Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Ni kwamba anajichanganya ama sisi ndio tunajichanganya?

Hivi umewahi kuona samaki anajiweka nyavuni ama ndege anajiweka mtegoni? Binadamu kafanikiwa kujiweka kitanzini mwa mikono yake mwenyewe (atomic bomb, weapons of mass destruction, biological weapons of mass destruction, guns, drones....etc) halafu analalamika Mungu kasababisha maafa! How? !?

My point is ameshatupa Uhai na uamuzi juu ya maisha yetu ya sasa na baadae anakuwaje tena responsible na maovu ambayo tunayasababisha sisi wenyewe kwa kisingizio cha maendeleo ya kijamii na teknolojia? Imani yangu; Our Life - Our Choices / Our Choices - Our Life.....

Kibaya zaidi [HASHTAG]#Karma[/HASHTAG] + [HASHTAG]#Fate[/HASHTAG] are so real!
Ahaa kama ni ivo basi mungu hajapanga wala hajui nini kitatokea kesho si ndio.mkuu? Ukisema Atomic ivi.unajua kuwa hata Dawa ni sumu? Sitaki kuamini kama hujui kuwa kitu chochote kikitumika vibaya kina leta madhara, dawa za kulevya zinatumiwa na doctors wakati wa operations je tuache kuzifanyia research kwa vile zinaleta mateja?
Nani aliyetengeneza hicho kitanzi anachojiweka mwanadamu? Je ni mungu au kama ndie je bado ana upendo nasi ile hali katuwekea mtego afu later atupe adhabu
 
Dini zote ni mifumo ya maisha ya jamii fulani, Uharaka wao wa Kufanya maendeleo na kuwaweka superior ndio ulipelekea Mifumo yao ya maisha (dini) kutapakaa dunia nzima wapo wajanja pia kama wamisionari waliona fursa ya dini na kuamua kuitumia kuja Nayo mataifa mbalimbali na kuwapa imani hizo kwa mgongo wa kuwahadaa ili iwe rahsi kuwa colonize, Wewe unadhani babu zetu wangekuwa superior kiuchumi, kijamii wange copy takataka za Uislamu na Ukiristo wa wazungu?? Yani kisa Uarabuni hakuna miti ni jangwa na mbao hakuna na nyie afrika mliokuwa na mistu ya kutosha mnaliridhi Uzikaji bila kuweka mtu kwenye Frame za mbao(Jeneza), Leo unaambiwa atakae ibariki Israel nae atabarikiwa atakaye ilani nae ataalaaniwa kweli tunashindwa kureason vitu simple kama ivi nashangaa mno kuona Machinga wanatembea na Bendera za israel, yani Unaona hawa hawa wanaombea watu ni wameona fursa ya dini ndio mana wamejazana mijini kwenye pesa

Ok kabla ya hao wazungu na waarabu kuja mababu zako walikuaje?
 
Walikuwa na taratibu zao za kuabudu mana dini ni mfumo wa maisha ya watu kulingana na mazingira yao
Kuwa na taratibu za kuabudu na dini ni vitu viwili tofauti,hata hao waarabu na wazungu walikuwa na taratibu zao za kuabudu kabla ya ujio wa uislamu na ukristo,dini ni zaidi ya taratibu za kuabudu ni mfumo wa maisha.
 
Nilichogundua humu Mungu anaelezwa kwa mafundisho ya kikristo na wakristo imani yao imebebwa na imani ya uwepo wa Mungu,na ndiyo maana wengi tunaona wakisema dini haina mchango wowote na ni mpango tu wa binaadamu.
Tatizo mkuu watu wamegundua kuwa dini hazina faida ktk dunia ya leo kumfanyia wema mwenzako ni ungwana na si vitabu viseme
 
Kwani dini inafundisha kinyume na hayo?
Dini ukiingia deep sana utakua frustrated
Mungu anampa yoyote chochote mda wowote
Na kama ni watu wenye hali ngumu kimaisha basi ni wale walioshika dini sanaa...js observe
 
Nimefungua huu uzi mida hii nimesoma comments zote, one at a time.....haki Nimeogopa watu mnavyomkana Mungu!! Muumba wa Ardhi na Mbingu mbele yenu amekua si lolote si chochote?! Hatari sana dunia inaenda kasi ya ajabu!!

***Sorry sina maana ya kuwakwaza ila nimeshangaa sana, hadi usingizi umekata! !!!
Ugumu wa maisha
Kuomba Mungu doesnt excuse u from life trials
Unadhani walioko syria hawaombi Mungu?.
 
Dini ukiingia deep sana utakua frustrated
Mungu anampa yoyote chochote mda wowote
Na kama ni watu wenye hali ngumu kimaisha basi ni wale walioshika dini sanaa...js observe
Waarabu huko wameshika dini na bado ni matajiri,sasa sijui utasema waafrika wameshika dini kuliko waarabu?

Ni kweli Mungu humpa yeyote yule.
 
Ila mkuu kiuhalisia maisha ni zaidi ya kumfanyia mtu wema,maisha yanahitaji muongozo.
watu wamegundua sasa hivi hawapimi tena uzuri wa dini kwa kutumia vitabu bali wanapima kwa matendo yako thats why kuamini dini jambo gumu kwakuwa dini sasa ndio zinazoleta chuki vita embu angalia palestina
 
watu wamegundua sasa hivi hawapimi tena uzuri wa dini kwa kutumia vitabu bali wanapima kwa matendo yako thats why kuamini dini jambo gumu kwakuwa dini sasa ndio zinazoleta chuki vita embu angalia palestina
Mkuu unazungumzia matendo ya watu au dini? maana matendo ya watu ndiyo yamesababisha vita kuu mbili za dunia,na sasa tunaambiwa inaweza kutokea vita kuu ya dunia ya tatu.

Dini ina mafundisho kuishi kwa amani na kuilinda hiyo amani.
 
Ugumu wa maisha
Kuomba Mungu doesnt excuse u from life trials
Unadhani walioko syria hawaombi Mungu?.


Life trials are the main reason why we are created. Loosing faith and doing bad things simply because life is hard is also not an excuse that God should be blamed for all our misfortunes.
 
Life trials are the main reason why we are created. Loosing faith and doing bad things simply because life is hard is also not an excuse that God should be blamed for all our misfortunes.
Oh baby give me a break...God has heaven why cant he js cut this short and take us all there?binafsi i js wanna go to heaven

Loss of faith ni kwa sababu kwny maisha unaishi vile atakavyo Mungu na sio utakavyo wewe
Ye ndo Mungu bwn tutafanyaje ss
Am not blaming God...i js realized life rolls his way not anyones way
 
Ahaa kama ni ivo basi mungu hajapanga wala hajui nini kitatokea kesho si ndio.mkuu? Ukisema Atomic ivi.unajua kuwa hata Dawa ni sumu? Sitaki kuamini kama hujui kuwa kitu chochote kikitumika vibaya kina leta madhara, dawa za kulevya zinatumiwa na doctors wakati wa operations je tuache kuzifanyia research kwa vile zinaleta mateja?
Nani aliyetengeneza hicho kitanzi anachojiweka mwanadamu? Je ni mungu au kama ndie je bado ana upendo nasi ile hali katuwekea mtego afu later atupe adhabu


Anajua kila kitu, ya siri na dhahiri, anajua yaliyomo ndani ya vifua vyetu hata kabla hayajatoka na ndio maana akatuonya kwa vitabu vitakatifu. Na hayo maandiko ni kama ramani ya maisha upite wapi ufanye nini usipite wapi husifanye nini......yes dawa zinamadhara sana tu nafahamu na ndio maana kuna Onyo la "matumizi mabaya/kuzidisha ........ni hatari kwa maisha yako"" same as Mungu kaumba Mwana Adam na kumpa mamlaka juu ya ardhi, kazi kwake kuchagua kinalomfaa, jema ama baya na on top of that kampa na maandiko !
 
Oh baby give me a break...God has heaven why cant he js cut this short and take us all there?binafsi i js wanna go to heaven

Loss of faith ni kwa sababu kwny maisha unaishi vile atakavyo Mungu na sio utakavyo wewe
Ye ndo Mungu bwn tutafanyaje ss
Am not blaming God...i js realized life rolls his way not anyones way



Chief as much as huwezi kukuta uncut diamond or gold or ruby kwenye jewelry store then ndivyo hivyo ulivyo uumbaji, all the pain and misery is to bring out the best out of us and to cleanse us off of all the darkness that was curses upon us (humans) when Adam + Eve disobeyed God.
 
Ukisoma biblia vizuri utagundua Mungu ni mwenye upendo wa Ajabu,yaani ametupa uhuru na utashi wa kimaamuzi either kumfuata yeye au la,lakini kwa msaada wa Roho mtakatifu hesema nasi kila sekunde. Mfano mtu anapotaka kufanya dhambi nafsini anajua ni kosa ila hupotezea kwa kuwa amepewa uhuru huo. Mungu ni Mungu tu ufahamu wetu hauwezi kumpima,kumchunguza wala kupata picha halisi yeye jinsi alivyo na mipango yake.
Kwa ufupi pitia hapa...1 KOR. 2:6-16
Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu
. ...
Pia anasema
YER. 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa"
Sasa fikiria kabla hujaumbwa ulikuwa wapi na badala ya kufa utakuwa wapi?
1 WAKORINTHO15:42..
Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko...
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo na si hadithi zilizotungwa na watu tu?
Mungu yupo na ndio maana mleta mada akaandika alichoandika na ndio maana na wewe ukaja kuchangia....
Angekuwa hayupo asingetajwa hapa wala kujadiliwa na yeyote yule.. Kisichopo hakipo
 
Back
Top Bottom