TFF: Hatuna vazi la taifa ambalo taifa stars lingevaa

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema Taifa Stars haikuvalia vazi linalowakilisha taifa wakati ikiwasili Morocco kwenye mashindano ya AFCON kutokana na Tanzania kutokuwa na vazi rasmi la Taifa.

Ndimbo ameongeza kuwa hata vazi la Kimaasai, ambalo wengi wamelitaja, si utambulisho rasmi wa taifa, kwani hata Kenya kuna kabila la Kimaasai.
1766219824471.png

Picha hii imetengenezwa kwa msaada wa akili unde (IA) wadau wakidai kuwa Stars walipaswa kuingia nchini Morocco.​
 
Kuna nchi wao walitinga na mitindo ya mavazi ya kiislam kabisa. Kwa tanzania mavazi ya kimasai yangebamba kwa kwa kuwa wangeonekana ni wa kipekee kuliko wale wa mitindo ya kiislam na kinaijeria. Tz ingetinga shuka za kimasai na sendeu zake plus mkanda kiunoni na sime feki ya kuzugia ingependeza sana
 
Wangevaa tu mavazi ya CCM kama vazi la chama tawala pia wangependeza
 
Kuvaa vazi flani hivi la kupendeza, sare kwa wote hakuna uhusiano wowote na vazi la kitaifa, wangeweza hata kuvaa suti wote , wametoa majibu mepesi sana
 
Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema Taifa Stars haikuvalia vazi linalowakilisha taifa wakati ikiwasili Morocco kwenye mashindano ya AFCON kutokana na Tanzania kutokuwa na vazi rasmi la Taifa.

Ndimbo ameongeza kuwa hata vazi la Kimaasai, ambalo wengi wamelitaja, si utambulisho rasmi wa taifa, kwani hata Kenya kuna kabila la Kimaasai.
View attachment 3518161
Picha hii imetengenezwa kwa msaada wa akili unde (IA) wadau wakidai kuwa Stars walipaswa kuingia nchini Morocco.​
Wangefanya hivi ama vile haitosaidia kitu,muhimu watafute vazi la taifa
 
Hivi vazi la taifa ndio kitu gani? Naomba kueleweshwa na mataifa mengine yote yana hii kitu?
 
Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema Taifa Stars haikuvalia vazi linalowakilisha taifa wakati ikiwasili Morocco kwenye mashindano ya AFCON kutokana na Tanzania kutokuwa na vazi rasmi la Taifa.

Ndimbo ameongeza kuwa hata vazi la Kimaasai, ambalo wengi wamelitaja, si utambulisho rasmi wa taifa, kwani hata Kenya kuna kabila la Kimaasai.
View attachment 3518161
Picha hii imetengenezwa kwa msaada wa akili unde (IA) wadau wakidai kuwa Stars walipaswa kuingia nchini Morocco.​
Wapigwe tu warudi nyumbani kuendelea kuimba mapambio
 
wameingia vyema sioni tatizo lolote kwani ni ubunifu mzuri tuachane na haya mavazi ya mabeberu
 
Kuna nchi wao walitinga na mitindo ya mavazi ya kiislam kabisa. Kwa tanzania mavazi ya kimasai yangebamba kwa kwa kuwa wangeonekana ni wa kipekee kuliko wale wa mitindo ya kiislam na kinaijeria. Tz ingetinga shuka za kimasai na sendeu zake plus mkanda kiunoni na sime feki ya kuzugia ingependeza sana
Vazi la kiislam likoje,walivaa hijab?
 
Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema Taifa Stars haikuvalia vazi linalowakilisha taifa wakati ikiwasili Morocco kwenye mashindano ya AFCON kutokana na Tanzania kutokuwa na vazi rasmi la Taifa.

Ndimbo ameongeza kuwa hata vazi la Kimaasai, ambalo wengi wamelitaja, si utambulisho rasmi wa taifa, kwani hata Kenya kuna kabila la Kimaasai.
View attachment 3518161
Picha hii imetengenezwa kwa msaada wa akili unde (IA) wadau wakidai kuwa Stars walipaswa kuingia nchini Morocco.​
Huu ufisadi hadi lini ?wengi amjui mkisikia watu wanaongelea vazi la taifa mnadhani ni kweli...nyuma yake ni ufisadi ...ni project za kifisadi ndiyo maana wimbo ni huo huo .....TUACHANE NA MAMBO YAMAVAZI YA TAIFA ...HUO NI WIMBO WA MAFISADI MNAO IMBISHWA BILA YA KUJUA KUWA NI MRADI WA MAFISADI .
 
Back
Top Bottom