Sakata la Ngorongoro ni kweli wazungu wana mapenzi ya dhati na Tanzania?

olimpio

JF-Expert Member
Apr 5, 2023
402
834
Nimewaza sana baada ya kuona bunge la umoja wa nchi za ulaya umepiga kura kwa wingi kabisa kulaani serikali ya Tanzania kuwaondoa kwa hiari wamaasai Ngorongoro .
Hamaki yangu kubwa ilisimamia hapa

1. Je, ni kweli wanatupenda sana hawa wazungu kuliko ndugu zao wanaoteseka huko Ukraine ?
Nchi kibao haziwa support ukraine lakini ziko tayari kuwa support wamaasai , huu ni upendo wa agape kwa wamaasai wa ukweli?

2. Wazungu wanapeleka silaha kali za kuangamiza ndugu zetu katika imani na wapigania uhuru wao huko Gaza
,watu wanakufa maelfu kwa maelfu , lakini hawaizuii Israel kuua watu , je wamaasai ni watu bora sana kuliko wanaokufa huko gaza?

Ngoro ngoro wamekufa wamaasai wangapi? Israel imeua wapalestina wangapi?
kwa nini Tanzania?

3. Wazungu waliua babu zetu na kuwatumikisha kwa dharau na mpaka leo hawajawahi kuomba radhi kwa ufedhuli waliotufanyia, leo hii mapenzi ya dhati ya kuwatetea wamaasai yako yametoka wapi?

4. Wazungu walitukataza tusijenge bwawa la mwalimu nyerere la kufua umeme ,wakisema tutafukuza vyura adimu duniani,yaani wanajali zaidi vyura kuliko maisha ya watanzania , leo wanapata wapi nguvu ya kuendelea kuwa remote ya maamuzi yetu?

Hawa wameua babu zetu ,wamemuua Mkwawa , wameua viongozi wetu wa kale wengi sana , na bado wamekua remote za maamuzi yetu , ni lini Tanzania itakua nchi huru? ni lini tutafanya mambo yetu bila hawa wanaojiita wapigania haki kutuingilia?

wanafiki wakubwa , wameruhusu ushoga kwenye nchi zao , wanatupa misaada ya masharti mabaya na magumu , wanatupeleka kuzimu hawa.

ngorongoro.jpeg
 
Maamuzi ya kuwaondoa wamasai katika makazi yao ya asili yalikua ya kishetani.

Hivi angekuja mtu na kuwahamisha watu waliokaa pale kizimkazi kwa miaka 30 wenye madaraka sasa wangeafiki??

Unyanyasaji tu na matumizi mabaya ya madaraka.

Ila ushetani huo umewekwa wazi na dunia imejua kuwa wamasai wamenyanyaswa nchini mwao.

Aibu kwa wahusika.
 
Sometimes wazungu wako kama wehu fulani, "we conserve" tunapunguza shughuli za kibinadamu ambazo ni tishio mbugani, wao wanaona si sawa, na binadamu waendelee tu kujazana mbugani"
Dr. Tulia aende akawaelimishe wajinga hawa.
 
Sometimes wazungu wako kama wehu fulani, "we conserve" tunapunguza shughuli za kibinadamu ambazo ni tishio mbugani, wao wanaona si sawa, na binadamu waendelee tu kujazana mbugani"
Dr. Tulia aende akawaelimishe wajinga hawa.
Mbuga gani wamasai walikua wanaishi, Loliondo imekua mbuga tangu lini kama kitu hukijui piga kimya
 
Ukishakuwa ombaomba lazima unyanyaswe na hauwezi kuwa huru kwenye maamuzi yako, kila ambapo mabwana zako watakapoona hauendi nao sawa lazima watafute mahala pakukufix.
 
Ukitaka kuwa huru, anza kujitegemea kwanza, tunajifanya viburi huku kutwa kucha tunaombaomba na jamaa wanajua hata hiyo misaada yenyewe inaingia kwenye matumbo na mifuko binafsi.
 
Back
Top Bottom