Je, ni faida au hasara kwa Taasisi na Mashirika ya Umma kuajiri yenyewe bila kupitia Utumishi (Ajira Portal)?

sychellis

Senior Member
Oct 16, 2018
135
114
Kwa sasa hali imebadilika taasisi na mashirika mengi ya umma yanaajiri yenyewe kupitia Portal zao bila kuhusisha utumishi au Ajira portal. Leo hiii watu wanaomba kazi TRA kupitia portal ya TRA. NSSF pia watu wanamba kupitia uko na taasisi nyengine za umma.

Je, kuruhusu Mashirika na Taasisi za Umma kuajiri zenyewe ni faida kwa wananchi na Taasisi husika au kuna hasara ndani yake?
 
Safi tuu hata huko rushwa zipo

Taasisi zichichagulie watu wa kufanya nao kazi
 

Rejea....​

Rais Samia aagiza Mashirika ya Umma kuajiri Watumishi moja kwa moja


Watu wanashingilia bila kujua wanashingilia nini. Yakigeuka utawaskia tu, we subiri

Hii kitu ni hatari kupita maelezo.
Huko kwenye mashirika kumejaa upendeleo wa kiwango cha SGR, wakubwa wa hayo mashirika wataajiri wakwe, vimada, vijukuu, marafiki zao tupu.

Subiri uone kimbembe chake.
Katika hoja zilizokaa kutafakari, ni hii hapa chini
Mamlaka na taasisi zisipewe mamlaka ya kujiajiri bila mchakato wa ndani kuratibiwa na kusimamiwa na utumishi. Taasisi zipewe jukumu la kutangaza ajira na tarehe za usaili lakini jukumu la kusimamia mchakato mzima wa ajira wasipewe wao.
 
Je, Kuruhusu Mashirika na Taasisi za Umma kuajiri zenyewe ni Faida kwa wananchi na Taasisi husika Au Kuna Hasara ndani yake?.
Zipo faida zinazoweza kupatikana, mfano kuwa na ...Uwezo wa kuajiri haraka bila ya kufuata vigezo ??
...Mashirika wanaweza kuvutia wabobezi(walengwa) na hata kutoa fidia na faida zaidi za Ushindani.
...Mashirika yanaweza kuongeza Ufanisi na kuboresha utendaji kwa kuajiri wagombea bora kwa. mahitaji yao maalumu na misheni bila kujali mgombea ametoka wapi(athari mbaya).

Sheria za Utumishi wa Umma zinawekwa kwa sababu nyingi na moja ya sababu hizo ni kuhakikisha, usawa na uwazi katika mchakato wa kuajiri. Kinyume chake ni kujitafutia kesi na vurugu mexhi kama za huku mitandaoni(public scrutiny and or Public court) kitu ambacho kinaweza kuiweka Shirika husika katika malumbano yasiyo na tija.
...Upo uwezekano wa kujenga mtazamo wa upendeleo, rushwa na undugunization katika maamuzi yao ya kuajiri, kitu ambacho wanahudhuri wengi hapa JF wameelezea.
 
Back
Top Bottom