Je, ni kweli Idd Amini alikuwa shujaa wa Afrika, Nyerere alitumiwa na wazungu kumchafua?

Waambie Waganda vizazi vya leo ambao wananyanyaswa na viwanda na maduka ya wahindi, uone kama hautatolewa nduki.....
Nyerere alikosea sana kumchokonoa Amin.
Amini hajawahi kua mtu wa maana tusidanganyane hapa! hakuna tofauti yake na M7
 
Ukweli ni kwamba Idd Amini alikuwa na kukosi chake maalum walikuwa wakivaa nguo za vitenge. Uganda waliwaita ichitenge, walikuwa kama watu wasiojulikana, wakikufuata hurudi. Hata Kikwete alikuwa na watu hawa wakiongozwa na Ramadhani Igwondu aliyemteka na kumtoa kucha na meno Dr. Ulimboka.
Pia magufuli alikuwa na watu wa aina hii. magufuli ni Mtakatifu wa kina Kulwa Jilala na Sukuma gang wote.

Bunge lililopitisha mkataba wa DP World ni matokeo ya utawala mbovu wa kifashisti wa magufuli
Hueleweki
 
Hakuna uchonganishi wowote hapo, idi amini alilewa madaraka akafanya aliyofanya ikiwemo kuvamia ardhi ya Tanzania , kumbukumbu zipo hivyo sio vizuri kupindisha historia
 
Weekend Kareem wapenzi wa JamiiForums popote mlipo. Naamini mu wazima wa siha muruwa kabisa huku mkifanya tathmini ya kile mlichokifanya kwa juma zima hili.

Leo nimeleta kwenu swali juu ya Idd Amini, sipendi kumwita Nduli ila tumuombe tu Mwenyezi Mungu aendelee kuipumzisha roho yake.

Idd Amini aliitwa majina yote mabaya na nchi za magharibi baada ya utiriri wa matukio ya wadhalilisha Wazungu na kuwatimua Wahindi ili Waganda wenyewe waendeshe shughuli zote za kiuchumi na kukuza uchumi wao.

Miongoni mwa visanga alivyo vifanya Idd Amini ni pamoja na:-
  • Kuwaamuru mabalozi wa nchi za Ulaya wambebe juu juu na kiti kisha kumzungusha mitaani huku wananchi wakishangalia. Alifanya hivi kulipa kisasi jinsi babu zetu walivyowabeba wazungù.
  • Kuna wakati Amin aliomba msaada wa kifedha kwa Malkia Elizabeth, msaada ukachelewa, baada ya miezi kadhaa ndipo Amin akapewa hiyo pesa, kwa jeuri akamwambia sina shida na pesa yako, akairudisha. Malkia alikasirika sana.
  • Idd Amini aliwatimua Waasia wote, Wahindi na Waarabu ili kupisha Waganda wenyewe wafanye biashara.
Hivyo ni basi baada ya kuwatoa Wazungu dole la jicho, ndipo walipomuanza kumchonganisha Mwalimu na Amini ili Mwalimu ampige Amini na apotezwe kabisa.

KUKAWA na maneno kati ya Mwalimu na Amini ambayo hayakuwa mazuri, hatimaye yakapelekea vita ya mataifa mawili haya.

Habari za Idd Amini kula nyama za watu, je ilikuwa uzushi ama propaganda?

Je habari za Amin kuwapasua wanawake wajawazito, ilikuwa ni kweli au uzushi?

Je habari za Amini kuwatupa mto Nile walemavu zina ukweli gani? Je kuna uhusiano gani na ule wimbo wa Mchakamchaka Idd Amini akifa siwezi kulia, nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba?

Karibuni waungwana
Nduli, joka kuu, kumbe nawe sawa na yeye. Ungejua watz wa wakati huo alivyowasababishia usumbufu usingesema hivyo. Inabidi upimwe damu ya uraia wako.
 
Wazungu wameendelea kutuchezea hado leo hii braza, na ni mbaya zaidi. Tangu enzi za harakati na kabla ya hapo, tumechezewa sana, na hadi leo ni yaleyale. Na mataifa mengine yanafuata nyayo zile zile. Sasa hivi Mwarabu nae keshachomoa mikucha yake .... kama zamani. Sasa sie na werevu wote hatujaweza chomoa ... kama kina WAHUNI walipotezea kupatikana kwa RAIS bora awamu ile, na mwenye vinasaba vya huko, kwani uzalendo wake ulikua na shaka? Hapana! Je kuibuka kwa mapandikizi yenye vinasaba na mataifa mengine ni MBINU za kimkakati ? Tusubirie na wa Kihindi au kabla ya hapo yule wa KICHINA. Kiafrika bana???
 
unaweza kumlaumu idd Amin lakini pia usimlaumu. Alichokosea Amin ni kujaa kwenye mtego wa obote. Amin alimtoa madarakani obote , obote akakimbilia tanganyika , huku tanganyika kukawa na mipango ya namna ya kumlejesha obote madarakani , amini alipoliona Hilo akachukua shortcut ambayo ikawa ni fursa kwa obote kwa upande wake , na hasara kwa tanganyika.

Ile Vita ilitakiwa iishie kagera tu , hakukuwa na sababu kuingia Hadi Uganda. hasara tuliyoipata ni kubwa mno , wageni wengi waliikimbia nchi , uchumi ukayumba , yaani tabu tunazopitia miaka hii ya kiuchumi asilimia 90 ni matokeo ya ile Vita ya Uganda.
 
Alipambanishwa
Nope!
Hivi ukigombana na mke wako na baadaye ukasikia jirani yako amempa room mkeo katika nyumba yake, hivi utafanyaje?
Sifahamu kama unajua ugomvi wa Milton Obote na Nduli Idi Amin Dada?
Hivi Obote alipopinduliwa na Idi Amin mwaka 1971 alikimbilia nchi gani?
 
Nope!
Hivi ukigombana na mke wako na baadaye ukasikia jirani yako amempa room mkeo katika nyumba yake, hivi utafanyaje?
Sifahamu kama unajua ugomvi wa Milton Obote na Nduli Idi Amin Dada?
Hivi Obote alipopinduliwa na Idi Amin mwaka 1971 alikimbilia nchi gani?
Tz
 
Back
Top Bottom