NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Pole sana kwa kumpoteza rafiki yako, umenipa majonzi sana kwasababu umenikumbusha nilivyompoteza rafiki yangu mwaka 2010 sababu ya pumu, siwezi sahau hadi siku nitakayoingia kaburini.
Turudi kwenye mada;
Ndugu yangu, kuna muda ukifikiria sana kuhusu uwepo wa Mungu unaweza jikuta kwenye maumivu makali na kufuru zisizosameheka hasa unapokuwa unapitia changamoto zisizoisha! Mimi sijawahi kuwa na furaha ya kweli tokea mwaka 2013 hadi muda huu ninapoandika hapa, huwa nacheka, nakaa natizama movies, nk lakini ni kujipa moyo tu na kuendelea kujivika moyo wa ujasiri, unajua kwanini? Kwasababu mimi naamini sana katika uwepo wa Mungu na pia namuomba sana ila tokea mwaka 2013 hadi leo sijawai ona nafuu katika ninalopitia zaidi ni kwamba hali inazidi kuwa mbaya kila nionapo asubuhi mpya! Lakini sijawahi kuamka nikaacha kumshukuru Mungu kwa kunipatia zawadi ya pumzi kwa siku nyingine tena, japokuwa naona baadhi ya watu wakiponywa matatizo yao lakini mimi naomba na kutoa sadaka kwa miaka 10+ lakini hali inazidi kuwa mbaya.
Ninachojua ni kitu kimoja tu, kuanzia YESU mwenyewe, mtume MUHAMMAD, na hata wale wanafunzi 12, wote walipitia mateso makali japokuwa (kwa maandiko yasemavyo) walikuwa na ukaribu na MUNGU zaidi yetu. Na imani hiyo ndio msingi wangu unaonifanya hadi leo hii niendelee kumuomba MUNGU japokuwa hali yangu inaendelea kuwa mbaya, naamini hatakama nateseka ila si bado naamka asubuhi kwahiyo bado ni NEEMA kubwa.
Nathubutu kusema, nisingekuwa na haka KATONE ka imani, basi nisingekuwa hai leo! Kwasababu kwa ninayopitia ni ajabu siku naletewa taarifa kwamba rafiki yangu fulani kafariki, huwa nabaki kushangaa kwasababu nahisi kama aliyestahili kuwai kuondoka ni mimi na sio yeye ambae alikuwa mzima kiafya na mwenye nguvu za kutosha!
Yote kwa yote, hiastoria za maandiko ndio msingi wangu wa kuamini kwamba MUNGU yupo na ananisaidia sana despite ya haya yote ninayopitia. Hata wewe usikate tamaa ndugu yangu, ukiweza hata ule wakati ya pumzi yako ya mwisho endelea kusema tu kimoyo moyo ASANTE MUNGU, ASANTE MUNGU... haijalishi unaamini kama yupo au hayupo, hatujui tuendako!