Je, ni kweli Idd Amini alikuwa shujaa wa Afrika, Nyerere alitumiwa na wazungu kumchafua?

Weekend Kareem wapenzi wa JamiiForums popote mlipo. Naamini mu wazima wa siha muruwa kabisa huku mkifanya tathmini ya kile mlichokifanya kwa juma zima hili.

Leo nimeleta kwenu swali juu ya Idd Amini, sipendi kumwita Nduli ila tumuombe tu Mwenyezi Mungu aendelee kuipumzisha roho yake.

Idd Amini aliitwa majina yote mabaya na nchi za magharibi baada ya utiriri wa matukio ya wadhalilisha Wazungu na kuwatimua Wahindi ili Waganda wenyewe waendeshe shughuli zote za kiuchumi na kukuza uchumi wao.

Miongoni mwa visanga alivyo vifanya Idd Amini ni pamoja na:-
  • Kuwaamuru mabalozi wa nchi za Ulaya wambebe juu juu na kiti kisha kumzungusha mitaani huku wananchi wakishangalia. Alifanya hivi kulipa kisasi jinsi babu zetu walivyowabeba wazungù.
  • Kuna wakati Amin aliomba msaada wa kifedha kwa Malkia Elizabeth, msaada ukachelewa, baada ya miezi kadhaa ndipo Amin akapewa hiyo pesa, kwa jeuri akamwambia sina shida na pesa yako, akairudisha. Malkia alikasirika sana.
  • Idd Amini aliwatimua Waasia wote, Wahindi na Waarabu ili kupisha Waganda wenyewe wafanye biashara.
Hivyo ni basi baada ya kuwatoa Wazungu dole la jicho, ndipo walipomuanza kumchonganisha Mwalimu na Amini ili Mwalimu ampige Amini na apotezwe kabisa.

KUKAWA na maneno kati ya Mwalimu na Amini ambayo hayakuwa mazuri, hatimaye yakapelekea vita ya mataifa mawili haya.

Habari za Idd Amini kula nyama za watu, je ilikuwa uzushi ama propaganda?

Je habari za Amin kuwapasua wanawake wajawazito, ilikuwa ni kweli au uzushi?

Je habari za Amini kuwatupa mto Nile walemavu zina ukweli gani? Je kuna uhusiano gani na ule wimbo wa Mchakamchaka Idd Amini akifa siwezi kulia, nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba?

Karibuni waungwana
Ni kweli kabisa Idi Amin alikuwa shujaa wa Afrika.

Hata Magu alikuwa shujaa wa Afrika na dunia, lakini mabeberu wakamuonea wivu, wakawatumia vibaraka wa ndani kumuwahisha ahera.

Uzuri wa Mangu ni kwamba kule mbinguni, Mungu amempa cheo cha mkuu wa malaika. Na analipwa bonge la mshahara, mara 10 ya mshahara wa Prof. Nabi kule kwa Madiba.
 
Aliwatimuaga wahindi- waliokuwa wafanya biashara uganda

Wahindi wakatimkia marekani na wakafanikiwa huko balaa kwenye biashara zao na badala ya kumlaani Iddy Amini wakamshukuru kwa kutimuliwa kulee na Iddy Amini na kusema wangekaa hata miaka mia uganda wadingepata mafanikio yalee waliyoyapata marekani kwa mda mfupi sana kwenye biashara zao

Wameweka picha za Iddy Amini kwenye maduka yao huko marekani kama shukrani kwa walibyofukuzwa na huyo jamaa
Wahindi namba nyingine mzee kuna kitabu cha Andy Chande kiliwekwa humu.Mzee wake alitoka kwao mwaka 1922 au 1925 kuja kufanya biashara huku bongo tena Bukene,Tabora -Tanzania na akamake .Huyo Chande alioa kwa tajiri namba moja ( muhindi) huko UG .Huyo tajiri Idd alichukua mali zake zote baadae akarudi akamake tena .Huyo Chande utajiri ambao mzee wake aliuhangaikia kwa miaka zaidi ya 35 ndani ya saa mbili tu ulitaifishwa na Nyerere lakini hakufa kinyonge.Wahindi,🙌🙌🙌
 
Ni kweli kabisa Idi Amin alikuwa shujaa wa Afrika.

Hata Magu alikuwa shujaa wa Afrika na dunia, lakini mabeberu wakamuonea wivu, wakawatumia vibaraka wa ndani kumuwahisha ahera.

Uzuri wa Mangu ni kwamba kule mbinguni, Mungu amempa cheo cha mkuu wa malaika. Na analipwa bonge la mshahara, mara 10 ya mshahara wa Prof. Nabi kule kwa Madiba.
Duh
 
..Alivamia ardhi ya Tanganyika.

..kuna jamaa mmoja aliniambia Nyerere hakutaka vita ile.

..anadai kulikuwa na makamanda wa Jwtz ambao ambao walikuwa na hasira na walisisitiza lazima Amin afundishwe adabu.

Hao wanaojifanya watu wakale wengi ni waongo sana, usipende kabisa kuwaamini
 
Wahindi namba nyingine mzee kuna kitabu cha Andy Chande kiliwekwa humu.Mzee wake alitoka kwao mwaka 1922 au 1925 kuja kufanya biashara huku bongo tena Bukene,Tabora -Tanzania na akamake .Huyo Chande alioa kwa tajiri namba moja ( muhindi) huko UG .Huyo tajiri Idd alichukua mali zake zote baadae akarudi akamake tena .Huyo Chande utajiri ambao mzee wake aliuhangaikia kwa miaka zaidi ya 35 ndani ya saa mbili tu ulitaifishwa na Nyerere lakini hakufa kinyonge.Wahindi,🙌🙌🙌

wahindi ni wapambanaji kinoma mkuu, Sisi kinachotutesa ni choyo tu.
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Ukweli ni kwamba Idd Amini alikuwa na kukosi chake maalum walikuwa wakivaa nguo za vitenge. Uganda waliwaita ichitenge, walikuwa kama watu wasiojulikana, wakikufuata hurudi. Hata Kikwete alikuwa na watu hawa wakiongozwa na Ramadhani Igwondu aliyemteka na kumtoa kucha na meno Dr. Ulimboka.
Pia magufuli alikuwa na watu wa aina hii. magufuli ni Mtakatifu wa kina Kulwa Jilala na Sukuma gang wote.

Bunge lililopitisha mkataba wa DP World ni matokeo ya utawala mbovu wa kifashisti wa magufuli
Naomba ni mtag ndugu yetu hapa pengine ana lakuchangia kwenye uhuru ulioutumia wakujieleza. Karibu ndugu Pascal Mayalla useme neno hapa

Asante msikilizaji
 
Huu ni ukweli ambao makada wa CCM hawataki kuusikia. Nyerere alizingua
Nyerere ndiye alianza kwa kumchokonoa Amin, Nyerere alihifadhi waasi wa Uganda akina Museveni na kuwapa mafunzo ya kijeshi na matunzo.
Huo ulikua uchokozi mbaya sana, hebu waza hapo msikie Kenya inawapa mafunzo maelfu ya wapiganaji waje kuipindua serikali ya Tanzania.
Historia ya huu ugomvi huwa hamtaji hiki alichokifanya Nyerere, huwa mnaanzia pale pa Amin kuvamia Kagera.
Nimekua Uganda, ukitaja mabaya ya Amin unaweza hata ukapigwa, wanamkumbuka sana, hususan leo ambapo wengi wanaamini Wahindi wameachiwa nchi wafanye watakavyo.
 
Uganda ipi wewe? Amini hajawahi kua mtu wa maana
 
Mtu aliyeivamia nchi yetu na kuwaua ndugu zetu wasio na hatia hawezi kuwa mtu mzuri! Labda kama alijutia makosa yake na kuomba msamaha.
 
Back
Top Bottom