Hata kama hajauza shares, Serikali haiwezi tu kukamata fedha za mtu, labda wacheze na mtu asiyejua sheria za Kimataifa. Rostam ni kitu ingine, ni msomi, ni mfanya biashara, ni mwana siasa, ni tajiri, ni kichwa.
Kumbuka kuwa Tanzania ina dhamana za Kimataifa za wawekezaji kuwa hawatowataifisha. Hapo sasa.
Hata zingekuwa hazipo, tumeona jinsi Nyerere alivyohenyeshwa na Tiny Rowland alipojidai kumtaifisha, nakumbuka Nyerere alipoambiwa usifanye hivyo, akasema yeye hageuki nyuma, akigeuka nyuma atageuka jiwe! Looh! mbona alikiona kimbembe cha Tiny Rowland, alirudisha mwenyewe mali na ali compensate zote zisizoweza kurudishwa.
Watu wakawa wanasemea pembeni "mbona hajageuka jiwe?". Maana siku hizo hata kivuli chako unakiogopa kisije kuwa ni shushushu. Hata ukisingiziwa tu, unapotea.
Leo ni neema kubwa sana tuna uhuru wa maoni kiukweli.