Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,309
- 11,406
Katika kitabu cha Ufunuo 13:16-18 tunasoma,
Naye awafanya wote... wapokee chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao... na hesabu yake ni 666.
Katika maandiko matakatifu inaonyesha kuwa "alama ama chapa" ina maanisha ishara ya utii na mamlaka ya kiroho juu ya wanadamu wengi.
Kupokea chapa ama alama inahusu kile kilichopo akilini yaani nia ya kukubaliana kwa dhati ya moyo wako wote, kupokea katika mkono wa kiume ni kile ambacho utalazimika kukitenda.
Kupokea katika Mkono wa kiume unalazimika kufanya ama kutenda, na kupokea katika Paji la uso unalazimika na kukubaliana kwa dhati hadharami kuwa kipo akilini mwako na unakiamini
Chapa ya 666 inalingana na mfumo wa kibinadamu wenye kuhusisha mamlaka za kidini na kisiasa ambao unajipa mamlaka ya kubadilisha sheria ya Mungu na kuweka mamlaka ya kiroho kwa utii wa jinsi ya kibinadamu.
Kwa kuwa mpango mzima wa wokovu unahusisha utii juu ya Jina la Mungu Muumbaji, Cheo chake, na Eneo lake la mamlaka, hivyo basi jambo muhimu la kukumbuka ni juu ya hesabu hii ya 666 kwamba ni ya kibinadamu iliyo kinyume kabisa na mpango wa wokovu wa Mungu wenye kukamilika kupitia namba 777 yaani ili uenaendane na mfumo wa utiifu wa imani ya kiroho kwa wanadamu wote duniani.
Hii ni namba ya kutokamilika kwa kuwa namba 7 ni kamili ya Mungu. 6 ni namba ya mwanadamu - imetengenezwa kww asili ya siku ya 6.
Kwa hiyo kupitia pattern ya namba 666 ni kwamba mwanadamu anajaribu kuchukua nafasi ya Mungu kwa kuharifu amri zake kuu kupitia mpango wake kamilifu wa pattern ya 777
Alama ama chapa ya mnyama ni
suala la mpambano katika Mungu na Ibilisi juu ya ibada na mamlaka ya kuwatiisha watu wote kiimani kwa kile kiitwacho mungu
Alama ya mnyama kukubali mamlaka ya wanadamu juu ya Amri ya Mungu.
Alama ya Mungu ni kukubali mamlaka ya Mungu kama Muumbaji.
Toka kuumbwa kwa mwanadamu wa kwanza hapajatokea mwanadamu aliyeitawala dunia na hata kujiinuwa nafsi yake juu na kujifanya yeye ndiye mungu hapa duniani, hata kujifanya ndiye pekee astahiliye hicho cheo mbele ya wanadamu wote duniani na kulazimisha aabudiwe na watu wote duniani, rejea 2 Wathesalonike 2:3-4
Maandiko yanatuonyesha anguko la kwanza la Adamu akiwa katika bustani ya Eden, rejea Mwanzo 3:1-24. Sura hii ndiyo ilikuwa ni yenye kuonyesha uasi wa Adamu wa kwanza hata kuiingiza uzao wote wa wanadamu katika hatia ya dhambi na mauti. Huyu ndiye Adamu wa kwanza mwenye tafsiri ya namba ya kibinadamu 6.
Lakini katika ramani ya mpango wa wokovu ili kuzishinda nguvu za mauti ilipasa aje Adamu wa pili. Hi ilitokana na sababu ya kuwa hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi ambaye angeweza kufanya hivyo, rejea Ufunuo 5:3-10. Ujio wa Yesu Kristo na kuweza kuzishinda nguvu za mauti na kuzimu akawa Adamu wa pili yaani namba ya kipekee kabisa akiwa ni Mwana wa Mungu yaani mwenye tafsiri ya namba 66 rejea 1 Wakorintho 15:22-29, Waebrania 1:1-14, Ufunuo 1:17-18.
Mwisho wa dhambi, mauti na kuzimu utatokea atakapo funuliwa mpinga Kristo, ataingia jukwaani kwa maigizo kama mtu wa haki, ni mpanda farasi asiyefahamika jina lake lakini amempanda farasi mweupe rejea Ufunuo 6:1-2 lakini Kristo halisi na wa kweli hutambulika kwa jina lake, na ndiye pekee mwenye mamlaka ya kumpanda farasi halisi mweupe, rejea Ufunuo 19:11-16
Kufinuliwa rasmi kwa huyu Adamu wa tatu ndipo utimilifu wa wokovu utakapotimia. Huyu mtu wa kuasi ndiye atakayebeba nafsi ya chapa halisi ya Ibilisi mwenyewe katika umbile la kibidamu, ndiye atakaye ibeba tafsiri ya namba 666 na jina lake halisi ni Mauti na kuzimu itamfuata nyuma yake, rejea Ufunuo 6:7-8, 1 Wakorintho 15:26-28
Kwa hiyo kupitia tafsiri ya namba za kimaandiko hapa tunapa ufahamu kuwa,
*6 ikiwa moja ni namba ya Adamu wa kwanza rejea Mwanzo 1:26-31, 5:12
*66 yaani 6 zikiwa mbili ni Adamu wa pili ambaye ndiye Yesu Kristo rejea Mithali 8:22-31, Yohana 1:17-18, 17:1-5, 1 Wakorintho 15:20-23
*666 yaani 6 zikiwa mpangilio wa 6 tatu ni Adamu wa tatu ambaye ndiye mpinga Kristo rejea Ufunuo 13:18
Huyu Adamu wa tatu ndiye atakaye ipeleka dunia katika mwisho wa historia na mwisho wa wakovu hata idadi ya warithi wa ufalme ujao wa Mungu ipate kutimia. Huyu atakuwa ndiye Adamu atakaye pewa mamlaka ya kidini na kiserikali apate kuitawala dunia yote kwa siku 1,260.
Hawa Adamu watatu ndiyo wanadamu pekee waliopata kibali cha mbingu juu ya utawala wa vitu vyote duniani. Hii ndiyo pattern ya 666 yenye mpangilio wa kutupeleka kwenye uasi mkuu wa kidunia kutokea katika mnara wa Babeli. Wa kwanza na wa pili walipata kutoka kwa Mungu mwenyewe. Lakini watatu atakuja kukabidhiwa Ibilisi na nabii wa uwongo na kuunda roho 3 za uchafu mfano wa vyura zipotoshao watu wote.