Je, kuna Mungu? Kwanini aruhusu mateso makali duniani?

Achana na human made conceptions zote hizo zimemezwa na aspect moja na mind..

Na Mungu ni kila kitu including the mind
Mind ni nini?
Unaposema Mungu ni Kila kitu una maanisha nini?
Kule mwanzo ulisema ulitumia reasoning na meditation, hivi vitu vipo nje ya mind?
Kama mind ni Kila kitu, ,nature ni nini?
 
Mind the processing and functioning of the brain..

Huku soma vizuri nilisema ya kuwa nimefanya zile practices na reasoning ila zilinirudisha kwenye stillness na kujua uwepo wa Mungu.. Vitu hivyo vipo kwenye mind, ila vinasaidia kufikia utulivu wa hiyo mind

Mind sio kila kitu.. Sijasema hivyo.

Mungu ndio kila kitu.
 
Unajichanganya mwenyewe mpaka Sasa.
Hujui mind ni nini
Nature ni nini
Mungu ni nini
Huwezi Kutofautisha Budha mkuu na Yahweh.
Upo upo tu.
 
Unajichanganya mwenyewe mpaka Sasa.
Hujui mind ni nini
Nature ni nini
Mungu ni nini
Huwezi Kutoka Budha mkuu na Yahweh.
Upo upo tu.
Issue ni kuwa hakuna ajuae maana uhalisia usemekao sio wa kweli.. Ni ule unakuja na human conditioning..

So kamwe siwezi kuwa manipulated by another being.. Kwa sababu yeye a nadhani au kuhisi tofauti na mimi.. As long as it comes to man made concepts

Hiyo ni jela nyingine ambayo wengi hutumia ku manipulate wenzao.

Kama hauna hoja ni bora ukaacha ku attack mtu.. Na kingine swala la Mungu ni personal mtu akikupa mawazo yake ni yake..

Tuko hapa kusaidiana kurudi katika ukweli na sio vita baina ya watu binafsi.
 
Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?

Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.

Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?

NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Ukishakubali Mungu yupo.
Ukishakubali kwamba Mungu anawapenda viumbe wake.
Ukishakubali kwamba Uwezo wa Mungu upo nje ya uwezo wa binadamu.
Basi "mabaya" yanayotokea duniani ni rahisi kuyaona ameyaruhusu kwa nia njema. Ni mfano kama mama unayempeleka mtoto wako achomwe sindano ya kutibu malaria. Mtoto analia kwa sauti ya maumivu lakini mama anamshikilia kwa nguvu asijitikise ili shughuli imalizike. Mtoto haelewi kwa nini anapata mateso hayo. Mama ana nia njema. Mama anataka kuokoa maisha ya mtoto wake.
 
Issue ni kuwa hakuna ajuae maana uhalisia usemekao sio wa kweli.. Ni ule unakuja na human conditioning..

So kamwe siwezi kuwa manipulated by another being.. Kwa sababu yeye a nadhani au kuhisi tofauti na mimi.. As long as it comes to man made concepts

Hiyo ni jela nyingine ambayo wengi hutumia ku manipulate wenzao.

Kama hauna hoja ni bora ukaacha ku attack mtu.. Na kingine swala la Mungu ni personal mtu akikupa mawazo yake ni yake..

Tuko hapa kusaidiana kurudi katika ukweli na sio vita baina ya watu binafsi.
Maelezo ni Yako ikiwa utayatunza kichwani mwako.
Ila ukiyaleta jamii forum si yako tena.

Kama hayo mawazo yote ni human concepts then kubali tu kama wengine.

Hakuna Mungu simple
Unatumia reasoning na meditation in a wrong way
 
Sikusema kuwa ujimilikishe mawazo yangu, nilisema either ukubali au ukatae hilo ni jukumu lako maana maelezo ya kusemekana haya akisi uhalisia kamili

Siwezi kukubali maana hayanifanyi nielewe ujinga ambao wengine wamemezeshwa..

Basi kama unahisi reasoning na meditation Zina namna bora ya kutumika kazitumie wewe Kadri uwezavyo.. Na uhisivyo ni sawa kutumika

Bado unakuja na mentality ya ku attacck mtu, that's your problem not mine
 
Ukishakubali Mungu yupo.
Ukishakubali kwamba Mungu anawapenda viumbe wake.
Ukishakubali kwamba Uwezo wa Mungu upo nje ya uwezo wa binadamu.
Basi "mabaya" yanayotokea duniani ni rahisi kuyaona ameyaruhusu kwa nia njema. Ni mfano kama mama unayempeleka mtoto wako achomwe sindano ya kutibu malaria. Mtoto analia kwa sauti ya maumivu lakini mama anamshikilia kwa nguvu asijitikise ili shughuli imalizike. Mtoto haelewi kwa nini anapata mateso hayo. Mama ana nia njema. Mama anataka kuokoa maisha ya mtoto wake.
Nia njema kwa watoto wadogo kubakwa na kuugua cancer ?

Nia njema ya watoto wa Gaza kuuwawa vitani ni ipi?
 
Hiyo ni pepo ambayo wataingia watakaofaulu.
Kinyume chake wewe ungetaka mijambazi,mafisadi,wauwaji,watekaji wote waishi maisha kama peponi kitu ambacho sio fair.
I don't know why you dumb theists can't reason properly.
Kwa kuanzia Mimi sitaki majambazi, mafisadi, wauaji na watekaji wawepo kabisa, kuwepo ni tatizo na swali ni kwa nini mwenye nguvu zote aruhusu wawepo? Kwa nini asizuie wasiwepo? Kwa nini aruhusu njaa, magonjwa, majanga, vita na vifo??
 
Yesu mwenyewe ambae Mungu alimtangaza kama mwanae mpendwa Mungu aliruhusu apitie maumivu makali mateso makali na alikua na uwezo wakukiondoa kikombe cha mateso,mnaosena Mungu kama yupo kwanini anaacha watu waumie wabakwe wauliwe hiyo pekee yake haiweki kuaminisha Mungu hayupo
 
1 Samuel 15:3- "Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."

Kumbukumbu la Torati 20:16- "Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu chochote kipumzikacho"

Kwa nini mungu wa Israel alikuwa anaamuru wototo, wanawake na wanyama wauwawe vitani ?
Kwa nini alikuwa anaamuru WaIsrael wafanye mauaji ya kimbari(genocide) ?
 
I don't know why you dumb theists can't reason properly.
Kwa kuanzia Mimi sitaki majambazi, mafisadi, wauaji na watekaji wawepo kabisa, kuwepo ni tatizo na swali ni kwa nini mwenye nguvu zote aruhusu wawepo? Kwa nini asizuie wasiwepo? Kwa nini aruhusu njaa, magonjwa, majanga, vita na vifo??
Hayo maswali yako hayapaswi kuulizwa hata na mtoto mdogo mwenye akili timamu.
Njaa isingekuwepo wewe ungeijulia wapi?
Hiyo ni mitihani tuliyopewa kwa hiyo unapaswa kutumia akili yako uliyozawadiwa kuikwepa.
Yaani swali lako halinq utofauti na kumuuliza mwalimu"Mwalimu kama wewe una nia nzuri na ufaulu wa wanafunzi wako kwa nini unatupatia mtihani,ni kwa nini usiandike kwenye ripoti kwamba darasa lote tumefaulu"
 
Watu wengi wanaamini tu lakini hawajui kama Mungu yupo. Unapotazama ulimwengu na vilivyomo, utajiuliza pia hivi vitu vilitokea wapi? Ni wazi kuna nguvu fulani au kiumbe kinachohusika na uwepo wetu na dunia yenyewe. Huenda ndio Mungu. Na labda lengo lake ilikuwa dunia iwepo tu. Hizi dini ndio zimetufanya tutarajie Mungu atufanyie mambo fulani au miujiza ambayo labda sio shida zake. Nawaza tu.
 
Hayo maswali yako hayapaswi kuulizwa hata na mtoto mdogo mwenye akili timamu.
Njaa isingekuwepo wewe ungeijulia wapi?
Hiyo ni mitihani tuliyopewa kwa hiyo unapaswa kutumia akili yako uliyozawadiwa kuikwepa.
Yaani swali lako halinq utofauti na kumuuliza mwalimu"Mwalimu kama wewe una nia nzuri na ufaulu wa wanafunzi wako kwa nini unatupatia mtihani,ni kwa nini usiandike kwenye ripoti kwamba darasa lote tumefaulu"
Kwa sababu Mwalimu wa darasani hana akili za kujua kila kitu kuhusu wanafunzi wake ndio maana inabidi atafute njia mbalimbali za kuwapima, pia mwalimu wa darasani hana uwezo wa kuwapa wanafunzi wake akili, pia mwalimu wa darasani anaweza kuwa ni muovu katili anayefurahia wanafunzi kufeli.

Ni ujinga kumfananisha mwalimu wa darasani na kiumbe anayesemewa anajua kila kitu wakati wote, ana nguvu zote na ana upendo mkuu.
 
Hayo masuala ni ya Kiimani zaidi, kama vile mtu asiye na Kazi anavyoweza kuwa na imani kuwa siku moja atapata kazi, basi pia kuhusu Mungu watu Wana imani na kuamini kuwa yupo hata kama hawatakuwa na uwezo wa kukuthibitishia lakini ndiyo imani yake ilivyo, it's all about faith
 
Mim
Nia njema kwa watoto wadogo kubakwa na kuugua cancer ?

Nia njema ya watoto wa Gaza kuuwawa vitani ni ipi?
Kwa akili yangu siwezi kuona nia njema kwa majanga kama hayo.
Lakini tukirudi kwenye misingi ya hoja, mtoto anayedungwa sindano hawezi kuona nia njema katika mateso anayopitia.
Mtoto haelewi na hana uwezo wa kuelewa kwa nini mama anayempenda ghafla anaruhusu watu wamuumize bila sababu.
 
Acheni kumdogosha mungu wenu kumfanya awe na nguvu sawa na binadamu.

Mtoto anachomwa sindano kwa sababu ndio last option inayokuwepo kama binadamu tungekuwa na nguvu za kuamuru mtoto apone bila sindano, oparesheni au dawa zozote tungefanya hivyo ila hatuna huo uwezo, mungu wa Abraham anasemwa ana huo uwezo tena na wa zaidi hata kuzuia magonjwa kabisa.

Wewe ukienda hospitali halafu daktari akasema una cancer inabidi ukatwe mguu baadaye ukaja kugundua daktari alikuwa ana dawa au namna ya kukuponya bila mguu kukatwa na ukawa sawa kabisa utajisikiaje kuhusu huyo daktari??
 
Kwa sababu Mwalimu wa darasani hana akili za kujua kila kitu kuhusu wanafunzi wake ndio maana inabidi atafute njia mbalimbali za kuwapima, pia mwalimu wa darasani hana uwezo wa kuwapa wanafunzi wake akili, pia mwalimu wa darasani anaweza kuwa ni muovu katili anayefurahia wanafunzi kufeli.

Ni ujinga kumfananisha mwalimu wa darasani na kiumbe anayesemewa anajua kila kitu wakati wote, ana nguvu zote na ana upendo mkuu.
Kama mwalimu wa darasani hawezi kujua uwezo wa wanafunzi wake je ni nani huyo mwenye uwezo wa kujua akili za binadamu bila kuwapima?
 
Back
Top Bottom