Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Wewe unafikiri Nchimbi atakula wapi, wakati Wizara yake haina project za maana
 
Kwa nini Nchimbi asianzishe mjadala juu ya namna ya kuinua michezo nchini? Kwa nini asitafute kiini kwa nini Kenya wanatoa wanariasha lakini Tanzania bado iko nyuma? Kwa nini asitafute mbinu za kuinua michezo kama sehemu ya kutoa ajira kwa vijana?
 
hivi hilo vazi la taifa ni nini?je ni umeme wa uhakika?
nchi tunajua iko uchi je wameliona hilo?

mimi nashauri vazi la taifa ni chadema.
tuharakishe tuuondoe utupu(ccm)katika taifa letu.
 
​:shock:
jamani kuna huu mchakato wa vazi la taifa unaoendelea , nimejaribu kutafuta umuhimu wake kwa sasa sikuweza kuuona . wizara ita tumia helanyingi kwenye hi shuhuli lakini itamsaidiaje mtanzania wakawaida ? hivi na wenzetu kama Nigeria walifanya hivyo kupata vazi lao?

ok pamoja na maswali nilio nayo bado nimegundua hata wano endesha hishuhuli hawana utaifa kabisa na sithani hata kama ilo vazi litakua na utafa.

Tuangalie mfano mmoja. kwenye Matangazo ya Television wana sisitiza hilo vazi lazima liwe na rangi za bendera ta taifa lakini wao wenyewe kwenye tangazo lao halina rangi ya bendera ya taifa sijui kwanii , baada yakusikia na kuona hilo tangazo nikajipa moyo nikasema labda ni kwasababu ni tangazo lamunda tu na mwisho wake ni baada ya mchakato .

Kwenye hayo matangazo ya TV kuna Tovuti wana toa kwaajili ya kujiandikisha ama kujiunga kama wataka kushiriki ,nikaamua kuifuatilia ile Tovuti na hiki ndicho kinachonijulisha kua Vazi lataifa linatafutwa na watu wasio na utaifa.

Nimaranyingisana tumesikia mamlaka ya mawasiliaano ina himiza watanzania tutumie domin ya tanzania kwenye Tovuti ya kitanzania yaani Tovuti ziwe www.tovuti.co.tz ilikuonyesha utaifa zaidi kua tunajali vya kwetu. kilichonishangaza nikukuta Tovuti ya vazi lataifa ni www.vazilataifa.com yaani haijatokana na domain yenye uwakilishi wa Tanzania yaani www.vazilataifa.co.tz sasa hapo kuna utaifa kweli ? mi nafikiri mambo kama haya yangeanza kwa waandaji kua na utaifa kwanza kabla ya kuleta kwetu.

ok nilipo ona hilo nikafikikiri wamejisahau nikajipa moyo ninga access Tovuti yenyewe www.vazilataifa.comkusema kweli imenikatisha tamaa na kugundua huumchakato umeshakua sawasawa na ule mchakato wa kupata katiba mpya yaani tumeshaanza na mguu mbaya. iweje wana sisitiza kua vazi lataifa linatakiwa liwe na rangi ya bendera ya taifa lakini rangi zilizopo kwenye Tovuti yenyewe hazina uhusiana na bendera ya taifa na kwenye Title bar ya hiyo Tovuti inasomeka my business ina maana hi Tovuti ni kwaajili ya business yao ?ama walikua wana maanisha nini ? ina maana hawapo serious na wanachofanya ama nikupuuzia?

niulize wadau inachukua mudangani kutengeneza Tovuti? sikutegemea hata sikumoja kama kutengeneza Tovuti inaweza chukua mwezi mima ? siamini kama walishindwa kuitengeneza ndani ya wiki moja kama inashindikana basi msiitangaze ama mwiifunge kabisa ili hicho kinacho waonyesha kua hamjajipanga kisionekane .

lingine ni hili la matumizi ya luga kwenye hii Tovuti, Lugayetu kuu inayo waounganisha watanzania wote ni kiswahili lakini kwenye hii Tovuti kunamchanganyiko wa kiswahili na kiingereza.
pamoja na matangazo yoote wanayofanya iliwashindaje kuweka maelezo yote kwenye hi Tovuti hata kuweka ile kamati imewashinda ama kuwenka hivyo vigezo wana vyo tangaza kwenye TV imewashinda ?

mimi naishauri hii kamati ifanye mambo kwenye uhalisia na ijarubu kuelimisha watu hili Vazi la taifa lina maana gani na litatusaidiaje . Nina wasiwasi mkubwa kua tulio wengi hatujui maana ya hili vazi na litatusaidiaje nilishangaa kusikia watu wana bisha na nakusema hili vazi litakua uniform yaani watu hawatatakiwa kuvaa nguonyingine , wengine wakasema hilivazi litakua ndo vazikuu lasherehe na matukio makubwa ama kama watu wanasafiri kwenda nje ndo watalivaa.
pia nilisha wahi sikia watu wanajiuliza je hilivazi litakuaje je kutakuana na lakike na lakiume? je kutakua na hijabu yataifa ama wapenda hijabu watavaanini wakati wakitaka kuvaavazi lataifa na je wale wamasai wa arusha wata tupa vazilao nakujiunga na vazi lataifa na wale wazee wetu wa pwani wavaao misuli watawekachini misuli na kuvaa vazi la taifa?
hayo na mengineyo mengi nimaswali ambayo yapo vichwani mwa watu na hawana majibu ilikuhakikisha kua hilivazi linaletamaana kabla yakuli tengeneza nivyema watu wakajua maana na umuhimuwake na faida zake na litatumika wakati gani na kwamuda gani

kamati ijipange tena kwani inaonekana inataka kuanza na mguu mbaya na mwishowe tutakua tumetumihe helanyingi bila maana yeyote kwan hakutakua na wanao jua maana yake na umuhimu wake , kwani litaishia kuwemwa kabatini na lisiwe namaana yeyote kama ilivyo kusudiwa. kamati haijachelewa nivyema ikaaza sasa
 
Vazi la taifa huwa halichaguliwi na timu ya watu; huu ni ukosefu wa akili, tofauti na vazi la nchi - nitaeleza.
Ukichunguza kwa ukaribu utakuta kuwa nchi zenye vazi la taifa mara nyingi huwa ni zile ambazo zina utamaduni mmoja au tamaduni kadhaa ambazo generally zinafanana tabia na asilia zao, mfano ni Rwanda au Burundi. Nchi kama South Africa ambayo ina makabila kadhaa yenye tamaduni zenye nguvu haina vazi la taifa kwa sababu ni vigumu. Hili ndilo tatizo ambalo hapa kwetu pia tunalo; kuna makabila mengi sana na kila moja lina tamaduni na uvaaji wake. Mfano, je, ukipewa kazi ya kutengeneza vazi moja ambalo mwanamke wa kimasai na uvaaji wake wa waziwazi na bila kufunika kichwa, na mwanamke mwarabu wa Kariakoo anayejifunika mwili wote kasoro macho, ambalo wote hawa watalikubali utatengeneza vazi gani? Impossible.
Timu za watu huwa zinachaguliwa kutengeneza vazi la nchi hasa kwa ajili ya matukio ya kimataifa kama vile Olympics au michezo ya Jumuiya ya Madola. Hapa sasa ndipo ile dhana ya rangi za bendera ya nchi inapoweza kutumika.
Otherwise, huu mchakato wa Nchimbi na akina Kussaga ni wendawazimu tu, pamoja na "designers" wao. Hakuna mwenye vision pale.
 
Vazi la taifa huwa halichaguliwi na timu ya watu; huu ni ukosefu wa akili, tofauti na vazi la nchi - nitaeleza.
Ukichunguza kwa ukaribu utakuta kuwa nchi zenye vazi la taifa mara nyingi huwa ni zile ambazo zina utamaduni mmoja au tamaduni kadhaa ambazo generally zinafanana tabia na asilia zao, mfano ni Rwanda au Burundi. Nchi kama South Africa ambayo ina makabila kadhaa yenye tamaduni zenye nguvu haina vazi la taifa kwa sababu ni vigumu. Hili ndilo tatizo ambalo hapa kwetu pia tunalo; kuna makabila mengi sana na kila moja lina tamaduni na uvaaji wake. Mfano, je, ukipewa kazi ya kutengeneza vazi moja ambalo mwanamke wa kimasai na uvaaji wake wa waziwazi na bila kufunika kichwa, na mwanamke mwarabu wa Kariakoo anayejifunika mwili wote kasoro macho, ambalo wote hawa watalikubali utatengeneza vazi gani? Impossible.
Timu za watu huwa zinachaguliwa kutengeneza vazi la nchi hasa kwa ajili ya matukio ya kimataifa kama vile Olympics au michezo ya Jumuiya ya Madola. Hapa sasa ndipo ile dhana ya rangi za bendera ya nchi inapoweza kutumika.
Otherwise, huu mchakato wa Nchimbi na akina Kussaga ni wendawazimu tu, pamoja na "designers" wao. Hakuna mwenye vision pale.

hilo nalo neno , na chaajabu sijaona hata wana toa maelezo kua hilo vazi kazi yake ni nini haswa . na chakushangaza je nikwanini nilazima liwe na rangi ya bendera ya Taifa?
miningefikiri hata wasinge paswa kusumbuka saana , na fahamu kua hizinguo kitambaa vya batiki vingetosha kututambulisha kwani kilamtu ana weza kulivaa. yaani hiserikali sijui inini inacho weza
 
Miaka 50 Tanganyika bila vazi la Taifa. Mnasubiri nini kupata utambulisho wenu?
 
Kamati ya vazi la Taifa linatutangazia kuwa kama tunataka kushiriki ktk upatikanaji wa vazi la Taifa basi tunaweza kupata fomu za kujiunga kupitia website ya Vazi la Taifa,cha kushangaza website hiyo haina mahali popote pa kuweza kupakuwa fomu hizo na unakutana na neno hili ktk hiyo website


WEBSITE COMING SOON

sasa huu si ubabaishaji jamani?


My Business - Home
 
Vazi la taifa la nin wakati watu maisha yametubana huku mtaani?
 
Wnabuniana miradi ya kupiga hela tu,anyway,aliye nacho huongezewa!
 
Nchi ya watu wadogoooogo/ Nchi ya kitu kidoooogo/ Ukitaka vazi ewe mama nenda dukaaani/
 
Habari wana JF,kwa kipindi kirefu sasa tumeshuhudia mchakato usiokwisha wa vazi la taifa.Mchakato huu una malengo ya kulipatia taifa vazi ambalo litalitambulisha taifa.Hakuna ubaya kwenye hili. Pengine labda vitu vingine vinavyolitabulisha taifakama nembo ya taifa, bendera, mlima Kilimanjaro wenye barafu ukanda wa joto,ziwa Victoria, simba wanaopanda miti, ziwa Tanganyika lenye kina kirefu Afrika,vyura wanaozaa na mengi tunayoyajua havijaweza kulitambulisha kamailivyotakikana.Kutafuta vazisishangai, lakini kinachonishangaza ni hiki;
  • Linatafutwa na nani ( taifa maskini/tajiri)?
  • Lifanye kipi cha msingi na maendeleo?
  • Likatutambulishe kwa nani?
  • Na linatafutwa baada ya kuhakikisha mangapi ya msingi kama taifa tumeshayakamilisha?
  • Livaliwe na nani katika jamii maskini kama hii?
Je, hilililikuwa la kipaumbele kwa taifa kwa sasa? Kipindi ambacho umeme nikichefuchefu, maji hayatoki mabombani-si mijini wala vijijini! Mfumuko wa beiza nafaka nishati, bidhaa zingine na maisha kwa ujumla, kushuka kwa thamani yashilingi kila kukicha, ajira kwa vijana, kushuka kwa elimu kama yanavyooneshamatokeo, miundo mbinu mibovu, foleni sugu Dar es Salaam, kamchezo ka rushwaa.k.a takrima, ukame wa utawala bora, uvurugwaji wa haki za binadamu, malariana mengine chungu mbovu!Ikumbukwe pia, mchakatohuu kwa namna moja ama nyingine unakula pesa za walipa kodi maskini. Mfano,tumeshuhudia maafisa utamaduni wa wilaya na mikoa wakisafiri kikazi kutoka mkoammoja hadi mwingine kwa kazi hiyo hiyo.Apa kuna sura yauzalendo kweli? Au ni mradi wa mtu anataka kuupatia soko kwa kigezo cha vazi lataifa? Je, haya ndio mambo yakufanywa na nchi maskini ili itoke kwenye lindi laumaskini? Je, ndio yanayotegemewa na wamama waja wazito wasio na zahanati hukovijijini? au kundi la sekondari zisizo na waalimu maabara madarasa na matunduya vyoo? Wakulima wenye mazao yanayoozea shamba? Je, ni kazi ya kufanya aukusimamiwa au kuratibiwa au ata na ofisi nyeti kamawizara?Tuje upande wapili wa shilingi, viwanda vitakavyotengeneza vitambaa viko wapi? Au ndio vazila taifa kitambaa kitapatikana kwa pesa ya kigeni??? Wakuu, kwamtazamo wangu hii imekaa vibaya. Ilipaswa ifanywe na wenzetu wa dunia yakwanza, sio sisi tunahitaji kufanya ya umuhimu kwanza.
 
Ndo ukweli huo mkuu,watu wanapeana tenda wale wakati tuna matatizo kibao!ukifuatilia kwa undani unaweza kukuta yametengwa mabilioni eti kwaajili ya vazi la taifa.shame on them
 
Back
Top Bottom