Je, Jeshi la Polisi linamkwamisha na kumgombanisha Rais Samia na Wananchi?

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Ni muda mfupi tu umepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan apokee taarifa ya Tume ya Haki Jinai na moja ya maeneo yaliyotajwa kama kinara kwa uozo na uovu ni Jeshi la Polisi hasa kitengo cha Usalama Barabarani.

Wakati Rais Samia akifanya jitihada za kuboresha mfumo wa utoaji haki, Kikosi cha Usalama Barabarani ambacho ni dhahiri kuwa kimeshindwa kupunguza ajali nchini kwani kiwango cha ajali kimeongezeka maradufu kimeacha kufanya majukumu ya msingi ya kuokoa roho za Watanzania badala yake wamejikita katika masuala yasiyo na tija hata kidogo.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo imeeleza kuwa Jeshi hilo LIMESISITIZA KUWA
litaendelea kuwakamata madereva wa magari wanaoweka ‘tinted’ kwenye taa za magari pamoja na wote wanaoweka namba aina ya 3D kwenye magari.

Yaani katika matatizo yote tuliyonayo huko barabarani, ndugu zetu hawa wameamua kutumia mishahara yao inayotokana na kodi zetu, eti kufuatilia namba za 3D, ni kitu gani hasa kinawawasha kwa wenye magari yao kuamua kuwa na namba za 3D au kuweka tinted kwenye taa kwa lengo la kusaidia taa zisiharibike kwa ukungu.

Lakini kama nia yao ilikuw ni njema na sio kuleta taharuki na kuwafanya wananchi wailaumu na kuichukia Serikali kwanini hawakutoa TAARIFA kwa umma kuwataka wananchi kuondoa vitu hivyo tena huku wakiainisha sheria iliyovunjwa? Wao wamechagua tu kuingia barabarabi na kuandika faini.

Pamoja na hayo yote, suala la "kishenzi" kabisa (Ashakum si matusi) ni hili la kuwapiga picha wananchi wakiwa wanabandua hizi stika au 3D na kuzisambaza mtandaoni, hili ni tendo la kukemewa na kupingwa kwa nguvu zote.

Jeshi la Polisi lilikuwa wapi wakati hizi kampuni za kuweka 3D zinasajiliwa, zinapewa leseni na kuanza biashara tangu magari yakiwa namba D za mwisho mpaka leo tuko namba ED za mwisho, je walizibwa mdomo? ilikuwa ni dili la mkubwa? au vipi? maswali ni mengi sana.

Kama ilivyopendekezwa na tume ya haki jinai, Jeshi la Polisi liachane na hili suala la kujifanya na wao wanakusanya mapato kama TRA, muda wote wako na mashine kazi yao kuandika faini kwani kufanya hivyo nadhani ni sawa na kumgombanisha Rais Samia na Wananchi anaowaongoza.
 
Kazi Za Kufanya Hawana Bila Shaka Lakini Hii Nayo Ni Aibu Sana Kwa Geshi
 
Hangaya hana akili!

Ona mafuta leo yamepanda na kila kituo sasa yapo wakati jana walikuwa wanasema yameisha!
Yeye yupo tu!

Bure kabisa!
 
Jeshi la police linatakiwa liundwe upya kabisa ikiwa ni pamoja na kuondoa neno force na kuwa service, inabidi tuwe na special units within police service, Mara poor of the poorest wamepoteza maisha because hatuna vikosi maji ndani ya jeshi la police, mikoa yote yenye maeneo yenye maji ilitakiwa tuwe na vikosi hivi, sasa wale walala hoi wanawategemea wavuvi wenye zana duni kuongoza uokoaji!,vitu vya ajabu mno,from Dar hadi Morogoro ni 200km,nimehesabu check points, zilikua 15!!!,zote hizi za nini, ni rushwa,rushwa rushwa kila check point
 
Ni muda mfupi tu umepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan apokee taarifa ya Tume ya Haki Jinai na moja ya maeneo yaliyotajwa kama kinara kwa uozo na uovu ni Jeshi la Polisi hasa kitengo cha Usalama Barabarani.

Wakati Rais Samia akifanya jitihada za kuboresha mfumo wa utoaji haki, Kikosi cha Usalama Barabarani ambacho ni dhahiri kuwa kimeshindwa kupunguza ajali nchini kwani kiwango cha ajali kimeongezeka maradufu kimeacha kufanya majukumu ya msingi ya kuokoa roho za Watanzania badala yake wamejikita katika masuala yasiyo na tija hata kidogo.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo imeeleza kuwa Jeshi hilo LIMESISITIZA KUWA
litaendelea kuwakamata madereva wa magari wanaoweka ‘tinted’ kwenye taa za magari pamoja na wote wanaoweka namba aina ya 3D kwenye magari.

Yaani katika matatizo yote tuliyonayo huko barabarani, ndugu zetu hawa wameamua kutumia mishahara yao inayotokana na kodi zetu, eti kufuatilia namba za 3D, ni kitu gani hasa kinawawasha kwa wenye magari yao kuamua kuwa na namba za 3D au kuweka tinted kwenye taa kwa lengo la kusaidia taa zisiharibike kwa ukungu.

Lakini kama nia yao ilikuw ni njema na sio kuleta taharuki na kuwafanya wananchi wailaumu na kuichukia Serikali kwanini hawakutoa TAARIFA kwa umma kuwataka wananchi kuondoa vitu hivyo tena huku wakiainisha sheria iliyovunjwa? Wao wamechagua tu kuingia barabarabi na kuandika faini.

Pamoja na hayo yote, suala la "kishenzi" kabisa (Ashakum si matusi) ni hili la kuwapiga picha wananchi wakiwa wanabandua hizi stika au 3D na kuzisambaza mtandaoni, hili ni tendo la kukemewa na kupingwa kwa nguvu zote.

Jeshi la Polisi lilikuwa wapi wakati hizi kampuni za kuweka 3D zinasajiliwa, zinapewa leseni na kuanza biashara tangu magari yakiwa namba D za mwisho mpaka leo tuko namba ED za mwisho, je walizibwa mdomo? ilikuwa ni dili la mkubwa? au vipi? maswali ni mengi sana.

Kama ilivyopendekezwa na tume ya haki jinai, Jeshi la Polisi liachane na hili suala la kujifanya na wao wanakusanya mapato kama TRA, muda wote wako na mashine kazi yao kuandika faini kwani kufanya hivyo nadhani ni sawa na kumgombanisha Rais Samia na Wananchi anaowaongoza.
Tumeshaagombana naye mda tu kwa kushindwa kuchukua hatua kwa baaddhi ya mambo yanayoenda ndivyo sivyo
 
Back
Top Bottom