KARIBU KWENYE MADA WANA GREAT THINKERS 🧠 ☕️
Unaweza vipi kusoma mawazo ya mtu mwingine au kujua kinachoendelea kwenye akili yake?
Unaamini kama kuna watu wanaoweza kusoma akili au mawazo ya watu wengine?
Unadhani ni nini huwa kinatokea pale mtu anapoona maandishi ya mtu au akiwa kwenye mazungumzo na mtu mwingine, halafu akagundua kwamba huyu mtu anawaza kitu fulani?
Na ajabu, unakuta baadae yule mtu anafanya kitendo au vitendo vinavyothibitisha kwamba yale aliyogundua mwanzo yalikuwa sahihi
Kisayansi hali hii inaelewekaje?
Hawa watu tunaweza kuwaita watambuzi.watu wenye intuition kubwa wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua watu, au ni geniuses?
Na wewe binafsi unaamini unaweza kusoma akili ya mtu?
Kama ndiyo unafanya hivyo kwa namna gani?
Maoni yangu 👇
Kikawaida kabisa, naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kutambua mambo hata bila mtu kuyaeleza moja kwa moja
Sio kwamba wanatumia akili ya ajabu au wanaingia kwenye akili ya mtu mwingine bali kuna wakati mtu akiwa makini sana anaweza kuona signals ndogo ndogo ambazo watu wengine hawazioni
Hata kama mtu anajaribu kufake au kuficha mawazo yake kwa kuongea au kuandika kitu tofauti na anachohisi, ukiwa makini sana unaweza kugundua kuna kitu hakipo sawa
Ni sawa na mtu ambaye anaweza kukuonyesha kwamba amefurahi sana kwa sababu umepata kazi
Anaweza kucheka kukusifia na kukuambia:
Hongera sana ShesRise_1 nimefurahi kwa ajili yako umepata kazi
Lakini wakati huo huo kuna signals nyingine unaweza kuziona
Labda kwenye facial expression yake namna anavyocheka tone la sauti macho, movements za mikono, posture yake au hata namna anavyoendelea na mazungumzo
Unaona kabisa yeye wa ndani
Na yeye wa njee ni kama mifumo haisomani
Na kama wewe ni mtu ambaye una observation nzuri na ubongo wako unafanya kazi shap utagundua haraka sana
Huyu mtu kwa ndani hafurahii kama anavyosema
So patterns ukiziona unagundua huyu anawaza kwa namna nyingine kabisa tofauti na anachokionesha
Na kinachofanya jambo hili liwe interesting zaidi ni pale unapokuja kugundua kwamba baadae yule mtu anafanya kitu kinachothibitisha kile ulichohisi mwanzo
Swali la mjadala?👇
Hua najiuliza nimeisoma akili yake, au nilikuwa nimeisoma signals zake vizuri na kwa haraka?
Na kama kweli kuna watu wenye uwezo huu mkubwa wa kutambua kile ambacho wengine wanajaribu kuficha...
Uwezo huu unatokana na nini?
Ni intuition?
Ni experience?
Au kuna kitu kingine ambacho bado Labda wengi wetu hatujakifahamu kwa undani
Na kama kipo je ni kitu gani?
Nataka kusikia mawazo yenu🧠
Cc:
Marcostilone
ShesRise_1 ✋️