Je, Kinachomponza Mbowe ni Anasa?

Status
Not open for further replies.

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Mimi nadahani hapa suala si kwamba eti mtu yeyote ambaye hayuko madarakani kwa sasa basi yeye hana "elements" za ufisadi, la hasha! Ufisadi (greed) ni tabia binafsi ya mtu na inaweza kuonekana hata kama hajaiba mali ya umma.

Viongozi wa vyama vya upinzani tunaweza kuhoji tabia zao kutokana na maisha wanayoishi sasa na kugundua yupi mwenye sifa za ufisadi. Ukiona mtu anapenda sana kujilimbikizia mali basi huyo siku akipata nafasi serikalini ataiba pesa ya umma mpaka mtakoma. Tena anaweza hata kubadili katiba ya nchi ili atawale milele. Take my words!
naona KIngunge Mwiru angejieleza vizuri kuliko wewe! rudi chuoni kule kigamboni ufundishwe propaganda maana so far unaongea pumba tupu hapa!
 
Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,596
Points
2,000

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,596 2,000
Hicho ni chama kilichojaa mazingaombwe na watabiri wa kila aina.Hii nchi inaongozwa kimazingaombwe mazingaombwe tu,leo mara leta kuku mweupe,kesho leta vifaranga vya Bundi mwekundu, halafu tuinainua uchumi wetu,tuingie kwenye shirikisho.Jamani,haya mazingaombwe hayana maana.Tuishi maisha ya kawaida tu na tuongoze nchi kama wananchi wanavyotegemea muwaongoze na si kupiga Ramli

Labda pia watabiri wao wa ndani wanaona chama kitaporomoka ndio maana kila mtu ankufa na chake!
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Hicho ni chama kilichojaa mazingaombwe na watabiri wa kila aina.Hii nchi inaongozwa kimazingaombwe mazingaombwe tu,leo mara leta kuku mweupe,kesho leta vifaranga vya Bundi mwekundu, halafu tuinainua uchumi wetu,tuingie kwenye shirikisho.Jamani,haya mazingaombwe hayana maana.Tuishi maisha ya kawaida tu na tuongoze nchi kama wananchi wanavyotegemea muwaongoze na si kupiga Ramli

Labda pia watabiri wao wa ndani wanaona chama kitaporomoka ndio maana kila mtu ankufa na chake!
mhhh.. kwi kwi kwi kwi...

yaani hapa sina mbavu jamani.... huyu masaki naona siku hizi kawa shehe yahya kwa kufanya utabiri... mwisho ataungana na Lowasa kuleta watabiri wa mvua ooooppppsss watengeneza mvua toka sijui monduli au wapi kule!
 
NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2007
Messages
560
Points
0

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2007
560 0
Hebu watuletee hiyo habari ya Rai tuidadavue! WanaCHADEMA walishawahi kusema hapa kuwa Mbowe aliwahi kukupa milioni 15 wakati huo ikiwa sijui nini chini ya Mkullo sasa ni NSSF toka mwaka 1990. Wakashindwana terms of repayment wakapelekana mahakamani. Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza CCM walianza kuitumia kesi hii kisiasa toka miaka hiyo wakimtumia jaji Manento. Wakati wote Mbowe kupitia wakurugenzi wengine wamekuwa wakiweka bayana kuwa hawana shida ya kulipa, ila hawawezi kulipa kiwango cha zaidi ya ambacho anawajibika kisheria. Na amesisitiza yuko tayari kusimamia haki yake!. Sasa wewe Balille na swahiba wako Rostam Aziz waliokutuma; tuelezeni, Mbowe amekopa lini bilioni 1.2 NSSF? Na hata kama angekopa, kuna ubaya gani? Mnadhani kwa kurusha matope kwa wapinzani ndio mtajisaficha kwa kashfa yenu ya EPA na Richmonduli?

Asha

ASHA, HABARI YENYEWE NAONA NDO HII HAPA

13.03.2008 0947 EAT

Mbowe aifilisi NSSF
::Adaiwa milioni 1200, hataki kulipa
::Atumia sheria kukwepa asifungwe
::Adai iliyokopa ni kampuni si yeye

na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakalia kiasi kikubwa cha fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kukataa kulipa deni alilokopa.

Mbowe anadaiwa wastani wa sh milioni 1200 (sh bilioni 1.2), kutokana na deni alilochukua mwaka 1990 kwa nia ya kufanya upanuzi wa Mbowe Hotel ya jijini Dar es Salaam, maarufu kama Bilcanas.

Kwa kutumia mamilioni aliyokopa kutoka NSSF Machi 10, mwaka 1990, Mbowe aliweza kupanua Mbowe Hotel kwa kujenga mgahawa wa Hard Rock, kumbi za Bilcanas, Much More na Sugar Mama, ambazo amekuwa azitumia kwa ajili ya biashara tangu wakati huo.

Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa deni la mkopo huo aliouchukua kwa kutiliana saini kati yake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuwa NSSF, sasa limekua na kufikia zaidi ya sh milioni 1200. Deni hili linatokana na mkopo aliouchukua na riba inayotokana na deni hilo.

Wakati wa kuchukua mkopo huo NPF (wakati huo) iliwakilishwa na Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, huku Mbowe Hotel ikiwakilishwa Mbowe mwenyewe aliyetia saini. Pande zote mbili zilikuwa na mwakilishi mmoja. Mkulo kwa sasa ndiye Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo kati ya Mbowe na NSSF, ambayo ilichukua majukumu ya NPF, Mbowe Hotel ilikopeshwa sh milioni 15, mwaka 1990. Ibara ya 5, ya Mkataba wa Mkopo kati ya Mbowe Hotel na NSSF yenye vifungu 5.01, 5.02 na 5.03, iliweka bayana kuwa riba ya mkopo huo ilikuwa asilimia 31, na kwamba kila mwaka iwapo riba isingelipwa kwa wakati nayo ingetozwa riba ya asilimia 31.

Kifungu cha 6.01 na 6.02 cha mkataba wa mkopo huo kati ya Mbowe na NSSF vinaeleza kuwa Mbowe Hotel ilitakiwa kulipa deni hilo kwa mikupuo sawa mitano katika kipindi cha miaka sita. Mwaka wa kwanza wa mkopo Mbowe Hotel haikutakiwa kulipa kitu kwa nia ya kuipa fursa ya kujiimarisha katika biashara kwa mwaka wa kwanza.

Malipo hayo yalipaswa kufanyika kila ifikapo Desemba 31, kuanzia mwaka 1991, ambapo kila mwezi alistahili kulipa sh 3,000,000 kama deni la msingi na riba ya asilimia 31 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Manase A. Mbowe, Freeman Aikaeli Mbowe na Dk. Lilian Mtei Mbowe, kwa sababu wanazozijua wao waliamua kuacha kulipa deni hilo bila mawasiliano ya aina yoyote na NSSF wala juhudi za wazi za kuonyesha nia ya kulipa hadi mwaka 1993, walipoamua kulipa sh 3,000,000 kati ya deni lote.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, hadi mwaka 1993, wakurugenzi hao walistahili kuwa wamelipa wastani wa sh milioni 9,000,000 katika deni la msingi, lakini walikaa kimya hali iliyolitia wasiwasi shirika la NSSF.

Baada ya kutoa malipo ya sh 3,000,000, wakurugenzi hao walikaa kimya na ilipofika Septemba 1996, NSSF iliamua kufungua kesi Mahakama Kuu. Kesi hiyo ya madai No. 277 ya mwaka 1996, ilikuwa ikidai Mkopaji alipe deni la msingi sh milioni 12 zilizokuwa zimesalia pamoja na riba.

Hatua hii iliwafanya wakurugenzi wa Mbowe Hotel kuomba suala hilo walimalize nje ya Mahakama. Hata hivyo, hawakuendelea kulipa hadi mwaka 1998, walipopewa tishio la kufungwa jela ndipo waliamua kulipa kwa mkupuo sh milioni 12.

Hadi wanatoa malipo hayo, deni lilikwishakuwa na kufikia wastani wa sh milioni 145.38, na kimsingi makubaliano ilikuwa ni kwamba deni hilo lingelipwa katika muda wa miezi 24 tangua tarehe ya makubaliano.

Hata hivyo, Mbowe na wakurugenzi wenzake waliamua kutoendelea kulipa deni hilo badala yake wakaamua nao kuchukua mkondo wa kisheria kwa kutumia wahasibu kukokotoa tena hesabu za riba, bila mawasilianao na NSSF, na kisha wakachagua kiasi wanachotaka kulipa wao.

Mbowe Hotel ikitumia kampuni ya uwakili ya Nyange, Ringia & Co., walifanya kazi ya kuwasiliana na wahasibu mbalimbali kisha kuwasiliana moja kwa moja na wakili wa NSSF, Ademba Gomba, kutaka deni la riba lipunguzwe.

Mgogoro na mvutano kati ya Mbowe Hotel uliendelea, huku riba ya deni nayo ikizidi kuongezeka na ilipofika Oktoba 11, 2002 Meneja wa Fedha wa Bilcanas Group Inc, Godbless Naftal, kupitia barua yake yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL02/02/01, alikokotoa hesabu na kutaka wakurugenzi wa Mbowe Hotel walipe wastani wa sh 31,959,369.86, kwa maelezo kuwa kanuni iliyotumiwa kukokotoa riba ilikosewa.

Januari 16, 2003 NSSF kupitia kwa Mussa S. A. kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alimjibu Naftal kwa barua yenye Kumb. No. NSSF/LA/F.131/10/89/135, akimweleza kuwa NSSF imekataa mapendekezo yake (Naftal) na hivyo wanapaswa kulipa deni lote kwa mujibu wa hukumu ya za Mahakama Kuu za mwaka 1999 na 2001.

NSSF na Mbowe Hotel waliendelea kupigana ngwala mahakamani na kwenye bodi za usuluhishi hadi ilipofika Oktoba, 2006 ambapo Jaji Manento alihukumu wakurugenzi wa Mbowe Hotel watiwe mbaroni na kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kulipa deni lao.

Wakili wa Mbowe Hotel, Herbert Nyange, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufaa hati ya kiapo ambayo muhuri wake umegonjwa Oktoba 30, 2006 akipinga wakurugenzi wa Mbowe Hotel kukamatwa kwa maelezo kuwa Mahakama Kuu ilikwenda nje ya mipaka kisheria kwa kutaka wakurugenzi wakamatwe.

“Uamuzi wa amri ya kukamatwa kwa walalamikaji (wakurugenzi wa Mbowe Hotel) ulifikiwa kwa misingi ya wazi ya uvunjaji wa kanuni juu ya wajibu wa wakurugenzi dhidi ya deni au uamuzi dhidi ya shirika, hivyo ni kinyume na sheria,” alisema Nyange katika barua hiyo ya kupingwa kukamatwa kwa akina Mbowe.

Hata hivyo, kutokana na Mbowe kuona mambo yanaendelea kuchacha, Desemba 14, mwaka 2006, mmoja wa wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Dk. Lilian Mtei Mbowe, aliamua kutoa malipo ya wastani wa sh milioni 50 kwa NSSF kwa hundi mba 298492, iliyoambatana na barua yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL06/01, huku akitaka warejee kwenye meza ya majadiliano badala ya kufungwa jela.

Barua hiyo pia iliomba NSSF irejee barua ya Kampuni ya Ushauri wa Fedha ya Morgan cKlien Associates iliyoteuliwa na Mbowe mwaka 2004 kushiriki majadiliano na usuluhishi juu ya jinsi ya kulipa deni hilo.

Kampuni hiyo iliyokuwa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Hubert Mengi, ilitoa maelezo mengi yenye kuonyesha kwa nini Mbowe Hotel ilishindwa kulipa deni lake kwa wakati. Anasema katiak moja ya vielelezo kuwa fedha zilipotolewa na NSSF mwaka 1990, nchini Tanzania hakukuwapo vifaa vya ujenzi.Mengi anaeleza kuwa Mbowe Hotel walilazimika kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi, na lilijitokeza tatizo lingine kwamba benki nchini hazikuwa na fedha za kigeni, hivyo Mbowe Hotel ililazimika kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo za kigeni.

Kwa maelezo hayo, anasema Mbowe Hotel walichelewa kupata vifaa na mradi ukashindwa kukamilika kwa wakati hali iliyosababisha wakurugenzi wake washindwe kulipa deni hilo kwani walikuwa hawafanyi biashara.

Baada ya mivutano yote hiyo, Mbowe Hotel wamealikwa kwenye NSSF kujadili jinsi ya kulipa deni hilo linaloendelea kukua lakini hadi jana vyanzo vyetu kutoka NSSF vilionyesha kuwa wakurugenzi wa Mbowe Hotel wameamua kukaa kimya.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini.

© Habari Corporation Ltd
All rights reserved
http://www.newhabari.com/rai/habari.php?id=479&section=habari
 
Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Messages
1,601
Points
2,000

Congo

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2008
1,601 2,000
Sasa tujiandae, vita ya wakubwa kwa wakubwa ndio imeanza. Ingawa imeanzia pembeni kwa Mbowe lakini inakuja polepole, wanaolengwa watafikiwa tu.
 
Tulamanya

Senior Member
Joined
Oct 18, 2007
Messages
128
Points
0

Tulamanya

Senior Member
Joined Oct 18, 2007
128 0
Masaki,

Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri! Wewe kuwa na access na computer au simu unayo tumia kufanya masiliano hapa, tayari inaonyesha uwezo au kipato chako ni juu ukilinganisha na watanzania walio wengi wanaoshindia mlo mmoja kwa siku! Je, tukuite fisadi kwa kutowajali watanzania wengi wanao ishi kwa mlo mmoja! Ina maana ukipewa madaraka utakua fisadi pia?

Jaribu kufikiria kidogo ndugu yangu, utajiri is a relative term!

Wewe kijijini ulikotoka wanakuita tajiri wa kutupwa japukuwa huwasaidii hata cent moja? Do you know that?
 
Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2006
Messages
2,124
Points
1,500

Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2006
2,124 1,500
Naomba mnisamehe kama lugha yangu itakuwa si ya kistaarabu.Mnaowavuta na kuwalea hawa vibaraka wa mafisadi ni nyie mnaorefusha MADA ZINAZOONEKANA KABISA KUANZISHWA KAMA UTEKELEZAJI WA ASSIGNMENTS FLANI (za mafisadi).Busara nyepesi tu inaonyesha mtu sober akibishana na mlevi wote wanaonekana walevi.KWANI KUNA UGUMU GANI KUPUUZA?Reactions zenu kwa upuuzi wao zinawasafishia CV kwa hao wanaowatuma (it's like pay-per-click kwa mtu anayetuma spams).MKIWAPUUZA HAWATAREJEA HAPA KWANI WATAGUNDUA TUMEWASHTUKIA.....KUMBUKENI MAPAMBANO DHIDI YA JF YANAENDELEA,AND PART OF THE STRATEGY NI KU-DIVERT MIJADALA YA UFISADI HASA WA EPA/BOT
 
Masaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,464
Points
1,250

Masaki

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,464 1,250
naona KIngunge Mwiru angejieleza vizuri kuliko wewe! rudi chuoni kule kigamboni ufundishwe propaganda maana so far unaongea pumba tupu hapa!
Tatizo lako wewe kila anayempinga Mbowe basi anaongea pumba. Ila anayekosoa serikali basi huyo anaongea pointi. Mimi sio mwanasiasa na wala si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Nachangia kama Mtanzania.

Kwa bahati mbaya sana kuna watu humu wanaongea kwa ushabiki wa kisiasa zaidi kuliko uhalisia wa mambo yenyewe. Kwa kifupi hakuna kiongozi yeyote wa upinzani ninayemwamini mpaka sasa kwamba anatufaa! Hawana tofauti yoyote na walioko madarakani.
 
chinga

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2006
Messages
312
Points
0

chinga

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2006
312 0
Mada Ya Mbowe Kufeli Chuo Kikuu-hull Mmeifunga Wakati Nina Ushahidi Wote Hapa. Rudisheni Niweke Vitu Vya Huyu Kilaza.
Mwanaume Mzima Kakimbia Shule Yuko Kwenye Kitchen Party.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Naomba mnisamehe kama lugha yangu itakuwa si ya kistaarabu.Mnaowavuta na kuwalea hawa vibaraka wa mafisadi ni nyie mnaorefusha MADA ZINAZOONEKANA KABISA KUANZISHWA KAMA UTEKELEZAJI WA ASSIGNMENTS FLANI (za mafisadi).Busara nyepesi tu inaonyesha mtu sober akibishana na mlevi wote wanaonekana walevi.KWANI KUNA UGUMU GANI KUPUUZA?Reactions zenu kwa upuuzi wao zinawasafishia CV kwa hao wanaowatuma (it's like pay-per-click kwa mtu anayetuma spams).MKIWAPUUZA HAWATAREJEA HAPA KWANI WATAGUNDUA TUMEWASHTUKIA.....KUMBUKENI MAPAMBANO DHIDI YA JF YANAENDELEA,AND PART OF THE STRATEGY NI KU-DIVERT MIJADALA YA UFISADI HASA WA EPA/BOT
Mlalahoi,

katika siasa mambo kama haya yanategemewa na the best way to deal with them ni kuyaface moja kwa moja kila yanapojitokeza. Kwa wale walioko marekani wanakumbuka makosa aliyofanya John Keryy kwa kupuuzia udaku uliokuwa unaenezwa na swift boat guys kwa kudhani kuwa watu watapuuzia na alipokuja kushtuka akajikuta amechelewa kusafisha jina lake kwani watu wengi walikuwa wameamini huu uongo.

Huu ni udaku na mbinu za kumchafua Mbowe hasa baada ya kuuliza juzi kuwa ni kwa nini Kikwete anaficha majina ya "wanaorudisha" pesa? Hili linajulikana na habari za vikao vilivyokaa zimevuja.

Hapa JF tunawaambia kina Balile na wenzao kuwa tuko tayari na mapambano at the same time tukiendeleza libeneke mpaka Kikwete na wezi wenzake huko ikulu warudishe mabilioni ya mapesa ya waTZ

Hii nayo ngoja iwe hapa na wapambe wajue tu gharika la JF bado lipo na watakuwa confroted on their own faces.
 
chinga

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2006
Messages
312
Points
0

chinga

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2006
312 0
ASHA, HABARI YENYEWE NAONA NDO HII HAPA

13.03.2008 0947 EAT

Mbowe aifilisi NSSF
::Adaiwa milioni 1200, hataki kulipa
::Atumia sheria kukwepa asifungwe
::Adai iliyokopa ni kampuni si yeye

na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakalia kiasi kikubwa cha fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kukataa kulipa deni alilokopa.

Mbowe anadaiwa wastani wa sh milioni 1200 (sh bilioni 1.2), kutokana na deni alilochukua mwaka 1990 kwa nia ya kufanya upanuzi wa Mbowe Hotel ya jijini Dar es Salaam, maarufu kama Bilcanas.

Kwa kutumia mamilioni aliyokopa kutoka NSSF Machi 10, mwaka 1990, Mbowe aliweza kupanua Mbowe Hotel kwa kujenga mgahawa wa Hard Rock, kumbi za Bilcanas, Much More na Sugar Mama, ambazo amekuwa azitumia kwa ajili ya biashara tangu wakati huo.

Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa deni la mkopo huo aliouchukua kwa kutiliana saini kati yake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuwa NSSF, sasa limekua na kufikia zaidi ya sh milioni 1200. Deni hili linatokana na mkopo aliouchukua na riba inayotokana na deni hilo.

Wakati wa kuchukua mkopo huo NPF (wakati huo) iliwakilishwa na Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, huku Mbowe Hotel ikiwakilishwa Mbowe mwenyewe aliyetia saini. Pande zote mbili zilikuwa na mwakilishi mmoja. Mkulo kwa sasa ndiye Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo kati ya Mbowe na NSSF, ambayo ilichukua majukumu ya NPF, Mbowe Hotel ilikopeshwa sh milioni 15, mwaka 1990. Ibara ya 5, ya Mkataba wa Mkopo kati ya Mbowe Hotel na NSSF yenye vifungu 5.01, 5.02 na 5.03, iliweka bayana kuwa riba ya mkopo huo ilikuwa asilimia 31, na kwamba kila mwaka iwapo riba isingelipwa kwa wakati nayo ingetozwa riba ya asilimia 31.

Kifungu cha 6.01 na 6.02 cha mkataba wa mkopo huo kati ya Mbowe na NSSF vinaeleza kuwa Mbowe Hotel ilitakiwa kulipa deni hilo kwa mikupuo sawa mitano katika kipindi cha miaka sita. Mwaka wa kwanza wa mkopo Mbowe Hotel haikutakiwa kulipa kitu kwa nia ya kuipa fursa ya kujiimarisha katika biashara kwa mwaka wa kwanza.

Malipo hayo yalipaswa kufanyika kila ifikapo Desemba 31, kuanzia mwaka 1991, ambapo kila mwezi alistahili kulipa sh 3,000,000 kama deni la msingi na riba ya asilimia 31 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Manase A. Mbowe, Freeman Aikaeli Mbowe na Dk. Lilian Mtei Mbowe, kwa sababu wanazozijua wao waliamua kuacha kulipa deni hilo bila mawasiliano ya aina yoyote na NSSF wala juhudi za wazi za kuonyesha nia ya kulipa hadi mwaka 1993, walipoamua kulipa sh 3,000,000 kati ya deni lote.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, hadi mwaka 1993, wakurugenzi hao walistahili kuwa wamelipa wastani wa sh milioni 9,000,000 katika deni la msingi, lakini walikaa kimya hali iliyolitia wasiwasi shirika la NSSF.

Baada ya kutoa malipo ya sh 3,000,000, wakurugenzi hao walikaa kimya na ilipofika Septemba 1996, NSSF iliamua kufungua kesi Mahakama Kuu. Kesi hiyo ya madai No. 277 ya mwaka 1996, ilikuwa ikidai Mkopaji alipe deni la msingi sh milioni 12 zilizokuwa zimesalia pamoja na riba.

Hatua hii iliwafanya wakurugenzi wa Mbowe Hotel kuomba suala hilo walimalize nje ya Mahakama. Hata hivyo, hawakuendelea kulipa hadi mwaka 1998, walipopewa tishio la kufungwa jela ndipo waliamua kulipa kwa mkupuo sh milioni 12.

Hadi wanatoa malipo hayo, deni lilikwishakuwa na kufikia wastani wa sh milioni 145.38, na kimsingi makubaliano ilikuwa ni kwamba deni hilo lingelipwa katika muda wa miezi 24 tangua tarehe ya makubaliano.

Hata hivyo, Mbowe na wakurugenzi wenzake waliamua kutoendelea kulipa deni hilo badala yake wakaamua nao kuchukua mkondo wa kisheria kwa kutumia wahasibu kukokotoa tena hesabu za riba, bila mawasilianao na NSSF, na kisha wakachagua kiasi wanachotaka kulipa wao.

Mbowe Hotel ikitumia kampuni ya uwakili ya Nyange, Ringia & Co., walifanya kazi ya kuwasiliana na wahasibu mbalimbali kisha kuwasiliana moja kwa moja na wakili wa NSSF, Ademba Gomba, kutaka deni la riba lipunguzwe.

Mgogoro na mvutano kati ya Mbowe Hotel uliendelea, huku riba ya deni nayo ikizidi kuongezeka na ilipofika Oktoba 11, 2002 Meneja wa Fedha wa Bilcanas Group Inc, Godbless Naftal, kupitia barua yake yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL02/02/01, alikokotoa hesabu na kutaka wakurugenzi wa Mbowe Hotel walipe wastani wa sh 31,959,369.86, kwa maelezo kuwa kanuni iliyotumiwa kukokotoa riba ilikosewa.

Januari 16, 2003 NSSF kupitia kwa Mussa S. A. kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alimjibu Naftal kwa barua yenye Kumb. No. NSSF/LA/F.131/10/89/135, akimweleza kuwa NSSF imekataa mapendekezo yake (Naftal) na hivyo wanapaswa kulipa deni lote kwa mujibu wa hukumu ya za Mahakama Kuu za mwaka 1999 na 2001.

NSSF na Mbowe Hotel waliendelea kupigana ngwala mahakamani na kwenye bodi za usuluhishi hadi ilipofika Oktoba, 2006 ambapo Jaji Manento alihukumu wakurugenzi wa Mbowe Hotel watiwe mbaroni na kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kulipa deni lao.

Wakili wa Mbowe Hotel, Herbert Nyange, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufaa hati ya kiapo ambayo muhuri wake umegonjwa Oktoba 30, 2006 akipinga wakurugenzi wa Mbowe Hotel kukamatwa kwa maelezo kuwa Mahakama Kuu ilikwenda nje ya mipaka kisheria kwa kutaka wakurugenzi wakamatwe.

“Uamuzi wa amri ya kukamatwa kwa walalamikaji (wakurugenzi wa Mbowe Hotel) ulifikiwa kwa misingi ya wazi ya uvunjaji wa kanuni juu ya wajibu wa wakurugenzi dhidi ya deni au uamuzi dhidi ya shirika, hivyo ni kinyume na sheria,” alisema Nyange katika barua hiyo ya kupingwa kukamatwa kwa akina Mbowe.

Hata hivyo, kutokana na Mbowe kuona mambo yanaendelea kuchacha, Desemba 14, mwaka 2006, mmoja wa wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Dk. Lilian Mtei Mbowe, aliamua kutoa malipo ya wastani wa sh milioni 50 kwa NSSF kwa hundi mba 298492, iliyoambatana na barua yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL06/01, huku akitaka warejee kwenye meza ya majadiliano badala ya kufungwa jela.

Barua hiyo pia iliomba NSSF irejee barua ya Kampuni ya Ushauri wa Fedha ya Morgan cKlien Associates iliyoteuliwa na Mbowe mwaka 2004 kushiriki majadiliano na usuluhishi juu ya jinsi ya kulipa deni hilo.

Kampuni hiyo iliyokuwa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Hubert Mengi, ilitoa maelezo mengi yenye kuonyesha kwa nini Mbowe Hotel ilishindwa kulipa deni lake kwa wakati. Anasema katiak moja ya vielelezo kuwa fedha zilipotolewa na NSSF mwaka 1990, nchini Tanzania hakukuwapo vifaa vya ujenzi.Mengi anaeleza kuwa Mbowe Hotel walilazimika kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi, na lilijitokeza tatizo lingine kwamba benki nchini hazikuwa na fedha za kigeni, hivyo Mbowe Hotel ililazimika kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo za kigeni.

Kwa maelezo hayo, anasema Mbowe Hotel walichelewa kupata vifaa na mradi ukashindwa kukamilika kwa wakati hali iliyosababisha wakurugenzi wake washindwe kulipa deni hilo kwani walikuwa hawafanyi biashara.

Baada ya mivutano yote hiyo, Mbowe Hotel wamealikwa kwenye NSSF kujadili jinsi ya kulipa deni hilo linaloendelea kukua lakini hadi jana vyanzo vyetu kutoka NSSF vilionyesha kuwa wakurugenzi wa Mbowe Hotel wameamua kukaa kimya.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini.

© Habari Corporation Ltd
All rights reserved
http://www.newhabari.com/rai/habari.php?id=479&section=habari
DUUH JAMAA JIZI.
 
NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2007
Messages
560
Points
0

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2007
560 0
Mada Ya Mbowe Kufeli Chuo Kikuu-hull Mmeifunga Wakati Nina Ushahidi Wote Hapa. Rudisheni Niweke Vitu Vya Huyu Kilaza.
Mwanaume Mzima Kakimbia Shule Yuko Kwenye Kitchen Party.

Chinga, mada ilikaa hapa siku kibao, ukaingia mitini, leo imehamishwa, unakuja hapa kudai una ushahidi?

can you give us a break?
 
Asha Abdala

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2007
Messages
1,134
Points
0

Asha Abdala

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2007
1,134 0
Sasa tujiandae, vita ya wakubwa kwa wakubwa ndio imeanza. Ingawa imeanzia pembeni kwa Mbowe lakini inakuja polepole, wanaolengwa watafikiwa tu.
Hehee heeeeeeeeeee

Mustapha Mkulo aliyejichotea mamilioni NPF kuwa CCM kwa staili ya Deep Green kupitia kwa Kolimba.

Waanza kwa mkakati ule ule wa Rostam, Dr Slaa alipotaja orodha ya mafisadi, wakaanza kumwita mgoni na muuaji. Watu wakawapuuza, sasa kati ya Dr Slaa, Mkono na Rostam Aziz, nani anaheshimika?

Sasa baada ya Tanzania Daima, gazeti la familia ya Mbowe kumwanika Rostam Aziz na uwizi wake- sasa amemtuma mpishi wa habari bwana Balile amchafue bosi wake wa zamani kwa habari za kupindisha. Bahati nzuri nyaraka za kesi ziko wazi kwa umma, waandishi nendeni mahakamani mkaujue ukweli muwaumbue hawa habari cooperation.

Rostam usitumie kisingizio cha Mbowe kumhusisha Kikwete na ufisadi kupata kuungwa mkono na usalama wa taifa katika kiu yako ya kumchafua ujiepushe.

EPA na RICHMOND/DOWANS ni mizigo yako, ibebe! Tutakufungia tukupeke nayo huko kwenu ulipotoka

Balile, unakumbuka yaliyomkuta swahiba wako Lowassa? Sasa bwana(master) wako mpya naye yuko njiani.

Angalia habari yako ya kishabiki- NSSF imekopesha milioni 15 kwa Mbowe, vipi ifilisike kwa kiasi hicho tu kuchelewa kulipwa tena kutokana na kesi? Tena ukweli ni kuwa tayari Mbowe ameshatoa zaidi ya milioni 50.

Sasa tutajie madeni ya wale mabwana zako wengine NSSF, PSPF, Benki mbalimbali kwa dhamana ya BOT, tupe moja baada ya lingine.

Tueleze pia na ule mkopo wako ulilopewa kwa kimemo cha Lowassa, je rostam amekusaidia kulipa?

Asha
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Chinga, mada ilikaa hapa siku kibao, ukaingia mitini, leo imehamishwa, unakuja hapa kudai una ushahidi?

can you give us a break?
utawaweza hawa kwa kulialia? ile mada walianzisha kwa udaku na upuuzi ili ihamishwe waanze vilio vyao kama watoto wachanga kuwa vidali po vyao vimepotea.

Ikaachwa hapa na wao wakaingia mtini kama kawaida yao.. sasa leo hata hajui kuwa bado iko hapa JF... niliwaonya zamani kuwa hapa JF hakuna maziwa kwa watoto... warudi shule kwanza wasome maana inaonekana kuna watu walimiss elementary education zao ambako maziwa hutolewa bure shuleni...lol
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Points
0

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 0
Hehee heeeeeeeeeee

Mustapha Mkulo aliyejichotea mamilioni NPF kuwa CCM kwa staili ya Deep Green kupitia kwa Kolimba.

Waanza kwa mkakati ule ule wa Rostam, Dr Slaa alipotaja orodha ya mafisadi, wakaanza kumwita mgoni na muuaji. Watu wakawapuuza, sasa kati ya Dr Slaa, Mkono na Rostam Aziz, nani anaheshimika?

Sasa baada ya Tanzania Daima, gazeti la familia ya Mbowe kumwanika Rostam Aziz na uwizi wake- sasa amemtuma mpishi wa habari bwana Balile amchafue bosi wake wa zamani kwa habari za kupindisha. Bahati nzuri nyaraka za kesi ziko wazi kwa umma, waandishi nendeni mahakamani mkaujue ukweli muwaumbue hawa habari cooperation.

Rostam usitumie kisingizio cha Mbowe kumhusisha Kikwete na ufisadi kupata kuungwa mkono na usalama wa taifa katika kiu yako ya kumchafua ujiepushe.

EPA na RICHMOND/DOWANS ni mizigo yako, ibebe! Tutakufungia tukupeke nayo huko kwenu ulipotoka

Balile, unakumbuka yaliyomkuta swahiba wako Lowassa? Sasa bwana(master) wako mpya naye yuko njiani.

Angalia habari yako ya kishabiki- NSSF imekopesha milioni 15 kwa Mbowe, vipi ifilisike kwa kiasi hicho tu kuchelewa kulipwa tena kutokana na kesi? Tena ukweli ni kuwa tayari Mbowe ameshatoa zaidi ya milioni 50.

Sasa tutajie madeni ya wale mabwana zako wengine NSSF, PSPF, Benki mbalimbali kwa dhamana ya BOT, tupe moja baada ya lingine.

Tueleze pia na ule mkopo wako ulilopewa kwa kimemo cha Lowassa, je rostam amekusaidia kulipa?

Asha
Asha,

mimi niliwaonya wakati wanajiandaa kuanza kueneza huu udaku wa kuhusu mkopo wa Mbowe kuwa hii story itamgeukiwa Mkullo wao wakaleta yenge yenge nyingiiii!..

sasa hivi yangu macho tu... tik tak tik... nimekamata pop corn zangu maana zile story za Mkullo ndio zimepata pa kutokea na this time hadi Kikwete mwenyewe ndani ya nyumba...

I love jamboforum(s)
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,382,754
Members 526,462
Posts 33,836,634
Top