Je, Kinachomponza Mbowe ni Anasa?

Je, Kinachomponza Mbowe ni Anasa?

Status
Not open for further replies.
....Mbowe aligoma kulipa kiasi kilichotajwa, na wakati wote aliweka bayana kiasi ambacho alikuwa tayari kulipa wakati wowote kama mahakama ingeelekeza. Na alikilipa, the rest ni yada yada ya Rostam Aziz na Balille. Tusubirini Mbowe ajitokeze na kuanika nyaraka zote ndipo Rostam atakapoaibika

Dada Asha,
Huu ni mkopo ambao ulitolewa kwa mkataba na naamini Mheshimiwa na timu yake walipitia kila kipengele na kukielewa kwa undani.Interest rate ya 30% ni kubwa lakini aliikubali na kama angekuwa mjanja kwa rate hiyo angemaliza kulipa hilo deni within the 6 years agreed terms but hadi sasa ni miaka 18, unategemea hilo deni lisikue? Na kwani Mbowe ni ani hadi awe na uwezo wa ku dictate kiasi ambacho anataka kulipa?

For the sake of Chadema, wanachama wenye uchungu hapa mngetakiwa sasa hivi mumshinikize Mwenyekiti wenu atoe tamko kuhusu hili suala au aachie ngazi mapema, its going to be a shame kama CCM itaendelea kuwa madarakani in 2010 and more shame kama hili litatokea kwa kuwa tu watu wanamuone haya Mbowe( au sijui ni kumuogopa? )
 
Kana Kansungu

Wewe ni kati ya watu wanaoheshimika humu kwa kuchambua kabla ya kusema. Hebu kasome kidogo mtiririko wa matukio kuhusu suala hili utaelewa kwa nini Mbowe aligoma kulipa kiasi kilichotajwa, na wakati wote aliweka bayana kiasi ambacho alikuwa tayari kulipa wakati wowote kama mahakama ingeelekeza. Na alikilipa, the rest ni yada yada ya Rostam Aziz na Balille. Tusubirini Mbowe ajitokeze na kuanika nyaraka zote ndipo Rostam atakapoaibika. We unadhani kwani nini NSSF kama taasisi miaka yote hiyo wameuchuna? Wanajua kinachoendelea

Asha

Jamani alipe tu.kama hili la miaka kumi na nane halipi vipi madeni ya helikopter?

ina maana Mbowe akimkopa mtu leo hii analipa baada ya miaka kumi na nane?au alinyuti baada ya kuona shirika limebadilika jina toka AKIBA KWENDA NSSF?

MWANKIJIJJI TANGAZA MCHANGO ILI HESHIMA YA MWENYEKITI IRUDI.AKIFIKA MAHAKAMANI NA MACHO YAKE YA KUMCHUZI ITAKUWA AIBU KUBWA.

NA HUKO HULL UNIVERSITY INAWEZEKANA KAKIMBIA NA DENI LAO LA MWAKA WA KWANZA.INAWEZEKANA NI KATABIA KAKE HUYU JAMBAWAZI.
 
Dada Asha,
Huu ni mkopo ambao ulitolewa kwa mkataba na naamini Mheshimiwa na timu yake walipitia kila kipengele na kukielewa kwa undani.Interest rate ya 30% ni kubwa lakini aliikubali na kama angekuwa mjanja kwa rate hiyo angemaliza kulipa hilo deni within the 6 years agreed terms but hadi sasa ni miaka 18, unategemea hilo deni lisikue? Na kwani Mbowe ni ani hadi awe na uwezo wa ku dictate kiasi ambacho anataka kulipa?

KKN,

kesi imekuwa mahakamani kwa muda sasa na hakuna kitu NSSF wamekuja nacho. Hii issue inabidi iundiwe tume ya bunge na sio swala la Mbowe kujieleza. Inabidi tume ya bunge ichunguze yote kuanzia waliokopa NSSF, walioiba, na ambao "wamekopa" bila maelezo kama MKullo na wenzake.

For the sake of Chadema, wanachama wenye uchungu hapa mngetakiwa sasa hivi mumshinikize Mwenyekiti wenu atoe tamko kuhusu hili suala au aachie ngazi mapema, its going to be a shame kama CCM itaendelea kuwa madarakani in 2010 and more shame kama hili litatokea kwa kuwa tu watu wanamuone haya Mbowe( au sijui ni kumuogopa? )

Hii issue sio for the sake ya Chadema mkuu, hii ni issue ambayo ni for the sake of the country. Kuna habari kuwa hata KIkwete ni mmoja waliofaidika na pesa za MKulloo alizochota NSSF. Iundwe kamati huru ya bunge kuchunguza hili na haya ya uchaguzi wa 2010 yatajulikana.
 
Jamani alipe tu.kama hili la miaka kumi na nane halipi vipi madeni ya helikopter?

ina maana Mbowe akimkopa mtu leo hii analipa baada ya miaka kumi na nane?au alinyuti baada ya kuona shirika limebadilika jina toka AKIBA KWENDA NSSF?

.......

Unda tume huru ya bunge kuchunguza hili kama bosi wako Rostam na wezi wenzake kina Mkullo wana ubavu huu. zaidi ya hapo nenda kachezee makopo maana naona vilio vyako havijaisha
 
Binafsi sijasoma article inayozunguzia suala zima la mikopo ya Bwana Mbowe. Lakini sioni kosa kwa mtanzania yeyote kukopa kutoka kwenye vyombo vyetu vya kifedha. Isitoshe hayo ndio maendeleo yenyewe. Hususan, watanzania watakapojua umuhimu wa kutumia rasilimali walizo nazo kama rehani dhidi ya mikopo ya benki.
Hata kama Mbowe hajalipa, au, ana matatizo katika ulipaji, hilo ni suala kati yake na vyombo vya kifedha vinavyomdai.
Kuwa na Range,Jumba la kifahari n.k huo ni uamuzi wake yeye na familia yake!
 
Kadhalika deni lolote likifika kiasi fulani, au chombo kilichokukpesha kikali'classify' kama bad debt, It is Ok to negotiate how much you are willing to service. Doing this does not mean dictating.Ni taratibu za kifedha tu!
 
Binafsi sijasoma article inayozunguzia suala zima la mikopo ya Bwana Mbowe. Lakini sioni kosa kwa mtanzania yeyote kukopa kutoka kwenye vyombo vyetu vya kifedha. Isitoshe hayo ndio maendeleo yenyewe. Hususan, watanzania watakapojua umuhimu wa kutumia rasilimali walizo nazo kama rehani dhidi ya mikopo ya benki.
Hata kama Mbowe hajalipa, au, ana matatizo katika ulipaji, hilo ni suala kati yake na vyombo vya kifedha vinavyomdai.
Kuwa na Range,Jumba la kifahari n.k huo ni uamuzi wake yeye na familia yake!

Mbowe hajashindwa kulipa au kukataa kulipa, wao kina Mkullo walikuwa wanageuza terms za deni (soma post ya gamba la nyoka) na ikabidi kesi iende mahakamani.

Kama ccm wanazani kuwa wana case hapa basi inabidi waendeleze kesi hii mahakamani au waunde tume huru ya bunge na kisha pesa zote zilizokopwa toka NSSF zifuatiliwe kujulikana zilikoishia.

Mimi hapa naanza kuomba kichwa cha Mkullo (waziri wa fedha wa Kikwete)!
 
Binafsi sijasoma article inayozunguzia suala zima la mikopo ya Bwana Mbowe. Lakini sioni kosa kwa mtanzania yeyote kukopa kutoka kwenye vyombo vyetu vya kifedha. Isitoshe hayo ndio maendeleo yenyewe. Hususan, watanzania watakapojua umuhimu wa kutumia rasilimali walizo nazo kama rehani dhidi ya mikopo ya benki.
Hata kama Mbowe hajalipa, au, ana matatizo katika ulipaji, hilo ni suala kati yake na vyombo vya kifedha vinavyomdai.
Kuwa na Range,Jumba la kifahari n.k huo ni uamuzi wake yeye na familia yake!

Mpendwa,
Kaisome story yenyewe kwenye page ya tatu, ni muhimu usome kwanza kabla hujatoa mchango wako hapa vinginevyo ni kama unaongelea jamabo usilolijua.
 
halafu hii thread si ilishaanzishwa
hebu cheki hii http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=10852

Mod merge hizi threads

Mkuu,

walioanzisha hizi thread walitaka zifutwe au ziunganishwe ili waanze kulilia maziwa kama kawaida yao. Sasa hii thread itakuwa ni wito kwa serikali kufuatilia masuala ya pesa ya NSSF ili ijulikane nini kinaendelea huko!

Kamati huru ya bunge itakuwa ni kitu muhimu sana cha kuanza nacho kwa muda huu ili ijulikane Mkullo na Kikwete wamefaidika nini katika pesa za NSSF.

Waliokopa NSSF wote (ikiwemo Mbowe) inabidi wajulishe kamati kuwa ni kiasi gani kimekopeshwa na vipi na malipo yamefanyika kiasi gani so far!

tik tak tik tak.....
 
Unda tume huru ya bunge kuchunguza hili kama bosi wako Rostam na wezi wenzake kina Mkullo wana ubavu huu. zaidi ya hapo nenda kachezee makopo maana naona vilio vyako havijaisha

unafikiri kila mtu ananunuliwa kama wewe? MBOWE KATUPA DOLA ELFU MBILI ZA KUFUNGUA KLH WEBSITE UNAMUONA KAMA MUNGU?

MWANAKIJIJI UNAJIABISHA SANA UKO NCHI ZA WATU UNAWEZA KUJIKUTA UKO TIMU YA ELTON JOHN KWA KUOMBAOMBA.
 
You will know their true colours soon as they open their mouths.
 
So far,

kwa mara ya pili mfululizo, umethibitisha kuwa huna hoja bali vilio na udaku tu. So kama kawaida, mada za ufisadi wa ccm zinaendelea kujadiliwa kwa sasa na wewe endeleza vilio vyako kama kawaida yako!
 
You will know their true colours soon as they open their mouths.

yaani we acha tu!

Hawakujua gharika inayowasubiria hapa.
Wamekaa vikao kina wakajadili hili na kudhani kuwa wana hoja bila kujua kuwa hii issue ya NSSF inamgusa Kikwete na Mkullo na sasa wameaibika wameanza kulilia maziwa kama kawaida zao wakiishiwa hoja.
 
unafikiri kila mtu ananunuliwa kama wewe? MBOWE KATUPA DOLA ELFU MBILI ZA KUFUNGUA KLH WEBSITE UNAMUONA KAMA MUNGU?

MWANAKIJIJI UNAJIABISHA SANA UKO NCHI ZA WATU UNAWEZA KUJIKUTA UKO TIMU YA ELTON JOHN KWA KUOMBAOMBA.

Wooow guys! its getting nasty and personal now, tubishane kwa hoja tu, hakuna haja ya matusi. I better sign off now!
 
unafikiri kila mtu ananunuliwa kama wewe? MBOWE KATUPA DOLA ELFU MBILI ZA KUFUNGUA KLH WEBSITE UNAMUONA KAMA MUNGU?

MWANAKIJIJI UNAJIABISHA SANA UKO NCHI ZA WATU UNAWEZA KUJIKUTA UKO TIMU YA ELTON JOHN KWA KUOMBAOMBA.

Chinga hivi Mbowe ni Mtani wako? Mara zote Breaking News za Mbowe anazijua sana chinga.
 
Kama kuna kosa kubwa mabalo Nyerere alililea ni lile la dhana potofu ya kuwa Utajiri ni sumu (Ubeari ni Unyama)!

Watanzania tumeendeleea kuwa vipofu na wagumu kukubali kuwa hata misahafu yazungumzia kuhusu jamee na falme zilivyokuwa na Utajiri. Tulichoshupalia kutoka misahafu na hasa biblia ni lile la yesu kuonyesha kuwa maskini ana nafasi kubwa kwenda Mbinguni kuliko tajiri. Hivyo basi kwa mafunzo ya kidini na itiadi tulizokuwa nazo za kijamaa zinatufanya tuhofie kuwa na mali, kuhofia kuwa matajiri eti tutaungua jehanamu.

Masaki umezungumzia kuwa Mbowe kuwa na kuishi kitajiri huku wananchi wanakufa na malaria, sijui ulitaka Mbowe aishi kimasikini au agawanye utajiri wake kwa kila mtu kwa kutoa chloroquine au chandarua?

Mbowe kakopa pesa, kaweka gumba na sahihi katika mkataba alipokopa. je kukopa ni uhalifu? je kuwa na mali au kuishi kwa fahari ni kosa la jinai? kwa mujibu wa katiba na vipengele vya sheria gani?

Mnaodai kuwa Mbowe kafeli elimu, sawa kafeli, yeye ni wa kwanza? Mnaodai kuwa mbowe anaishi maisha ya Anasa, je yeye ni wa kwanza? Mnaomuita mbowe mwizi, kaiba wapi?

Kwa wale mnaotuhumiwa kuwa makuwadi wa mafisadi, msifananishe mtu kukopa na mtu kuiba au kujipatia pesa kwa njia a udanganyifu!

mafisadi wenu walitengeneza kampuni hewa na kujichotea fedha; Uhujumu na Wizi! Mbowe kakopa, Lowassa kazembea kampuni hewa ikaingingia nchini na kuhujumu je mambo haya yanafanana?

Ni mawazo ya kidumavu na ambayo yanaturudisha nyuma kwa watu kuona kuwa kila mfanyabiashara mwenye mali ambaye kapata halali na kwa jashi lake, basi twamuona mwovu au fidhuli.

Ikiwa kuna mmoja wenu ana ushahidi kuwa Mbowe alijipatia utajiri wake kwa kuiba au kuhujumu, leteni huo ushahidi.

Hili la NPF-NSSF kutoa mkopo tayari mshatamka kuwa ni mkopo. ikiwa Mbowe atashindwa kulipa, kitakachomsibu kikubwa ni kufilisiwa mali za kampuni na si mali binafsi.

Hao mafisadi wenu wameiba na kujipatia fedha kwa udanganyifu BOT kupitia EPA. Waliosafi na wakopaji wazembe kama Mbowe walikwenda BOT wakakopa zile pesa za CIS kutoka Japan.

People! get your facts together!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom