Je, kuna umuhimu wa kumposti mpenzi kwenye mitandao ya kijamii?

Hivi mkipostiana kwenye mitandao ndo ishara ya upendo? Ingawa utaratibu wa kila mahusiano au ndoa ni wa wale waliomo, lakini kwangu hii kanuni naiona kama ulimbukeni flani hivi.

Labda kama mnaishi kwa umaarufu (fame), yaani kipato chenu kinategemea publicity ya wapenzi, huenda!
 
Wawakilishi wetu na maoni yako kuhusu kumpost au kutompost mpenzi wako kwenye social platforms, cha ajabu wote wanalia humu kuwa single ni kama mtu anakupa ushauri wa kidaktari halafu yeye siyo daktari.
Leejay49 mshamba_hachekwi View attachment 2790936
AddText_10-24-08.19.27.jpg
 
Wana MMU kwema? Nikutana na hii mada sehemu, je kuna umuhimu wa kumposti mpenzi kwenye mitandao ya kijamii?

Baadhi ya wanaume wanasema kufanya hivi ni kuanika mambo yako bila sababu ya msingi hivyo hakuna haja, huku wanawake wamegawanyika katika makundi mawili, baadhi wakisema hawawezi kupost wapenzi wao kwa kuhofia kuibiwa na wengine wakisema kupost ni muhimu ili kuonesha uamifu wako, kama hujampost kokote ujue kuna mambo unafanya hutaki mwenzako ajue,

Kwenu wakuu, kuna haja na ulazima wa kumposti mpenzi kwenye mitandai ya kijamii?

Kuna umuhimu kama ukifanya hivyo ni sehemu ya furaha yako.
Lakini hakuna umuhimu ikiwa haimaanishi chochote kwako
 
Back
Top Bottom