Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Ukishakubali Mungu yupo,ndiye chanzo cha kila kitu , basi ameumba dhambi kwa kusudi lake .
 
hoja thabiti kabisa hizi...nashangaa napoona kwamba tunaishi kwenye jamii inayoshindwa kuhoji maswali ya msingi kama haya
 
MPUMBAVU AMESEMA MOYONI MWAKE HAKUNA MUNGU

MDHALIMU KWA KIBURI CHA USO WAKE ASEMA HATAPATILIZA. JUMLA YA MAWAZO YAKE HAKUNA MUNGU
 
Hapa napo panachanganya hivi kweli shetani ana uwezo wa kupigana na Mungu muweza wa yote[emoji134] [emoji134]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Unazungumzia drones,bombs umesahau mstari usemao "nchi na vyote vijazavyo ni mali ya Mungu"

Mkuu ni vyake hivyo
 
Ukishakubali Mungu yupo,ndiye chanzo cha kila kitu , basi ameumba dhambi kwa kusudi lake .
"Ameumba dhambi kwa kusudi lake", dhambi/uovu ndio sababu hasa tunapata shida humu duniani. Sasa Mungu aliamua kuumba dhambi ili tupate tabu kweli?
 
Kuna mtu kathibitisha Mungu yupo hapa au bado stories tupu tu?
 
Kama unaamini hakuna Mungu huna la kujibu ila kama unaamini yupo basi aliumba kila kitu na dhambi ipo ndani ya " kila kitu " hivyo Mungu aliumba dhambi" utauliza kwa nini! Ukifa utaonana nae na utamuuliza kwa nini uturushie mrejesho huku duniani
 
So he knew before, that man will one day create such terrifying weapons and supersonic objects! isn't it
 
Wow! She can't go deep anymore, otherwise She gonna deny her premises!
 
Mkuu mimi nafikiri tungejikita kwenye sababu,,mfano kwa nini Mungu ajue kwamba huyu kiumbe Lucifer anaemuumba atakuja kuharibu kazi yake?? Ezekiel 28: ina majibu,,, kwamba Lucifer Alikuwa kaumbwa vizuri ila Alikuwa na tamaa,,,yako majibu kabisa kama ukiwa uko huru bila presha kutafuta majibu ya maswali yako.

Nimependa hapa uliposema anawajua walio wake toka kuwekwa misingi ya ulimwengu,,,mimi nikuulize kwamba wasi wasi wako ni nini kama labda hao walio wake mmoja wapo ni wewe?? Maana hakuwataja.
Ndio Unaweza ukawa na dhambi kama mimi na Baadae kumebaki dakika moja ufe ukatubu,,,nani anajua!
 
Huwa hatujiulizi maana ya ile miti miwili kwenye bustani ya Eden,,mti wa kwanza ulikuwa mti wa uzima na wa pili MTI WA MEMA NA MABAYA..na yote kaipanda Mungu.Kwa nini unahoji maswali mengi yanayohusu masahibu yetu wakati babu yetu wa siku nyingi alikula matunda ya mti wa mema na mabaya??

Dhambi kaiumba Mungu ni kweli lakini kuna namna alitaka tuishi ili isituathiri na wewe unajua.

Mtu anaposema eti Mungu alileta kifo maana hana accommodation za kutuhifadhi ni jambo la kustaajabisha,,,labda Kuna mtu aliwahi kujiuliza hizo sayari nyingine kaumbiwa nani?? Mtu anamwongelea Mungu kwamba ni failure pasi na kutafakari kwa kina kwa nini!!

Na tusisahau kitu kimoja zamani ya Adam Mungu Alikuwa anakaa na binadamu kila jioni anakuja kumsalimia Adam,,,je tunajua alikuwa anaongea nae nini??
 
Kilichobaki tunatakiwa kuishi kwa imani tu..Kwa hakika mimi naweza Kusema Mungu ana upendo sana na anatupenda sana.

Na hata mtu ukafa ukaenda motoni au paradise hakika unastahili sana unapoenda.Maana unastahili kulingana na ulichokuwa unafanya hapa duniani.
 

Utasemaje kuwa Lucifer alikuwa kaumbwa vizuri halafu tena awe na tamaa? Kitendo cha lucifer kuwa na tamaa inadhihirisha ya kwanba Lucifer aliumbwa akiwa na Mapungufu. Je kwanini uwezo wa Mungu umeshindwaje kujua hayo mapungufu na kisha kumfanya awe mkamilifu ili asije hasi?

Na swala la pili ni kwamba kitendo cha Mungu kusema kuwa "anajua walio wake toka kuwekwa misingi ya ulimwengu" ina maanisha kuwa wakati Mungu anamuumba mtu anajua fika ya kwamba huyu mtu X ataenda motoni na huyu mtu Y ataenda peponi. Huyu mtu X hata afanye jitihada kiasi gani hawezi kuwa mtu mwema kwasababu alishaumbwa kuwa sio mwema. Na hutu mtu Y hata hata apate vishawishi kiasi gani hawezi kuwa muovu kwasababu alishaumbwa kuwa mwema. Mtu muovu kubadilika kuwa mwema sio kwa jitihada zake bali ndivyo alivyopangawia awe alkadhalika kwa mtu mwema kuwa mtu muovu ndivyo alivyopangiwa awe hivyo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…