Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Nimeguswa sana na ukweli kwamba Kama taifa tumeshindwa kuchagua vipaumbele ambavyo vya kufishugulikia ili kuiondoa jamii yetu kwenye umaskini na kuiletea maisha bora. Kimekua na "tabia ya kutwanga maji kwenye kinu" mwisho wake ni maji uliyoanza nayo.
 
Toka mwanzo niliposikia suala la vazi la taifa, nilijua tu ni usanii wa watu kula hela. Sasa hivi wakiwa bado mwanzoni wameshaonyesha failure nyingi, ikiwemo ya kuamua rangi za vazi. Yan kama hawajui, niwajulishe tu kuwa Watanzania tumeshawagundua, kuwa wanakula ela. Hakuna cha maana watakachofanya.
 
Hivi nasikia vazi vazi la taifa hiv lina umuhimu gani?kwasababu watanzania wengi sidhani kama litachochea uzalendo.uzalendo unatakiwa kuanza na watawala kwanza.au ndo mambo ya posho?
 
Hivi nasikia vazi vazi la taifa hiv lina umuhimu gani?kwasababu watanzania wengi sidhani kama litachochea uzalendo.uzalendo unatakiwa kuanza na watawala kwanza.au ndo mambo ya posho?
hili vazi la taifa lingepata sapoti kubwa sana kama uanzishwaji wake ungeweza kuchochea kupunguza matatizo tuliyo nayo mfano mfumuko wa bei na vitu kama hivyo
 
Toka mwanzo niliposikia suala la vazi la taifa, nilijua tu ni usanii wa watu kula hela. Sasa hivi wakiwa bado mwanzoni wameshaonyesha failure nyingi, ikiwemo ya kuamua rangi za vazi. Yan kama hawajui, niwajulishe tu kuwa Watanzania tumeshawagundua, kuwa wanakula ela. Hakuna cha maana watakachofanya.
Naunga mkono hoja yako asilimia mia. Nimangalia mjadala live ITV hivi karibuni wakijadili aina ya kitambaa ambacho kitatumika. Hapo ilibidi nibadilishe channel kwasababu unajadili kitambaa/rangi wakati hapa nchini hatuna viwanda vya nguo vya kutengeneza vazi hilo! Vitambaa tunaagiza nje na hivyo ili kushona vazi hilo, WTz itatubidi kutumia fedha zetu nadra za kigeni kununulia. Hii haiingii akilini kabisa. Una anzisha vazi la taifa kwa kutegemea vitambaa vya kuagiza nje ya nchi! Huko ambako tutaagiza kitambaa hicho wakiamua kutuhujumu au kutotengeneza itakuwaje?
 
Vazi la taifa litavaliwa naturally na watu baada ya CDM kuchukua dola 2015, subirini mtakapoona watu wakivaa magwanda wenyewe pasipo kulazimishwa. Tutavaa rangi zozote kama wachina na tuta-save pesa nyingi za nje kwani yatatengenezwa hapahapa nchini.
 
siyo lazima vazi la taifa liwe na rangi za bendera na pia mbona vazi la taifa lipo toka siku nyingi?naomba wadau muwakumbushe hawa vijana waliozaliwa baada ya uhuru na CCM kuwa vazi letu tunalijua ambalo ni kofia ya Tarabushi,kikoi na aina ya nguo kama kanzu na haina rangi za taifa wasitupotoshe haiwezekani kuacha asili na kubuni lingine mamboleo wazee wetu watatuelewaje?au ni kwa kuwa wamezeeka sasa hawawezi kujitokeza na kuchangia mada humu?
 
FOCUS - Follow One Course Until Successful.
Hii ni kanuni mhimu sana kwa mtu yeyote, serikali yetu haina FOCUS na matokeo yake ni miradi kama hii ambayo haimsaidii mwananchi kutoka hapa alipo kuishi maisha ya heshima na utu kwa kupata angalau milo mitatu.

Tusubiri ripoti ya matumizi ndipo tutajua kwa nini Tanzania bado ni masikini
 
Upuuzi mtupu!!! We vazi la Taifa linaloandaliwa miaka 8 liko je? Toka 2004, watu wanazungumzia vazi la Taifa!! Hilo vazi kwanza lina nini cha zaidi, kama ni uzalendo wao wameweza kwa kiasi gani huo uzalendo? Wezi wakubwa! Baada ya ufisadi wa kutosha wameamua kwenda makanisani, eti harambee. Wanatutega hapo 2015 wakidhani wao ndo wenye akili peke yao! Bustard, vazi la Taifa wavae wenyewe hao Nyumbu!!
 
Vazi taifa iwe suruwali za kata K na vi tight kwa akina mama..
 
Hivi sisi walalahoi tutagawiwa jozi ngapingapi? Maana nasikia lilee salio la rada ndo limetengwa kwa ajili hiyo.
 
Sitashangaa wakiibuka na vigauni vya ngozi kama anavyovaa Mpoto kutuambia ndo vazi la taifa.
Kihistoria hatuna vazi la taifa. Kuna baadhi ya makabila yana mavazi ya desturi; mfano wazee wa kihaya wanavaa kanzu na kofia za pama, wamasai, wamang'ati n.k wanavaa rubega, watu wa pwani wanafunga msuli, wamama wanatanda kanga n.k.

Narudia tena, kinachofanyika sasa hivi ni usanii tu wa akina Kusaga kula kodi zetu. na Mungu atawalaani.
 
Siyo Kusaga peke yake bali na akina Merinyo ambao wanatafuta jinsi ya kutoka baada ya kufulia ile mbaya.
 
Siyo Kusaga peke yake bali na akina Merinyo ambao wanatafuta jinsi ya kutoka baada ya kufulia ile mbaya.

Yaani hata aibu hawana. Maana hii kitu haihitaji hata kuwa darasa la tatu kujua kuwa huwezi kubuni vazi la taifa lika-matirialize...
 
Ukisikia magoli ya mbali ndo hayo, utasikia wabunge wote na wakuu wa mikoa na wilaya watashonewa na serikali. Wananchi watakataa lakini watalazimishwa tu, interview hadi uvae vazi la taifa, hospitali hadi vazi la taifa. Ukiwa na shida ofisi ya serikali husikilizwi hadi uwe na vazi la taifa. Hii ndo bongo bana. Mtasikia tu.
 
Toka mwanzo niliposikia suala la vazi la taifa, nilijua tu ni usanii wa watu kula hela. Sasa hivi wakiwa bado mwanzoni wameshaonyesha failure nyingi, ikiwemo ya kuamua rangi za vazi. Yan kama hawajui, niwajulishe tu kuwa Watanzania tumeshawagundua, kuwa wanakula ela. Hakuna cha maana watakachofanya.
Na wka kuonyesha ni wizi zaidi, awali tuliambiwa kuwa kamati iliyoteuliwa na Waziri ilikuwa ni ya kukamilisha mchakato. Lakini matangazo wanayoyatoa na kazi wanazozifanya zinaonyesha kuwa mchakato ndio unaanza mwanzo!
 
Ndugu zangu, mimi baada ya kusikiliza na kutazama matangazo ya hawa jamaa, nimegundua kuwa hawatafuti vazi la Taifa, bali kitambaa......na baada ya kuwasikiliza zaidi, nikafahamu pia kumbe wanazo na hata rangi za hicho kitambaa, ambazo ni rangi ya bendera............... Baada ya kugundua hvyo, nikajiuliza! Sasa kwa nini wanatafuta kitambaa ilihali mabendera yenye rangi wanayoitaka ipo kibao, kwanini wasiende kuchukua hayo na kutuondolea kelele!

Sikuishia hapo lakini nikagundua kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa matukio, kwahiyo hili suala la vazi sasa hivi limekuja ili kuwapoteza WaTz maboya wasiconcetrate kwenye issue muhimu zinazowaumiza kama umeme, mafuta na kupanda kwa gharama za maisha, badala yake wahangaike na huu upupu wa vazi. Sasa hv hakuna babu wa loliondo, no north mara, no maandamano ya cdm, no kafulila, no ajali ya meli, sasa dawa ni kuibua ujinga wa vazi.
 
Hivi kama kizazi cha "wazalendo" (waliopitia JKT, vyuo vya siasa n.k) kina mawazo ya kuunda unda mikakati ya kuitafuna nchi (mali ya uma), je! si wengine tusiojua hata hyo JKT tuifanyaje nchi???
 
Mimi ata umuhimu wa hiyo wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo siuoni...Vazi la taifa sio kitu cha kutafuta ni you either have it or you don't, period!!
 
Back
Top Bottom