Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Yani kifupi ni kuwa huyo aitwaye shetani ameshinda, Mungu anawachukuwa watu kuwakimbiza mbinguni coz tayari shetani amejimilikisha dunia, dunia iliyoumbwa na Mungu.
Kwa hiyo wewe ni rahis kuamini kwamba shetan ana nguvu kuliko kuamini uwepo wa Mungu? Jaribu kukimbizana na upepo
 
Halafu ujue hawa wawili wanakutana sana, tangu shetani afukuzwe huko juu.

~Walikutana kipindi Ayoub anataka kujaribiwa, wakakubaliana kuwa Ayoub ajaribiwe tu ila asiuwawe...WALIKUBALIANA.

~Walikutana tena Yesu alipokuwa akijaribiwa huko nyikani, ila Yesu akamfukuza baada ya shetani kufanya mzaha na utani.

Kumbe bwana wanakutana na kukubaliana kabisa...Dah!!
Bwahahaa haha hahaaa.....
 
Hivi maswali ni magumu sana?

Kukesha kote kanisani/msikitini nashindwa kweli kujibu maswali marahisi kama haya kwa mistari ya biblia/Quran tukufu!.

Kumbe kanisani/msikitini naenda kupoteza muda tu
Yaaani inashangaza sana....ujinga ujinga mtupu " tu ...tunaongopeana watu wazima ....""
 
Nimekumbuka yule dogo aliyewashitaki wazazi wake kwa kumzaa mzungu badala ya mweusi


Hivi siku ya kiama haiwezekan kukata rufaa ukihukumiwa kwenda jehanam!?

Kwanza wewe hukuomba uumbwe ila yeye ndio alikuumba kwa malengo yake sasa kosa lako ni nini hadi upelekwe jehanam?
hapa ndio napata sana ukakasi
 
Usipende kuongea mambo usioyajua.
Jadili kile akili yako ikiwezacho
 
Ili uhesabiwe kuwa umefanya kosa lazima uvunje sheria. Sheria zimewekwa ili kuzuia makosa.

Kosa/dhambi ya kwanza kabisa duniani kwa mujibu wa maandiko ni usile tunda la mti wa katikati hii amri walipewa Adam na Evah/Hawa. Na adhabu yake ukipatikana na kosa hili ilikuwa ni kifo. "Mungu akasema, usile tunda la mti wa katikati, hakika siku mkila mtakufa".

Evah/Hawa alikuwa wa kwanza kula. Kisha akampa ma mumewe Adam naye akala. Mungu akaenda kinyume na utaratibu aliojiwekea. Badala ya kutoa adhabu ya kifo akabatilisha adhabu ikawa hii inayotutesa kwa sasa. Adhabu ikawa Utakula kwa josho(mwanamume) na kuzaa kwa Uchungu(mwanamke.) hapa ukiangalia kwa makini utaona kosa moja lina adhabu mbili tofauti.

Kaini alihesabiwa dhambi na Mwenyeenzi Mungu kwa kumuua ndugu yake Abbel/Habil. Nimeshindwa kutambua kosa la Kaini sababu kwa mujibu wa biblia Mungu hakuwa ameweka au kukataza kuuwa mtu mwingine. Sababu Dhambi ni kosa la kuvunja kusudi amri ya Mungu. Kaini kaingiaje hatiani wakati hakuvunja amri ya Mungu?
 
Kwa kifupi "ndiyo " tuliambiwa Mungu ni muumbaji wa vitu vyote kwa malengo yake. Hata hivyo baada ya kutafakari kwa makini, ni kwa nini Mungu aweke ubaya kwa watu wake? Chukulia kama hekaya za abunuasi
 
Back
Top Bottom