Je, ni kweli Rostam Ameuza Share zake Vodacom?

Nyerere kaiacha hii nchi senti mbovu ya kigeni hakuna hazina na BOT imechomwa moto.

Ukibahatika kuipata hotuba ya Ali Hassan Mwinyi ya "mikuki miwili", mwanzo mwanzo tu wa madaraka yake aliwaita wazee Diamond Jubilee na kuwaelezea namna alivyokabidhiwa hii nchi, alifanya kusudi asije kuambiwa yeye ndiyo kafuja.

Ukiisikia hotuba hiyo ndio utajuwa hii nchi aliipokea vipi. Utalia.

Mitaani foleni moja kwa moja, za kuanzia mafuta ya gari mpaka chakula cha kila siku. Ukipata kilo moja kwa wiki ya sukari kwa familia yako shukuru Mungu wako.

Tuulize tuliokuwepo upate faida ya kujuwa nchi hii imetoka wapi. Leo tuna neema kubwa sana, tunaongelea matajiri na mabilioni. Thubutu wakati huo, hata hicho ki share kinachoongelewa cha Rostam nchi nzima hii ilikuwa haina hata robo ya thamani yake. Kalagabaho.

Ni kweli Nyerere alituacha arosto,yan Mwinyi wakati anachukuwa Nchi hata mishahara ilibidi akaombe na kukopa kwa Mugabe miezi yake miwili ya mwanzo.
 
- Hivi karibuni kulikuwa na habari za kibiashara kwamba Rostam Aziz ameuza share zake alizokuwa nazo VODACOM, sio siri kwamba amekuwa akimiliki share 35% ya kampuni hiyo kubwa sana hapa nchini, Rostam aliuza Share 17% kwa Shillingi za Tanzania Billioni 387.

- Swali la the dataz ni je ni kweli hizi alizouza zilikuwa ni share zake? Kama sio zake ni za nani? Na kwa nini zimeuzwa now kuelekea uchaguzi wa Rais 2015 na sio huko nyuma? Ninaamini majibu ya hili swali yana habari nzito sana na mustakabali wa Taifa letu was just thinking aloud!!

FMES - Wazee wa Sauti ya Umeme!!

Alichokifanya huyu bwana ni kuhakikisha serikali ya Tanzania will never touch his money. Amechukuwa the 'long road to safety'. In other words, anajua tiktak zote za serikali hivyo kajiweka sawa. Touch him if you can!
 
Mara useme Rostam ameuza share zake, mara uulize ni zake au si zake.

Jipange upya hueleweki.

Kama unataka kujuwa kama share ni za Rostam au si Rostam? unaweza kutembelea BRELA, unalipia 6,000 unafanya official search unapata kujuwa yote uyatakayo, au una lingine zaidi?

Pitia hapa kwa maelezo zaidi: BRELA
FaizaFoxy# wewe ni muislamu msomi. Unaenda kwa data. Waislamu wote wangeenda shule Kama wewe tungekuwa mbali na mambo ya uzushizushi Kama ya hawa wanaobunibuni ya kina rostam bila kuwa na uhakika
yangekoma.
 
Alichokifanya huyu bwana ni kuhakikisha serikali ya Tanzania will never touch his money. Amechukuwa the 'long road to safety'. In other words, anajua tiktak zote za serikali hivyo kajiweka sawa. Touch him if you can!

Hata kama hajauza shares, Serikali haiwezi tu kukamata fedha za mtu, labda wacheze na mtu asiyejua sheria za Kimataifa. Rostam ni kitu ingine, ni msomi, ni mfanya biashara, ni mwana siasa, ni tajiri, ni kichwa.

Kumbuka kuwa Tanzania ina dhamana za Kimataifa za wawekezaji kuwa hawatowataifisha. Hapo sasa.

Hata zingekuwa hazipo, tumeona jinsi Nyerere alivyohenyeshwa na Tiny Rowland alipojidai kumtaifisha, nakumbuka Nyerere alipoambiwa usifanye hivyo, akasema yeye hageuki nyuma, akigeuka nyuma atageuka jiwe! Looh! mbona alikiona kimbembe cha Tiny Rowland, alirudisha mwenyewe mali na ali compensate zote zisizoweza kurudishwa.

Watu wakawa wanasemea pembeni "mbona hajageuka jiwe?". Maana siku hizo hata kivuli chako unakiogopa kisije kuwa ni shushushu. Hata ukisingiziwa tu, unapotea.

Leo ni neema kubwa sana tuna uhuru wa maoni kiukweli.
 
Hata kama hajauza shares, Serikali haiwezi tu kukamata fedha za mtu, labda wacheze na mtu asiyejua sheria za Kimataifa. Rostam ni kitu ingine, ni msomi, ni mfanya biashara, ni mwana siasa, ni tajiri, ni kichwa.

Kumbuka kuwa Tanzania ina dhamana za Kimataifa za wawekezaji kuwa hawatowataifisha. Hapo sasa.

Hata zingekuwa hazipo, tumeona jinsi Nyerere alivyohenyeshwa na Tiny Rowland alipojidai kumtaifisha, nakumbuka Nyerere alipoambiwa usifanye hivyo, akasema yeye hageuki nyuma, akigeuka nyuma atageuka jiwe! Looh! mbona alikiona kimbembe ch Tiny Rowland, alirudisha mwenyewe mali na ali compensate zote zisizoweza kurudishwa.

Watu wakawa wanasemea pembeni "mbona hajageuka jiwe?". Maana siku hizo hata kivuli chako unakiogopa kisije kuwa ni shushushu. Hata ukisingiziwa tu, unapotea.

Leo ni neema kubwa sana tuna uhuru wa maoni kiukweli.
Kila wakati nasema Faizafoxy ni muislamu msomi. Anaenda kwa data. Hana mambo ya kuzushazusha Kama wanavyofanya wengine. I love FaizaFoxy.
 
Mbona Zain waliuza kampuni ya simu kwa Airtel. Kwani hizo mobile operators kwenye nchi 12 za Afrika zilikuwa za hasara. Kabla ya kujisifia mko kwenye fani ya biashara na mbwembwe kibao ni bora uhakikishe unachokisema kiko sahihi ama hapana.

- Kaka mpaka hapa hujaelwa kinachoongelwa naomba ukae pembeni waachie wanaoelewa kinachoongelewa tizama mda tena maana sio siri huelewi kitu hapa!!

Es
 
Alichokifanya huyu bwana ni kuhakikisha serikali ya Tanzania will never touch his money. Amechukuwa the 'long road to safety'. In other words, anajua tiktak zote za serikali hivyo kajiweka sawa. Touch him if you can!

- Kaka una uhakika hizo share ni za Rostam na kama ni kweli ameziuza kwa roho yake saafi? kabla ya kurukia msiayoyajua muwa mnauliza kwanza!!

ES
 
Wewe mfanyabiashara au mjasiriamali? mfanyabiashara ana wakati wa kuja JF na kuanzisha mada za kipuuzi?

Wafanya biashara wakubwa huwa wana mengi wanayaona ambayo wewe huyaoni, yanayowapelekea kuuza amma kununua amma kuanzisha biashara nyingine. Wana muono wa mbali katika biashara na ndiyo maana wanafanikiwa sana.

Usione biashara inakuwa kubwa ukadhani na faida inakuwa kubwa. Kumbuka biashara kama hii ya Vodacom ni kila siku inatakiwa ikuwe, unaweza kukuta mapato yote yanarudi tena katika kuwekeza ukuwaji wake.

Ulishaziona faida za Vodacom hata utake kutuaminisha kuwa ina faida kubwa?

Wewe utaona wapi na macho unayo lakini hayaoni? hukuona Celtel ikiuzwa? hukuona Tritel ikiuzwa? tena si shares ndogo ndogo ni zote kwa ujumla wake.

Hivi ukiandika huwa unafikiri wote humu ni misukule? Jipange upya.

- Hii topic sio siri ni nje ya uwezo wako wa kufikiri na kuona mambo, so ni bora ukanyamaza tu maana haya yote unayoyaanidka hayahusu kabisa, soma tena kaka mada hii ni nzito sana kuliko unavyoijibu na kurikua rukia ni mada kubwa sana nzito kuliko uwezo wako, niliyeileta ninajua sana nini maana yake na wanaohusika wakiiona ndio watashituka kuwa kumbe kuna wanaojua, wewe mkuu hujui na huhitaji kuambiwa maana!!

ES
 
- Kaka una uhakika hizo share ni za Rostam na kama ni kweli ameziuza kwa roho yake saafi? kabla ya kurukia msiayoyajua muwa mnauliza kwanza!!

ES

Wewe mwenyewe umeuliza kwenye post #1 , ungekuwa unajuwa ungeuliza? au umeshasahau mara hii, kweli ni mfupi kumbukumbu. Halafu unataka kushindana na FF? Pole sana.
 
Mbona Zain waliuza kampuni ya simu kwa Airtel. Kwani hizo mobile operators kwenye nchi 12 za Afrika zilikuwa za hasara. Kabla ya kujisifia mko kwenye fani ya biashara na mbwembwe kibao ni bora uhakikishe unachokisema kiko sahihi ama hapana.

Huyo anaejiita Field Marshall ES hana lolote pumba tu, mfatilie nyuzi zake humu, ni porojo zisizo na kichwa wala miguu.

Wewe Tazama post #1 hajui anachokitaka, ili mradi alete ----- wake, tena kawekewa na link kistaarabu humu kujulishwa kuwa hii habari imo humu tayari, yeye anajifanya haelewi anaendelea tu. Unajuwa kwanini? lugha ya kule ilimshinda akaona aje kufunguwa nyuzi hapa halafu ajifanye anajuwa sana.

Mwache aje ntaenda nae samba-samba.
 
kwa urasimu uliopo nchi hii hasa unapo fatilia interest za wakubwa,unadhani ni rahisi hivyo?wewe ulishawahi kufanya na ukafanikiwa?!

Kufanya nini na kufanikiwa? Kama unauliza bishara? mimi si mfanya biashara, mimi ni "semi retired" kwa hiyo ni "part time" mshauri wa biashara (Business Consultant).

Kazi yangu kwa zaidi ya miaka 10 sasa ni kukusanya kodi za majumba niliyorithi na kuyaendeleza na kulima kwetu Mkuranga.

Ndiyo maana unaniona muda mrefu nnaweza kuingia JF bila waswas.

AlhamduliLlah, nnashkuru nimefanikiwa kwa yote hayo.
 
Mbona Zain waliuza kampuni ya simu kwa Airtel. Kwani hizo mobile operators kwenye nchi 12 za Afrika zilikuwa za hasara. Kabla ya kujisifia mko kwenye fani ya biashara na mbwembwe kibao ni bora uhakikishe unachokisema kiko sahihi ama hapana.

Wakati inauzwa, Zain was struggling. Airtel mpaka sasa haifanyi vizuri hapa Africa. Airtel is really struggling to turn profitable. In fact, it is making losses overall. That said, you are right. Wafanyabiashara makini huuza shares wakati kampuni inafanya vizuri kwa kuwa bei ya share iko juu (Naturally, a company is more valuable when it is doing well than when it is making losses). Vilevile, wafanyabiashara makini hununua shares wakati kampuni haifanyi vizuri (when share price is as low as it can be. A big gamble though.).
 
Unasikitisha sana, unajuwa nimekubana kila pembe huna cha kutokea.

Kuna Mzee mmoja kule Dodoma alikuwa anajifanya ana-akili sana na akawa ana kiburi sana, akaja kudondoshwa tena kwenye uchaguzi wa awali tu na kijana mdogo sana pale Mtera, umeshawahi kumsikia?

Huyo Mzee ana mwanawe humu JF aka Le mutuz, baharia from Dodoma, nae hakuwa na akili wala muono wa kunizidi itakuwa wewe? pole sana.

- Kichwa cha mada nimeuliza swali je ni kweli hizi share 17 alizouza ni zake? Vipi unalo jibu la hilo swali? kama huna nyamaza tu mkuu unajaza hii topic fo nothing na sina mpango wa ligi na wewee maana on this ishu hujui lolote pole sana!!

ES
 
Huyo anaejiita Field Marshall ES hana lolote pumba tu, mfatilie nyuzi zake humu, ni porojo zisizo na kichwa wala miguu.

Wewe Tazama post #1 hajui anachokitaka, ili mradi alete ----- wake, tena kawekewa na link kistaarabu humu kujulishwa kuwa hii habari imo humu tayari, yeye anajifanya haelewi anaendelea tu. Unajuwa kwanini? lugha ya kule ilimshinda akaona aje kufunguwa nyuzi hapa halafu ajifanye anajuwa sana.

Mwache aje ntaenda nae samba-samba.

- Pumba ni zako swali langu ni je Rostam ameuza share zake kweli au za wengine? Jibu ninalo wewe huna pole sana!! zingekuw azake asingeziuza na hasira, tuliza boli tulipoanza hapa hukuwepo this is my world of dataz wewe hizi huna so tulia!!

Le Mutuz
 
Wanyonge ndio watabanwa kwenye kodi lakini baba mkubwa roatam atazidi kuwa juu hatujawahi Kuckia kati ya walipaji kodi bora kwann acwe tajiri
 
Nyerere kaiacha hii nchi senti mbovu ya kigeni hakuna hazina na BOT imechomwa moto.

Ukibahatika kuipata hotuba ya Ali Hassan Mwinyi ya "mikuki miwili", mwanzo mwanzo tu wa madaraka yake aliwaita wazee Diamond Jubilee na kuwaelezea namna alivyokabidhiwa hii nchi, alifanya kusudi asije kuambiwa yeye ndiyo kafuja.

Ukiisikia hotuba hiyo ndio utajuwa hii nchi aliipokea vipi. Utalia.

Mitaani foleni moja kwa moja, za kuanzia mafuta ya gari mpaka chakula cha kila siku. Ukipata kilo moja kwa wiki ya sukari kwa familia yako shukuru Mungu wako.

Tuulize tuliokuwepo upate faida ya kujuwa nchi hii imetoka wapi. Leo tuna neema kubwa sana, tunaongelea matajiri na mabilioni. Thubutu wakati huo, hata hicho ki share kinachoongelewa cha Rostam nchi nzima hii ilikuwa haina hata robo ya thamani yake. Kalagabaho.

Aliyechoma moto BOT ni jamaa yako mnaye-share kitanda. Amekuficha hii siri ajuza.
 
- Kaka kama haupo fani ya biashara sio rahisi kuamini mfanya biashara wa status ya Rostam anaweza kuuza share zake 17% kutoka kampuni yenye faida ya ajabu kama VODACOM kaka mimi mfanya biashara sijafikiam level ya Rostam lakini najua kwamba haiwezekani na haijawahi kutokea Duniani unless ni Russia ambako Serikali inakulazimisha kuziuza,

- Wailuze wanaojua biashara kaka haipo hakuna mafanya bisahara mwenye akili timamu anayeweza kuuza share zote hizo kutoka VODACOM hasa kwa wakati huu impossible!1

ES
Mkuu ES, kwanza karibu tena!, long time we missed you.
Hili la biashara kwa vile na wewe sio ndio maana pia huwezi kulifahamu!. Mfanyabiashara makini sio tuu anaangalia faida, bali pia anaangalia investments opportunities za kuwekeza kwenye faida zaidi na zaidi.

Yusuph Manji alikopa bilioni 30 toka penshions funds na kujenga ile Millenium Bussiness Park, kwa kutumia title deed ya eneo as collateral. Jengo lilipokamilika, linazalisha faida 100% profit, lakini kaamua kuliuza kwa hao hao penshen funds kwa shilingi bilioni 80!, katoa deni lao la bilioni 30 na kupocket faida yake ya bilioni 50 aka re ivest kwenye Quality Plaza!, nayo pia sasa kauza anaendelea kusonga mbele!.

Original Mmiliki wa Vodacom Tanzania ni Jaquline na Peter Noni kupitia Planetel, aliyekuwa akimiliki 35% ndipo akamuuzia Rostam kupitia Kampuni yake ya Caspian 19% Plenetel aka retain 16% huku ikiwa inatengeneza faida kubwa!. Rostam akaunda kampuni tanzu ya Mirambo iliyonunua shares zote za Caspian na shares zote za Planetel, hivyo kumiliki 35% yeye mwenyewe ingawa super deals wengine kama, Tanil Somaiya kupitia Shivacom, muzee wetu kupitia Alphatel, MO Dewji kupitia Zefona wanakamkono ndani yake.

Kwa mujibu wa TCRA, kampuni zote za mawasiliano lazima ziwe na not less than 35% local ownership, hivyo kama ni kweli kuna hii sale, ni kinyume cha sheria zetu!.

Hili la biashara kutengeneza faida na shares kuuzwa liko duniani kote naomba lisikushangaze, usikute mwenzako keshaona deal jingine kubwa, more profitable, kauza shares na kuja kuwekeza!. Sometimes unakuwa wala hujapanga kuuza, bali unafuatwa na offer you can't resist!, you just let it go!.

Bill Gates alianzisha Microsoft with 100% ownership na kampuni haijawahi kupata hasara, find out sasa anamili shares ngapi?!. Sio kila uuzwaji shares lengo lake ni kutengeneza faida, sometimes unauza shares ili kufanya divesture na hiki ndicho kitu Watanzania tunatakiwa tukipiganie, vikampuni vidogo vifanye divesification kuuza shares zake kwa wengine ili zipate mtaji mkubwa zipanuke!. Soko la Hisa la Dar es Salaam, limefungua dirisha dogo la Enterprise Growth Market, EGM ili small and medium enterprises SME's zifanye listing na kuuza shares zake!.
Pasco
 
Back
Top Bottom