Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Kama unaamini hakuna Mungu huna la kujibu ila kama unaamini yupo basi aliumba kila kitu na dhambi ipo ndani ya " kila kitu " hivyo Mungu aliumba dhambi" utauliza kwa nini! Ukifa utaonana nae na utamuuliza kwa nini uturushie mrejesho huku duniani
Kwani dhambi ni nini mkuu?
 
Hilo swali la kwanza liko tough,,ila kwa Kusema kawaida bila reference nawaza kwamba Mungu alikuwa akitafuta mshindani mwenye nguvu ila ambae kamuumba mwenyewe na ambae hawezi kumshinda.Maana kamchukulia Mungu malaika wake kwa kuwadanganya na pia hawa malaika wamekuwa chini yake akaweza kuanzisha ufalme.

Kuhusu Mungu kuwajua walio wake,,kila mmoja ana probability ya kuingia mbinguni.Ndio maana Suleiman Anasema kwenye mhubiri kwamba usiwe na haki sana wala usiwe na dhambi sana.Fanya mambo sahihi ya kukupa furaha ila usivuke mipaka.

Kuna mtu anafundisha dini namkubali sana,,,kuna siku alikuwa akifundisha kuhusu selection inayofanyika hapa duniani kwamba Mungu anatafuta watu wakaikae ile sehemu walioondoka malaika walioumeza uongo wa Luci.idadi ni hesabu ya 1/3 ya malaika wote waliokuwa mwanzo.Kwa hio hapa duniani tuko wengi ila mchujo unafanyika.kikubwa Jitahidi ufurahi Maana hujui kwamba wewe ni x,y au z
Utasemaje kuwa Lucifer alikuwa kaumbwa vizuri halafu tena awe na tamaa? Kitendo cha lucifer kuwa na tamaa inadhihirisha ya kwanba Lucifer aliumbwa akiwa na Mapungufu. Je kwanini uwezo wa Mungu umeshindwaje kujua hayo mapungufu na kisha kumfanya awe mkamilifu ili asije hasi?

Na swala la pili ni kwamba kitendo cha Mungu kusema kuwa "anajua walio wake toka kuwekwa misingi ya ulimwengu" ina maanisha kuwa wakati Mungu anamuumba mtu anajua fika ya kwamba huyu mtu X ataenda motoni na huyu mtu Y ataenda peponi. Huyu mtu X hata afanye jitihada kiasi gani hawezi kuwa mtu mwema kwasababu alishaumbwa kuwa sio mwema. Na hutu mtu Y hata hata apate vishawishi kiasi gani hawezi kuwa muovu kwasababu alishaumbwa kuwa mwema. Mtu muovu kubadilika kuwa mwema sio kwa jitihada zake bali ndivyo alivyopangawia awe alkadhalika kwa mtu mwema kuwa mtu muovu ndivyo alivyopangiwa awe hivyo.
 
Mungu amtafute mshindani ili iweje? Mungu Anafaidika nini na huo ushindani hadi amuumbe mshindani?

Naomba nipe hiyo probability ya mtu kwenda peponi ikiwa; wakati Mungu anamuumba mtu X alijua ya kwamba huyu fulani ninayemuumba akienda duniani atakuwa ni mzinzi na mwisho wa siku atakufa akiwa mtu wa motoni. Embu naomba nipe uwezekano wa huyu mtu kuja duniani na akawa kinyume na kile alichokipanga Mungu pindi anamuumba huyo mtu yaani akaja duniani na akawa sio mzinifu na mwisho akafa akiwa wa peponi.
 
Mungu alitafuta mshindani ili huyu mshindani awe kipimo cha kuwapima wale anaotaka Mungu watimize kusudio fulani,,waishi maisha flani ya haki,awapime e.g Ayubu,,,au daudi alivyoona yule mwanamke anaoga pale naamini shetani/luci hakuwa mbali,,,pia tusiende mbali Adam.Kama Adam angevuka uongo wa luci leo hii angekuwepo pia na tusingekuwa na maswali mengi sana.
Kwa hio utaona huyu mshindani akifanya mchujo hata kwako.

Kuhusu huyu mtu aliezaliwa na akawa mzinzi,,hapa tunaweza kutumia hata sayansi kidogo kwamba tabia za mwanadamu ziko za natural characteristics na aquired characteristics,,sidhani kama Mungu anakuwa amemuwekea hatma mtu kuwa total saturated kwenye dhambi fulani hadi ashindwe kuiacha na aende motoni,,ila hatima ya mtu huitengeneza mwenyewe kulingana na changamoto anazokutana nazo.labda tukiongezea namna ya kuchagua katika muktadha wa kuwajua walio wake

Hasa huyo mshindani anawapima binadamu au Mungu ndio anajipima yeye mwenyewe? Kwasababu yeye Mungu ndiye aliyemuumba huyo mshindani na ndiye yeye huyo huyo aliyeumba na binadamu, sasa kama binadamu ana mapungufu inamaana yeye ndio kafeli kuumba huyo binadamu akawa mkamilifu. Kwahiyo Mungu anampima binadamu ili ajue kakosea kumuumba kwa ukamilifu kwa asilimia ngapi?

Nimeuliza pia kuwa Mungu anafaidika na nini kwa kumuumba huyo mshindani? Wewe tu kama mzazi hupendi wala hutafurahia kuona mtoto wako anapata matatizo kwahiyo la kwanza utajitahidi kumwekea mazingira ya mwanao kutopata matatizo yoyote. Sasa kwa Mungu kumuumba mshindani kwa makusudi huoni inapingana na dai la Mungu ni mwenye upendo?

La pili ni kwamba binadamu wote wanaumbwa na Mungu mmoja si ndivyo? kama ndivyo na je akili ya binadamu pia anajiwekea mwenyewe huyo binadamu au Mungu ndio anamwekea na akili? Unadhani ni Kwanini akili ya mtu X iende duniani kuchagua dhambi wakati akili ya mtu Y isichague dhambi wakati wameumbwa na Mungu mmoja? Wakati Mungu anamuumba mtu X si alijua fika kuwa akili yake itaenda kuchagua dhambi duniani, je kitendo kumpeleka duniania hivyo hivyo pasipo kurekebisha kwa mfanya awe mkamilifu inaashiria nini?
 
NDIYO na SIYO..!

Najua hutaelewa maana kichwa chako kitakuwa kidogo. Iko hivi Mungu ni chanzo cha kila kitu hapa duniani na mbinguni ila sasa kwasababu na makusudi maalum.

Kitalaam( sheria&law philosophy) waliosoma criminology wanajua kuwa ni sheria tu, inayoweza kuunda/kuumba kosa. Kwa msingi huo nasema dhambi ni kosa au crime kwa Mungu na hakuna dhambi ambayo haivunji AMRI/SHERIA ZA Mungu rejea vitabu vya sheria ya Musa(vitabu vitano vya mwanzo katika agano jipya).

Pili siyo Mungu aliyeumba dhambi Mungu kaumba sheria na kuziwekea utaratibu wa kuzitekeleza siye tunaozivunja ndiyo waumba dhambi, ingawa Shetani anasingiziwa kila kukicha.

Bila shaka nimejibu kwa ufupi.
If God is a the ordering principle of the seen and unseen universe means everything happen must be mastermainded by God isn't?? Who created thing different from God??
 
Wakuu hamjambo!

Kama kichwa cha Uzi huu kinavyouliza, Mimi nikiri kuwa naamini uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba vyote vinavyoonekana na visivyoonekana pia.

Katika vitabu mbali mbali vya dini, tunaelezwa kuwa dhambi ilitokana na uasi alioufanya shetani dhidi ya Mungu, biblia inaenda mbali kwa kudai kuwa vita vilipiganwa huko mbinguni na shetani alishindwa na akatupwa duniani akiwa na theluthi ya malaika wakawa upande wake.

Maswali:

1. Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile, tena alikuwa mbinguni kwenye utakatifu wa MUNGU, je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi Ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?

2. Kama MUNGU hujua mwanzo hata mwisho wa viumbe vyake, INA maana alikuwa anajua kuwa shetani atakuja kuasi baadae na kusababisha dhambi, kwanini alimuumba?
Jambo la kufikiria hapa ni kuona kwamba MUNGU alimuumba shetani/Lucifer ( dhambi) mahususi ili kuja kuwa upande maovu. Dhana hii inadhihirisha kuwa MUNGU ndie aliyeumba dhambi.

3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?

4. Je, Dini ni matokeo ya mwanadamu kumhofia shetani?
Tunaishi katika jamii ambazo kila MTU ana juhudi za kujikwamua kuondokana na shida Kama magonjwa, njaa, vita, ambazo Mara nyingi wanadamu wanahesabu kuwa hayo yote ni sababu ya shetani, na dini wanaona ndio kimbilio ili kumkwepa shetani asiwadhuru.
Lakini wao wanaamini kuwa wanasali ili kumtukuza MUNGU, lakini kiukweli dini ni hofu ( fear of unknown) isiyo na ithibati yoyote.

5. Je, Mungu anawapenda wanadamu? Hapa jibu laweza kuwa ni ndiyo, bahati mbaya sana ukiangalia uhalisia toka zamani kuna ugumu wa kusema ndiyo au hapana.
Tunaambiwa kuwa mbinguni kulikuwa na vita Kali sana, mwaishowe malaika aitwaye Mikaeli alimshinda shetani, Mungu akamtupa ibilisi huyo huyo duniani kwa wanadamu anaowapenda sana. Mungu hakuona sehemu nyingine ya kulitupa hilo joka ila duniani ambako ndio wanadamu aliwaweka. Hii ni sawa na kuwarushia watoto wako furushi lenye nge wengi huku umewafungia chumbani na kuwataka wajikinge wasing'atwe hata kidogo.

Nimekuja kuamini kuwa: MUNGU yupo ila dini zote ni michezo ya kukamata fikra za wanadamu tu, inawezekana kabisa kuwa dini ziluletwa na shetani mwenyewe ili kuwachonganisha wanadamu wasiishi kwa upendo na amani.
Angalia jinsi Palestine na Israel, syria , Iraq n.k wanavyouana kwa misingi ya dini.

Niishie hapo, naomba waumini/maswahaba mje mtueleze hizi hoja.

Cc: Mshana Jr
Cc: Kiranga
Na wanajamvi wote karibuni.

Mungu ameumba viumbe. Dhambi siyo kiumbe. Hivyo, Mungu hawezi kuumba dhambi.
 
Hawezi kujibu hoja hii
Utasemaje kuwa Lucifer alikuwa kaumbwa vizuri halafu tena awe na tamaa? Kitendo cha lucifer kuwa na tamaa inadhihirisha ya kwanba Lucifer aliumbwa akiwa na Mapungufu. Je kwanini uwezo wa Mungu umeshindwaje kujua hayo mapungufu na kisha kumfanya awe mkamilifu ili asije hasi?

Na swala la pili ni kwamba kitendo cha Mungu kusema kuwa "anajua walio wake toka kuwekwa misingi ya ulimwengu" ina maanisha kuwa wakati Mungu anamuumba mtu anajua fika ya kwamba huyu mtu X ataenda motoni na huyu mtu Y ataenda peponi. Huyu mtu X hata afanye jitihada kiasi gani hawezi kuwa mtu mwema kwasababu alishaumbwa kuwa sio mwema. Na hutu mtu Y hata hata apate vishawishi kiasi gani hawezi kuwa muovu kwasababu alishaumbwa kuwa mwema. Mtu muovu kubadilika kuwa mwema sio kwa jitihada zake bali ndivyo alivyopangawia awe alkadhalika kwa mtu mwema kuwa mtu muovu ndivyo alivyopangiwa awe hivyo.
 
Mimi pia nina swali hapo,

Je, kabla Mungu hajaumba kitu chochote, alikuwa anakaa wapi!?

Makazi yake yalikuwa wapi!?

Tunaomba mtuelimishe wale waaminio!!
 
Dhambi inajadiliwa kwa misingi ya dini,
Dhami ni tendo au hali yoyote inayoenda kinyume na sheria au amri za Mungu.
Hata mimi nilitaka kuuliza hilo

Tunawezaje kujadili jambo ambalo haoijafafanuliwa bado..!?

Nakazia_Dhambi ni nini..? halafu tuendelee

Saguda47
 
Mimi pia nina swali hapo,

Je, kabla Mungu hajaumba kitu chochote, alikuwa anakaa wapi!?

Makazi yake yalikuwa wapi!?

Tunaomba mtuelimishe wale waaminio!!
Nadhani ingekuwa vizuri pia kwanza tutoe 'working definition ya Mungu' ili kutokana na hiyo definition tuweze kuona kama Mungu anahitaji makazi au alikuwa akikaa mahali fulani kabla ya kuumba chochote au alianza alipoanza kuumba.
 
Kuna kitabu kinaitwa Philosophy of Religion, kilipandishwa humu na mkuu Kiranga , aisee watu wanahoji ni balaa!!
 
huwezi co-conclude kwasababu ukijiuliza tena uwepo wa universe unakosa jibu maana haviwezi kujiumba vyenyewe
Na hapo kwenye hoja hii uliyotoa unaweza kujiuliza swali hili:

Kama Mungu aliumba universe, Je yeye aliumbwa na nani!?
 
Na hapo kwenye hoja hii uliyotoa unaweza kujiuliza swali hili:

Kama Mungu aliumba universe, Je yeye aliumbwa na nani!?
Hilo swali gumu sana na huwezi kulijibu mpaka utakufa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom