Je, ni kweli Idd Amini alikuwa shujaa wa Afrika, Nyerere alitumiwa na wazungu kumchafua?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,907
Weekend Kareem wapenzi wa JamiiForums popote mlipo. Naamini mu wazima wa siha muruwa kabisa huku mkifanya tathmini ya kile mlichokifanya kwa juma zima hili.

Leo nimeleta kwenu swali juu ya Idd Amini, sipendi kumwita Nduli ila tumuombe tu Mwenyezi Mungu aendelee kuipumzisha roho yake.

Idd Amini aliitwa majina yote mabaya na nchi za magharibi baada ya utiriri wa matukio ya wadhalilisha Wazungu na kuwatimua Wahindi ili Waganda wenyewe waendeshe shughuli zote za kiuchumi na kukuza uchumi wao.

Miongoni mwa visanga alivyo vifanya Idd Amini ni pamoja na:-
  • Kuwaamuru mabalozi wa nchi za Ulaya wambebe juu juu na kiti kisha kumzungusha mitaani huku wananchi wakishangalia. Alifanya hivi kulipa kisasi jinsi babu zetu walivyowabeba wazungù.
  • Kuna wakati Amin aliomba msaada wa kifedha kwa Malkia Elizabeth, msaada ukachelewa, baada ya miezi kadhaa ndipo Amin akapewa hiyo pesa, kwa jeuri akamwambia sina shida na pesa yako, akairudisha. Malkia alikasirika sana.
  • Idd Amini aliwatimua Waasia wote, Wahindi na Waarabu ili kupisha Waganda wenyewe wafanye biashara.
Hivyo ni basi baada ya kuwatoa Wazungu dole la jicho, ndipo walipomuanza kumchonganisha Mwalimu na Amini ili Mwalimu ampige Amini na apotezwe kabisa.

KUKAWA na maneno kati ya Mwalimu na Amini ambayo hayakuwa mazuri, hatimaye yakapelekea vita ya mataifa mawili haya.

Habari za Idd Amini kula nyama za watu, je ilikuwa uzushi ama propaganda?

Je habari za Amin kuwapasua wanawake wajawazito, ilikuwa ni kweli au uzushi?

Je habari za Amini kuwatupa mto Nile walemavu zina ukweli gani? Je kuna uhusiano gani na ule wimbo wa Mchakamchaka Idd Amini akifa siwezi kulia, nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba?

Karibuni waungwana
 
Obviously Nyerere alitumika Vibaya. Sijui Kwa kujua au Bahati Mbaya, ila baada ya hapoo ndipo Tanzania ilipoparaganyika
 
Nyerere alitumiwa na Wazungu kumchafua Iddi?

Mengine yote ungeweza kudanganya kwa nia ya kumpamba. Ila hilo la mgongano wake na Mwalimu ungeacha.

Iddi Amini alikuwa na maneno ya hovyo na vitisho. Mwalimu alijitahidi sana kutomzingatia. Mpaka pale Iddi alipojitoa ufahamu kutaka kung'ang'ania eneo la nchi yetu kuwa eneo la Uganda.

Uvumilivu huo usingeuvumilia hata wewe.

Kama ni Wazungu walimtuma Mwalimu kumchafua Iddi, basi hata wakati wa Vita wangempa msaada wa kivita ili kumchakaza Iddi Amini. Badala yake, Iddi Amini ndiyo alipata msaada kutoka nchi wahisani wa Kiislamu (Libya).
 
Ukweli ni kwamba Idd Amini alikuwa na kukosi chake maalum walikuwa wakivaa nguo za vitenge. Uganda waliwaita ichitenge, walikuwa kama watu wasiojulikana, wakikufuata hurudi. Hata Kikwete alikuwa na watu hawa wakiongozwa na Ramadhani Igwondu aliyemteka na kumtoa kucha na meno Dr. Ulimboka.
Pia magufuli alikuwa na watu wa aina hii. magufuli ni Mtakatifu wa kina Kulwa Jilala na Sukuma gang wote.

Bunge lililopitisha mkataba wa DP World ni matokeo ya utawala mbovu wa kifashisti wa magufuli
 
Mimi binafsi kwa kusoma story mbalimbali za viongozi mbalimbali wa Afrika baada ya uhuru ni kuwa karibu wote walikuwa makatili sema Idd Amin, Bokasa, Mobutu na Kamuzu Banda walivuka mipaka. Hata hapa Bongo waasia wengi pamoja na matajiri wazawa walitaifishiwa vitu vyao kibabe wakati wa azimio la Arusha. Ilikuwa sio poa. Walioenda mahakamani wakashinda kesi wamekuja kulipwa mamilioni ya fidia. Mzee Tango wa Arusha hadi mwaka 2009 alikuwa bado anadai bilioni 6.
 
Ukweli ni kwamba Idd Amini alikuwa na kukosi chake maalum walikuwa wakivaa nguo za vitenge. Uganda waliwaita ichitenge, walikuwa kama watu wasiojulikana, wakikufuata hurudi. Hata Kikwete alikuwa na watu hawa wakiongozwa na Ramadhani Igwondu aliyemteka na kumtoa kucha na meno Dr. Ulimboka.
Pia magufuli alikuwa na watu wa aina hii. magufuli ni Mtakatifu wa kina Kulwa Jilala na Sukuma gang wote.

Bunge lililopitisha mkataba wa DP World ni matokeo ya utawala mbovu wa kifashisti wa magufuli
Serikali gani duniani haina kutekana
Serikali nyingi zina mfumo huo

Ova
 
Ngoja nimalizie grants nitarudi
Wanywa SUNGURA mnajua kuiita majina mazuri, eti grants
Obviously Nyerere alitumika Vibaya. Sijui Kwa kujua au Bahati Mbaya, ila baada ya hapoo ndipo Tanzania ilipoparaganyika
Ilikuwa ni adhabu ya kujidai kuzisaidia nchi za kusini mwa Sahara zijikoboe. Ua uchumi wa Tanzania tuone huo ukombozi utaufanya vipi
 
Mimi binafsi kwa kusoma story mbalimbali za viongozi mbalimbali wa Afrika baada ya uhuru ni kuwa karibu wote walikuwa makatili sema ni kuwa Idd Amin, Bokasa, Mobutu na Kamuzu Banda walivuka mipaka. Hata hapa Bongo waasia wengi pamoja na matajiri wazawa walitaifishiwa vitu vyao kibabe wakati wa azimio la Arusha. Ilikuwa sio. Walioenda mahakamani wakashinda kesi wamekuja kulipwa mamilioni ya fidia. Mzee Tango wa Arusha hadi mwaka 2009 alikuwa bado anadai bilioni 6.
Nyerere hakuwa muona mbali. Mara nyingi alifanya mambo kwa mkurupuko.
Ie vijijini vya ujamaa, Azimio la Arusha etc vilifeli vibaya sana
 
Afrika bara zito sana, namtafakari aliyeshika mwavuli, aisee😆😅🤣😂
IMG-20220919-WA0052.jpg
 
Weekend Kareem wapenzi wa JamiiForums popote mlipo. Naamini mu wazima wa siha muruwa kabisa huku mkifanya tathmini ya kile mlichokifanya kwa juma zima hili.

Leo nimeleta kwenu swali juu ya Idd Amini, sipendi kumwita Nduli ila tumuombe tu Mwenyezi Mungu aendelee kuipumzisha roho yake.

Idd Amini aliitwa majina yote mabaya na nchi za magharibi baada ya utiriri wa matukio ya wadhalilisha Wazungu na kuwatimua Wahindi ili Waganda wenyewe waendeshe shughuli zote za kiuchumi na kukuza uchumi wao.

Miongoni mwa visanga alivyo vifanya Idd Amini ni pamoja na:-
  • Kuwaamuru mabalozi wa nchi za Ulaya wambebe juu juu na kiti kisha kumzungusha mitaani huku wananchi wakishangalia. Alifanya hivi kulipa kisasi jinsi babu zetu walivyowabeba wazungù.
  • Kuna wakati Amin aliomba msaada wa kifedha kwa Malkia Elizabeth, msaada ukachelewa, baada ya miezi kadhaa ndipo Amin akapewa hiyo pesa, kwa jeuri akamwambia sina shida na pesa yako, akairudisha. Malkia alikasirika sana.
  • Idd Amini aliwatimua Waasia wote, Wahindi na Waarabu ili kupisha Waganda wenyewe wafanye biashara.
Hivyo ni basi baada ya kuwatoa Wazungu dole la jicho, ndipo walipomuanza kumchonganisha Mwalimu na Amini ili Mwalimu ampige Amini na apotezwe kabisa.

KUKAWA na maneno kati ya Mwalimu na Amini ambayo hayakuwa mazuri, hatimaye yakapelekea vita ya mataifa mawili haya.

Habari za Idd Amini kula nyama za watu, je ilikuwa uzushi ama propaganda?

Je habari za Amin kuwapasua wanawake wajawazito, ilikuwa ni kweli au uzushi?

Je habari za Amini kuwatupa mto Nile walemavu zina ukweli gani? Je kuna uhusiano gani na ule wimbo wa Mchakamchaka Idd Amini akifa siwezi kulia, nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba?

Karibuni waungwana
Amini hafai hata siku moja kufukuza Waasia Uganda siyo kigezo cha kumtukuza Nduli Amini.
 
Duh
 
Back
Top Bottom