Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

kuna threads nyingine kama mbili hivi zinaongelea suala hili hili, nashauri moderator angeziunganisha kupanua mjadala huu.
Nilichowaambia hapa ni upotevu wa muda na inawezekana ndio maana Absalom Kibanda alijitoa kwenye kamati hiyo, inawezekana ana mambo ya msingi ya kufanya badala ya kupoteza muda huu muhimu.
Na nawahakikishia, hawa jamaa wakiendelea kututawala watafikia point ya kubuni 'Chakula cha Taifa'
Ni vazi la Taifa au kitambaa cha Taifa? Upuuzi mtupu!
wameteua waandishi wa habari ili kupunguza manunguniko, si magazeti hayataandika! Ila kwa maoni yangu hilo vazi litakuja automatic, halafu sio kweli vazi la taifa lina kuwa na rangi ya bendera, km ni hivyo si watu wanavaa wakati Serengeti boys inapocheza kuna watu walikaa wakabuni? Picha za mwanzo za uhuru Nyerere na Kawawa walikuwa wanavaa vazi la kiasili hatujaambiwa kwanini waliacha. Tufanye mambo ya msingi kama kufufua riadhaa na michezo mingine kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia badala ya kungangania vazi. Watu hawavaa timu ikiwa inafungwa bao 6 wataona aibu, imarisha michezo watu watakuwa proud na taifa na kuwa tayari kuvaa utambulisho wao mahali popote
 
Hatuihitaji vazi la taifa kama viwanda vyetu vya nguo vyote vimekufa vazi litatengenezwa wapi China or ????????
 
Tatizo si vazi la taifa kutokuwepo. Vati la Taifa lipo ila hatujui ni lipi. Haiwezekani hadi sasa tumeshafikisha mika 50 ya uhuru tuwe hatuna vazi la Taifa. watangulizi wetu hawakuwa vipofu; angalieni nembo ya Taifa yule Bibi na Bwana wamevaa nini.
 
Watanzania bana nahisi kuna vikao vinakaa na posho zinalipwa kwa kuchakachua vazi la taifa.

Unadhani mkuu wakati ndo ukweli? Ile kamati ya akina Kusaga, akina Merinyo na yule mama, wanakaa kila siku, wamepewa mamia ya mamilioni na wizara, eti waratibu mchakato wa 'kutafuta' vazi la taifa. Hivi hebu watupe historia kuwa vazi la taifa la nchi fulani ambalo lilitafutwa na kamati na likafanya kazi...
 
Huu mchakato ulianza toka 2004 af sijui ukaishia wapi, aniways sidhani kama tunahitaji vazi la taifa, kama utamaduni wa taifa ulishndwa kuzalisha vazi la taifa automatically then hamna haja, mbona tuna vitu vingi tu vinavyotupa identity kama taifa? Hilo vazi la nini, kwanza litakuwaje? Nani atavaa? Huo ni upotevu wa resources tu.
 
unamaanisha tuanze na taifa kwanza..lakini hivi majuzi tulisherehekea miaka 50 ya Tanzania bara a.k.a tanganyika.

Hilo lilikuwa disco show tu. Hatuna nchi wala taifa tumejikuta tu tuko hapa tunaishi kwa MoU
 
Kuna kanga, vitenge, msuli, kaniki.
Uchaguzi ni wako!!

Colourful kikoi au msuli not bad ila kiwe adjustable au ikishindikana watoe crash course ya kutufundisha jinsi ya kuvifunga visije vikaanguka huku tunatembea mitaani.
 
Tatizo letu ndio hilo. Badala ya kutilia maanani masuala muhimu, kama kuichangia timu yetu ya wanadada ya taifa kifedha wanahangaika na vazi kana kwamba wananchi tuko uchi au tutagaiwa bure! Si hasha kama wengi waonavo hapa pana maslahi BINAFSI zaidi ya tunavoelezwa.
 
mitumba, nguo kuukuu zilizochanikachanika...hicho ndicho kitambulisho cha Mtanzania. nani anabisha?
 
Lengo, Nia & Dhumuni la yote haya na mengine mengi ya aina hiyo ni kuweka mianya na mazingira endelevu ya semina, washa, makongamano & semina elekezi ilimradi tu watu waweze kuchukua vyao mapema! Hv jamani, leo hii mnaijelia popote pale atakapoonekana atatambulika kwa mavazi yake, sasa swali langu ni je hao wanaijelia walikaa na kujadiriana & hatimaye kufikia mwafaka kuwa vazi lao liwe ni hilo linalowatambulisha hv sasa duniani kote au ni kitu tu ambacho kilikuja kutokana na tamaduni zao?
 
Huu mchakato ulianza toka 2004 af sijui ukaishia wapi, aniways sidhani kama tunahitaji vazi la taifa, kama utamaduni wa taifa ulishndwa kuzalisha vazi la taifa automatically then hamna haja, mbona tuna vitu vingi tu vinavyotupa identity kama taifa? Hilo vazi la nini, kwanza litakuwaje? Nani atavaa? Huo ni upotevu wa resources tu.

Hii ni janja ya CCM kutafuta pesa za uchaguzi 2015 kupitia Kusaga, Mie nikienda nje utambulisho wangu ni NENO...i'm coming from Tz & our first President was Nyerere, Kwiishaaaaaaaa waaache ubabaishaji wao, anyway Chuin Lai ndio naikumbuka kama vazi nililolipenda na mpaka kaburini bado ntalipenda kama nembo ya uanaharakati bila ufisadi
 
"Napenda niwaaeleze wananchi kwamba sikukurupuka kuteua wajumbe wa kamati hii, nilipata ushauri toka kwa watu mbalimbali, wajumbe mnayo kazi kubwa kwani ni lazima tufike mwisho na tuwape Watanzania kile ambacho wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu,"alisema Nchimbi.



Tuwape watanzania kile ambacho wamekuwa wakikisubiri kwa muda mrefu... teh he he he.

Tunachokisubiri watanzania kwa muda mrefu ni kuona mabadiliko ya kweli ya kiuchumi na maisha bora na wala sio mambo ya vazi la taifa, sisi litatusaidia nini katika kukuza au kuimarisha uchumi wetu?

Au ni faida gani tutapata ambayo itatuwezesha angalau kujenga heshima ya kutambuliwa na wengine endapo uchumi wetu bado utakua ni dhaifu? Nani atavaa vazi kama hilo ili ajitambulishe mbele za mataifa mengine wakati taifa lenyewe lina sifa ya ufisadi na umaskini uliobobea?

Acheni mambo yasiyo na tija kwa taifa tuleteeni mambo ya msingi na yenye manufaa kwa taifa.
 
Hahaha!, hili litakuwa vazi la waandishi wa habari.

Hao wajumbe wa hiyo kamati ni kichefuchefu tupu, ebu waulizeni waliosoma chuo cha sanaa bagamoyo jinsi huyo katibu Angela Ngowi anavyovaa na hayo majukumu aliyopewa ya utaifa. Merinyo nae ni biashara zaidi .
 
huyo mwenyekiti kwanza angeandaa vazi la radio yake, watangazaji wake si ndo wanaongoza kata k na zile suruali za mabinti wanaita skin jeans na wa kike nao wanaongoza kwa kuweka maziwa nje. Kama kashindwa kua na mavazi ya hesima nyumbani kwake vip kuhusu taifa nazani nchimbi anatafuta vazi la waandishi wa habari tu na kujiandalia mazingira ya kupigiwa kampeni mwaka 2015.

kusaga!! Nenda clauds fm waambie watangazaji wako waache kutuonyesha yale manguo yao machafu ya ndani(kata k....) kisha hivyo vimini kwa hao madada, ukishafanikiwa kwa jambo hilo njoo sasa utuletee hiyo issue ya vazi la taifa
 
WAKATI nchi ikikabiliwa na matatizo mengi makubwa na mazito, serikali kwa kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imezua kwa mara nyingine tena mjadala usiokuwa na tija yoyote kwa wananchi hususani walalahoi – mjadala wa kutafuta vazi la taifa!

Mjadala huu hauna tija yoyote kwa Watanzania, ukiondoa watu wachache ambao hawana mipango yoyote ya maana kwa jamii. Hawa ni watu ambao wana fursa za kila siku kwenda Ulaya na sehemu nyingine duniani ambapo wanachokitaka ni kujulikana wanatoka Tanzania!

Ni aibu kwamba wakati kama huu ambapo serikali ingekuwa inaendesha mijadala muhimu kama kuandikwa kwa katiba mpya, inakubali watu kupoteza muda na raslimali kwa ajili ya kujadili magauni na mashati ambayo Watanzania wanatakiwa wayavae wakiwa ndani au nje ya nchi hii.

Kwa kifupi, hivi tunatafuta vazi la taifa ili iweje? Na tukishalipata vazi la taifa na kuanza kulivaa litatuongezea chumvi kwenye mboga au sukari kwenye chai?

Hebu tukae chini na kufikiria kama walimwengu wenzetu. Tuchukue mfano wa nchi zilizoendelea duniani kama vile Marekani, Canada, Japan, Ujerumani, Italia, Afrika Kusini, na kadhalika.

Je, nchi gani miongoni mwa hizi zina vazi rasmi la taifa? Au, je, ni lini ziliwahi kukaa na kupoteza muda kujadili vazi la taifa?

Kwa nini Watanzania tusiutumie muda wetu wa masaa 24 ya siku moja kujadili ukosefu wa maji ya kunywa katika sehemu kubwa ya nchi hii? Kwa nini tusianzishe mijadala angalau ya kurudisha uhai wa Reli ya Kati ambayo inabidi iwahudumie mamilioni ya watu nchini?

Nani aliwahi kusema vazi la taifa huja kwa kujadiliwa kwenye vikao? Nani aliwahi kusema, kwa mfano, mtindo wa muziki hujadiliwa kwenye vipindi vya radio na televisheni?

Hivi mtindo kama "Ndombolo" wa Congo na "Kwaito" wa Afrika Kusini ilijadiliwa kwenye vijiwe vya Kinshasa na Cape Town?

Mitindo hiyo ya muziki ilikuja yenyewe. Haikujadiliwa vijiweni au redioni!

Vivyo hivyo, mitindo ya uvaaji wa watu wa Afrika Magharibi, kama vile Nigeria, Ivory Coast, Guinea, Mali, na kadhalika, ilikuja yenyewe. Hakuna vikao vilivyofanyika na kupendekeza aina hiyo ya uvaaji.

Kwa nini tunashindwa kuelewa ukweli huo mdogo ambao hata watoto wa shule za msingi wanaufahamu?

Kuna wakati wapenda muziki walikaa na kuamua eti mtindo wa dansi nchini uitwe "Achimenengule"! Kilichofuata ni kwamba uamuzi huo uliishia kwenye meza walizokuwa wamezikalia wakati wa majadiliano hayo.

Hapakuwa na "Achimenengule" wala nini hadi leo!
Mtindo wa mavazi au kitu chochote huwa havipangwi, hujitokeza vyenyewe kwa kukubalika kimyakimya kwa watu – si kwa kutangazwa!

Hivi hatuna kitu cha maana cha kujadili kwa manufaa ya watu wengi? Kwa nini Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni inakubali kujishusha kiasi hicho wakati majuzi tu ilishindwa kuisafirisha timu ya wanawake ya taifa ya soka kwenda Namibia wakati kila mwaka inapewa bajeti nono na bunge?

Iwapo tatizo ni Watanzania kutaka kujulikana nje ya nchi, basi dawa yake ni ndogo sana. Mtanzania anayetaka kujulikana akiwa nje ya nchi hii ni kuvaa nguo yoyote na akaiandika kwa maandishi makubwa sehemu yoyote, kwa mfano: "I am a Tanzanian" (kwa Kiingereza), "Je suis un Tanzanien" (Kifaransa) au "Yo soy on tanzano" (Kihispania).
Yote hayo yanamaanisha kwamba: "Mimi ni Mtanzania".
Hiyo inatosha kabisa kuwafanya watu wakufahamu kwamba unatoka katika nchi mojawapo za bara maskini la Afrika. Inatosha!

Huna haja ya kuchora picha ya twiga au mlima Kilimanjaro kwani twiga ni wengi sana duniani achilia mbali milima mirefu zaidi ya Kilimanjaro.

Hata hivyo, kwa kifupi kabisa: Watu waliopania kwamba Tanzania lazima iwe na vazi la taifa ambalo litawatambulisha wakiwa ndani na nje ya nchi hii, wasipoteze muda kulitafuta – watumie mavazi ya Kimasai!

Ni mavazi yenye kuvutia na ni ya kipekee ambayo Mtanzania akivaa nje ya nchi hii ni hakika watu watamshangaa na kumfurahia.

Kama vazi hili watu hawalitaki basi ni heri tujadili jinsi ya kuzipatia shule za sekondari za kata kompyuta, tujadili jinsi ya kusomesha na kuwalinda maalbino nchini, tujadili jinsi ya kupunguza bei za betri za radio ili mamilioni ya maskini nchini waweze kuzitumia kirahisi kwa radio na tochi zao.

Kujadili mashati na magauni ya kuvaa wakati tuko kwenye ndege tukielekea Ulaya au wakati tuko kwenye semina za kujadili posho ni kupoteza wakati na raslimali za taifa bure.
Hivi Watanzania hatuna cha maana cha kufanya kwa ajili yetu na wajukuu zetu?
 
Back
Top Bottom