Kama mtanzania ukienda sehemu yoyote duniani na ukamuona mtu kajifunika/kavaa kanga lazima utamfutata huyo mtu kwa sababu Kanga ni vazi la Kiswahili.Tanzania ndio home of Kiswahili culture na ukimuuliza huyo mvaaji kanga lazima atatoa maelezo ambayo yatagusa Tanzania. ama alikuja yeye, au mtu aliyetembelea Tanzania alimnunilia.
Hapa naweza kusema kabisa kuwa Tanzania tunayo bahati kubwa ya kuwa na kitu kama kanga kwa sababu kanga sio tu maua bali pia kwa kawaida kanga inakuwa na 'msemo au ujumbe' ambao lazima mtu awe anafahamu Kiswahili ili aweze kuelewa nini kimeandikwa. Tukienda kwenye vitenge, karibu Afrika nzima inatumia vitenge, huwezi kudai hata kwa chembe kwamba kitenge ni asili ya Tanzania tofauti na ilivyo kwenye kanga. Kanga hata kama imetengezewa China lazima itengenezwe kwa kizingatia utamaduni wa Kiswahili.
Na kwa upande wa wanaume kaunda suti (zenye kola) ziko Tanzania na pengine India. Wachina wao hawana cola. Ukimuona mtu mwafrika kavaa kaunda suti (nadhani wote tunajua kaunda suti mshono wa Rais Kikwete, Mnyika etc) lazima huyo mtu ana connection fulani na Tanzania. Sasa mimi nilidhani kama ni vazi la taifa ni vizuri tuzingatie 'identities' ambazo zipo tayari.
Sioni kwa nini watu wanataka ku-reinvent the wheel wakati solutions zipo? If ain't broke don't fix it!
Pili, nimeona kwenye tv matangazo kuhusu ubunifu wa vazi la taifa kwa maana ya rangi (nadhani hapa wanaongelea rangi za kitambaa). Na kwenye matangazo hayo wanasisitiza uwepo wa rangi za bendera ya Taifa au/pia nembo ya kitaifa! Kwa sheria zilizopo sasa hivi ni kosa (kisheria) kuvaa bendera ya taifa au nembo ya taifa kinyume na sheria inavyoeleza. Wanasheria na hasa Tundu Lissu anaweza kutusaidia kwenye hili maana hata bungeni yuko mbunge mmoja wa CCM aliambiwa avue 'scarf' aliyokuwa amefunga shingoni. Sina hakika kama wajumbe wa hii kamati ya vazi la taifa wanalifahamu hili na sikukumbuki kama Dr Nchimbi akipeleka muswada bungeni ili kuruhusu nembo/rangi za bendera ya taifa kuvaliwa.
Ziko nchi nyingi watu wanavaa nguo, kofia hata tai zenye rangi ya bendera ya nchi zao. Sheria zao zinaruhusu, sasa kama sisi tunataka kufanya hivyo ni vema turekebishe kwanza sheria. Niliwahi kuuliza huko nyuma inakuwaje alama za bendera ya nchi zimetumika kwenye ZULIA la ukumbi wa bunge? Kipindi cha Mwl. Nyerere bendera ilikuwa na heshma mno pengine kwa sababu serikali ilijitahidi kuwaeleza wananchi matumizi ya bendera/rangi/nembo za kitaifa.
Mwisho, kati wa wajumbe wa hii kamati ya vazi nani ni mwanasheria?