ni dili ya kina ?Nchimbi.
  Kwani miaka ya nyuma hatukuwa tunavaa?
   
 3. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NATIONAL DRESS or Folk costume (also: regional costume, national costume or traditional garments) expresses an identity through costume which usually to a geographic area or a period of time in history, but can also indicate social, marital and/or religious status. Such costumes often come in two forms: one for everyday occasions, the other for festivals and formal wear.

  Following the outbreak of romantic nationalism, the peasantry of Europe came to serve as models for all that appeared genuine and desirable. Their dress crystallised into so-called "typical" forms, and enthusiasts adopted it as part of their symbolism.

  In areas where contemporary Western fashions have become usual, traditional garments are often worn in connection with special events' celebrations, particularly those connected with cultural traditions, heritage, or pride.

  In modern times there are instances where traditional garments are required by law, as in Bhutan, where the traditional Tibetan -style clothing of gho and kera for men, kira and toego for women, must be worn by all citizens-even those not of Tibetan heritage; or in Saudi Arabia, where women are required to wear the abaya in public.


  Vazi la Taifa halitafutwi linakuja automatically, ni kama lugha, nyimbo na chakula.
   
 4. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 5. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hahaha!, hili litakuwa vazi la waandishi wa habari.
   
 6. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Vazi la taifa ndo nini?
  litatusaidi nini?
  mbona hatutafuti chakula cha taifa, hivi muziki wa taifa uliishia wapi? hivi wale washindi wa vazi la taifa akina Rose Vallentine waliishia wapi? hivi Marekani wana vazi la taifa ? mbona wanatambulika na ni matajiri na wameendelea sana tu? hivi kama tanzanite imeshindwa kututambulisha, kama Serengeti (mbuga sio bia) imeshindwa kututambulisha, nguo ndo zitaweza?

  Tunakuwa kama vichaa, halafu jamani vitu vingine huwa havitungwi huwa vinatokea narturally, jengeni viwanda na mzingatie kilimo acheni ujinga, mtakula hilo vazi

  excuse my language lakini hapa naona vioja tu
  asanteni kwa kunisikiliza
   
 7. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  "Napenda niwaaeleze wananchi kwamba sikukurupuka kuteua wajumbe wa kamati hii, nilipata ushauri toka kwa watu mbalimbali, wajumbe mnayo kazi kubwa kwani ni lazima tufike mwisho na tuwape Watanzania kile ambacho wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu,"alisema Nchimbi.  Tuwape watanzania kile ambacho wamekuwa wakikisubiri kwa muda mrefu... teh he he he.
   
 8. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bongo flava kwa sasa inajulikana kuliko Zanzibar, Serengeti, Mt Kilimanjaro na Manyara, ikumbukwe kuwa tunapoteza fedha nyingi sana katika ku promote Zanzibar, mt Kili, Serengeti na Manyara etc.

  Bora wizara ingefikilia ni kwa kiasi gani inaweza ku promote muziki wetu kuliko kuja na hii hoja chakavu ya vazi la taifa.
   
 9. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eeeh mkuu, kuna mtu mmoja kwenye hiyo tume kituo chake cha Radio wafanyakazi wake wa kike wanavaa nusu uchi na wakiume wanavalia suruali chini ya magoti, leo wanataka kutupiga mchanga wa macho na vazi la taifa, hapana mkuu.
   
 10. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  in short hatuhitaji vazi taifa nchi yetu ilishapoteza dira haina mwelekeo, inanuka
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Labda kwanza wangetueleza vazi la taifa litakuwa linatumika katika matukio gani, wapi
   
 12. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Mi ningejiuliza kwanza jee, tunaviwanda vya kutengenezea materials na kushona hilo vazi?
   
 13. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Kama kuna mtu mwenye hadidu rejea za kamati hiyo aziweke hapa tuzipitie?

  Nakumbuka miaka ya nyuma zoezi hili lilifanyika je huu ni muendelezo au tunaanza upya na ni kwa nini?
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kama hayo matukio hayana umuhimu, basi suala la kuwa tunavyo viwanda au la, litakuwa lishakufa wenyewe

  Vazi la taifa wanataka tulitumie wapi?
   
 15. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 850
  Trophy Points: 280
  hawa viongozi huwa wananishangaza sana, tuna matatizo mengi lakini wao wanaweka kipaumbele vazi la taifa! This nation leaders never cease to amaze me.
   
 16. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Tupambane na mfumuko wa bei na ufisadi kwanza!----

  tuwe taifa kwanza, ndo tutafute vazi lake!
   
 17. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Hiyo tume nayo imetengewa fungu kwa ajili ya kazi ya kusaka vazi la taifa?

  BASATA watuambie kwanza ile kamati ya 2004 iliishia wapi na vazi la taifa kwani nao walitumia fedha nyingi tu za walipa kodi
   
 18. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyo mwenyekiti kwanza angeandaa vazi la radio yake, watangazaji wake si ndo wanaongoza kata k na zile suruali za mabinti wanaita skin jeans na wa kike nao wanaongoza kwa kuweka maziwa nje. Kama kashindwa kua na mavazi ya hesima nyumbani kwake vip kuhusu taifa nazani Nchimbi anatafuta vazi la waandishi wa Habari tu na kujiandalia mazingira ya kupigiwa kampeni mwaka 2015.
   
 19. m

  matunge JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Watanzania bwana, hatujui kuwa mavazi ni sehemu ya utamaduni wa jamii fulani....
  Ni sawa na chakula...
  Lugha...
  Hivi vyote huzuka tu...hakuna mtu anayekaa na kupanga...
   
 20. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kibanda keshajitoa afadhali kajiepusha na aibu.
   
Loading...